Ankal naomba nafasi kutoa mchango katika blog ya jamii ambao naamini utawasaidia washiriki wetu wa tusker project fame kwani ni watu wengi wataliona hili kosa endapo litawekwa kwenye hii blog ya jamii.

Watanzania tunalaumiwa kwa kutopenda kutoa support katika mambo ya maendeleo ya Watanzania wenzetu lakini mara nyingine tunapata maelekezo yasiyo sahihi au watu hawahamasishwi vya kutosha.

Katika suala la Tusker project Fame nafikiri Leah ametoka si kwa sababu watu hawakutaka kumpigia kura ila kwa sababu watu wengi walishindwa kupiga kura kutokana na maelekezo yasiyo sahihi.

Kuna makosa yanayosababishwa na Watangazaji wa vyombo vyetu vya habari katika kuelezea jinsi ya kuwapigia kura hasa jinsi ya kuandika ule ujumbe mfupi wa maneno.

Mtu hatakiwi kuacha nafasi baada ya kuandika neno “tusker”(mfano “tusker 3” kwa Leah) bali ile tusker inaunganishwa moja kwa moja na namba ya mshiriki bila kuacha nafasi(yaani “tusker3). Vyombo vyetu vya habari vinatangaza kwamba “andika neon tusker, uache nafasi halafu uandike namba ya mshiriki utume 15522”.

HII SIYO SAHIHI! USIACHE NAFASI BAADA YA KUANDIKA NENO TUSKER. Naamini watu walishindwa kumsaidia dada yetu ambaye tunaamini kwamba angeenda mbali sana kwenye shindano hili kwani ana kipaji cha hali ya juu ukilinganisha na hausimeti wake waliobaki.

Baada ya kufuata maelekezo haya nilishindwakumpigia kura lakini nilipotuma bila kuacha nafasi nilifanikiwa kumpigia kura 4 ambazo naamini kama 10% ya Watanzania wangepiga tungemvusha.

Tuwape support vijana wenzetu kwani kwa namna nyingine wanaleta manufaa si kwa familia zao tu bali kwa Watanzania wote kama Taifa. Bila kusahau kwamba watoto wetu wanajifunza kutoka kwao jinsi ya kuzingatia malengo yao kama ambavyo hawa vijana wanafanya.

Hivyo kama mmoja wao akishinda basi inakuwa kuwapa changamoto watoto wetu na hata sisi wenyewe katika kushindana kimataifa hata katika kazi, uongozi na biashara.

Ni hayo tu Ankal ila jina langu kapuni plz.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kama maelezo haya ni sahihi, basi hata TBC1 wamekosea kutoa muongozo na hivyo Msechu atakosa kura nyingi!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. THIS IS MISLEADING STUFF

    ReplyDelete
  3. TUSKER 9 to 15522 period!

    ReplyDelete
  4. Kuna watangazaji wengine TBC mambo haya ya burudani yamewapita kushoto kabisa. Eti leo kwenye habari asubuhi (around saa mbili asubuhi hivi) mtangazaji kasema Lady Gaga ni mwanamuziki wa Uingereza. Nikacheka sana.

    ReplyDelete
  5. This is misleading. I have sent "Tusker 9" to 15522 and got confirmation that my vote shall be counted.

    ReplyDelete
  6. mkandamizajiNovember 24, 2010

    mbona hilo tangazo la tusker hapo juu lina nafasi kabla ya 9?

    isije ikawa wewe ndio unatu-mislead mjomba tutakutafuta tukupate tuu maana ankal anwani na jina lako anavyo, tanzania ndogo hii ohoooo!.....

    ReplyDelete
  7. WEWE ndio unatuchanganya mie nishatuma sms kumpigia Leah, Aneth na pia kwa msechu na nikarudishiwa ujumbe unasema Thankyou for voting for Msechu kwa kuandika (Tusker 9 natuma kwenda 15522)iyo yako ni ya wapi isijekuwa wewe ndio unakosea chunga sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...