TANGAZO LA MKUTANO WA BALOZI
NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI SWEDEN
Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mheshimiwa Muhammed Mzale atakutana na Watanzania waishio nchini Sweden siku ya Jumamosi tarehe 11 Disemba 2010 kuanzia saa tisa alasiri katika ukumbi wa Kista Träff uliopo kwenye anwani ifuatayo:
Kista Torg 7
164 42 Kista
Stockholm
Watanzania mnaombwa mjitokeze kwa wingi ili mpate fursa ya kufahamiana na kujumuika na Mheshimiwa Balozi kwenye mkutano huu ambao pia utatumika kama sehemu ya sherehe ya miaka 49 ya uhuru.
Tafadhali mnaombwa sana kuzingatia muda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...