KUMBUKUMBU
Marehemu Mzee Joakim Daudi Henjewele
Mwaka mmoja sasa umetimia tangu Mpendwa wetu utuache katika majonzi mazito ulipoenda kuungana na yeye aliyekuumba. Sisi watoto wako tulio Luilo, Manda, Iringa, Dar Es Salaam, na nje ya Tanzania; pamoja na dada zako, wajukuu na vitukuu vyako, na ndugu wote kwa pamoja tunakukumbuka kwa mengi uliyoyafanya katika uhai wako.
Pengo uliloliacha kamwe halitazibika; bali kwa neema za Mwenyezi Mungu tunalipokea na kujifunza kulizoea. Tunamwomba Mwenyezi Mungu aliyekujalia hekima, ujasiri, na mapendo makubwa vile; akupe pumziko la milele mbinguni, na kukuangazia mwanga wa daima.
- Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...