Mwenyekiti na Mwanzilishi wa BTA wa kisura Tanzania,Juliana Urio (kati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo asubuhi ndani ya New Afrika Hotel kuhusiana na mchakato mzima wa shindano la Kisura Tanzania.
========= =========== ==========
MCHAKATO wa kumpata Kisura wa Tanzania 2010/11, unatarajia kuanza Desemba 11 mwaka huu mkoani Mwanza. Huu utakuwa ni mwaka wa tatu (3) tangu mradi huu ulipoanza mwaka 2007.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti na mwanzilishi wa kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), Juliana Urio alisema hatua ya kwanza ya usahili huo, mbali na Mkoa wa Mwanza, pia itahusisha mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora na Dar es Salaam, Arusha, Karatu, Dodoma, Iringa, Mbeya na Songea.

Alisema kuwa timu ya BTA ikiambatana na Mwanamitindo chipukizi Kemmy Kalikawe wanatarajiwa kuondoka jijini Dar es Salaam, Desemba 10 kwenda Mwanza kuanza usahili huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake.

Alisema kuwa mbali ya mchujo kwa wasichana wenye sifa zinazotakiwa (uferu sentimita174, mapaja 36, kiuno 27, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27) katika shindano hilo, pia wasichana hao watakaoshiriki kwenye mchujo watapewa mafunzo juu ya janga la Ukimwi.

Ms. Urio alisema kuwa mchujo kwa wasichana wa Mwanza utafanyika Desemba 11 hadi 12 katika hotel ya Stone Town, Mwanza Hotel

kabla ya usahili huo kuhamia Musoma (Mara) ambapo watafanya mchujo Desemba 13 hadi 14 katika hoteli ya Mativila.

“Desemba 15 itakuwa ni zamu ya wasichana wa mkoani Kagera ambapo mchujo utafanyika kwa siku moja na Desemba 16 Timu ya BTA itaelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuendelea na usahili huo katika hoteli ya Ibaza hoteli,” alisema Ms. Urio.

Aliongeza: “Desemba 17 timu ya BTA itaelekea mkoani Tabora kuendelea na mchujo huo katika Club Royal na baada ya hapo msafara huo utarejea Dar es Salaam kwa ajili ya usahili huo utakaofanyika jijini humo kwa siku mbili, yaani kuanzia Desemba 19 hadi 20 siku ambayo ndiyo mwisho wa hatua ya kwanza ya usahili huo.”

Ms. Urio alisema kuwa hatua ya pili ya usahili huo (Phase II), itafanyika katika mikoa ya Arusha, Karatu na Dodoma kuanzia Desemba 21 hadi 29.

Alisema kuwa Desemba 22 mchujo huo utaanzia katika Mkoa wa Arusha na usahili utafanyika kwenye hoteli ya Via Via na utafanyika kwa siku mbili kabla ya kuhamia Dodoma Desemba 27 hadi 29 kwenye Hotel ya Dear Mama , hiyo ikiwa ndiyo mwisho wa hatua ya pili.

Alisema kuwa hatua ya tatu ya mchakato huo itahusisha mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma. Kuanzia Januari 2 hadi 4 mwaka 2011 watakuwa Mkoa wa Iringa na usahili ufatanyika Twisters Club.

“Januari 4 msafara wa BTA utahamia Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya mchujo utakaofanyika kwa siku moja na kwamba Januari 6 usahili huo utahamia mjini Songea, mkoani Ruvuma ambapo utafanyika kwa siku moja pia.

“Januari 8, 2011 itakuwa ndio mwisho wa mchakato huo wa mchujo wa kumtafuta Kisura wa Tanzania 2010/11. Ms. Urio alisema usahili huo utaonyeshwa katika kituo cha Televisheni cha TBC1.

Aliongeza: “Fainali za mashindano hayo yanatarajiwa kuwa Machi 2011 katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.”

Taji la Kisura wa Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Diana Ibrahim kutoka Mkoa wa Mara.

Ms. Urio aliongezea akisema, pamoja na kuwa shindano zima linahusu kumtafuta mwanamitindo (model) ambaye ataiwakilisha nchi yetu ndani na nje vile vile lengo kuu la shindano la Kisura wa Tanzania ni:-

· Kuwajengea uwezo watoto wa kike kwenye kiwango cha uelewa na kujitambua katika mabadiliko ya tabia, kwa kuwapa elimu iliyopo katika mfumo rasmi (shuleni) na ile iliyopo nje ya mfumo rasmi;

· kuwafundisha masuala ya uzazi, afya, pamoja na jinsi ya kujikinga na magonjwa hasa ugonjwa wa ukimwi;

· kuwafundisha ujasiriamali ili waweze kuwa vinara wa mabadiliko katika maisha yao na kwa taifa zima kwa ujumla;

· kuwajengea uwezo katika masuala ya uongozi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.

Ms. Urio aliendelea akisema, Shindano la Kisura linawatumia wanamitindo kama nyenzo ya kuelimisha na kufikisha ujumbe kwa jamii ya kitanzania.

Mdhamini mkuu wa shindano la Kisura wa Tanzania 2010/11 ni Family Health International (FHI), na wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort Hotel, TanFoam (Arusha), SBC Tanzania Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA na GRM Production.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa hapa Dar auditions zitafanyikia wapi? Asante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...