MAMA ASHA BILAL AFUNGUA MAONYESHO
YA KAZI ZA WAKE WA MABALOZI DAR
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua rasmi maonyesho ya kazi za wake wa Mabalozi, yaliyoandaliwa na Kikundi cha wake wa Mabalozi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki jijini Dar es Salaam leo
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akipokea zawadi ya mpira uliokuwa na ujumbe usemao USIMPIGE MWANAMKE PIGA MPIRA’. kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Wake wa Mabalozi, Anne Clarke, wakati alipoalikwa kufungua maonyesho ya kazi za Wake Mabalozi, ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watu wasiojiweza na NGO’s, yaliyoandaliwa na kikundi hicho na kufanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki Jijini Dar es Salaam leo
Mama Bilali akiwa banda la Norway
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akiangalia bidhaa za Vitenge vya Nigeria katika Banda la Nigeria wakati wa Maonyesho ya Kazi za Wake wa Mabalozi yaliyoandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, yaliyofanyika Shule ya Tanganyika International Masaki Jijini Dar es Salaam leo Nov 2o. Kushoto ni Wabunge wa Viti Maalum, Zainab Vullu na Halima Mamuya
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akikagua bidhaa katika banda la Namibia, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya kazi za Wake wa Mabalozi, yaliyoandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza. Maonyesho hayo yalifanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki Jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na mdau Muhidin Sufiani

Way to go My sister! you look great!
ReplyDeleteAnd she is fluent in English and French!
ReplyDeleteKwa hivyo usicheze na huyo mama.