Align CenterNdugu Emanuel Reginald Kapongo

Jumuiya ya Watanzania Italy sasa ina uwakilishi wake Tanzania. Ndugu Kapongo pichani ameteuliwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italy ndugu Abdulrahaman A.Alli kuwa muwakilishi (Represantative) wa Watanzania wanaoishi Italy.

Ndugu Kapongo amerejea Tanzania wiki iliyopita baada ya kufanya ziara fupi makao makuu ya jumuiya ya Watanzania Italia mjini Napoli. Katika ziara yake alipata wasaa wa kuzungumza na watanzania waliofika katika sherehe ya tawi la Chama cha Mapinduzi la Napoli zilizofanyika tarehe 6/11/2010.

Muwakilishi huyo ameahidi kushirikiana na Watanzania wote wanaoishi Italy katika masuala yote hata ya binafsi.Wengi wa watanzania wanaoishi ughaibuni huwa ni kawaida kuhusisha ndugu zao katika masuala yao kama ya ujenzi na mara nyingi huwa hawatendewi haki au kuambiwa ukweli,ndugu Kapongo atakuwa akifuatilia nakujuwa taarifa kama hizo.

Jumuiya ya Watanzania Italy inafungua Darasa la kufundisha lugha ya kitaliani mjini Daressalaam ili kuwaanda wanafunzi au wafanyakazi wanaotegemea kwenda Italy au kwa yeyote atakaye penda kujifunza lugha ya kitaliani.

Ofisi ya muwakilishi huyo ipo Dar es Salaam mtaa wa Rufiji/Nyamwezi.
Kwa mawasiliano na ndugu Kapongo piga simu.
tel. +255 22 2180971 cell.
(+255) 0713 382428.

au andika barua pepe kwa
katibu mkuu wa Jumuiya-
tnzncommunity@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mwenyekiti. Haya ndo mambo yanayotakiwa.

    Suti ya mwenyekiti si mchezo. Lazma utokwe na jasho ukiivaa.

    ReplyDelete
  2. kufutiana ulaji tuu

    ReplyDelete
  3. vichekesho munoooooo.this is ridiculous yaaani diaspora wetu mnahitaji mwakilishi nyumbani kwenu Tanzania..stupid. Mwakilishi wenu kwa nani..huko Italy mnakuwa na mwakilishi ili aweze kuratibu mambo yenu wenyewe na kuyawakilisha katika ubalozi wenu huko ambao ndiyo serikali yenu kuratibu mambo yoote kwa kuwa mko mbali na nyumbani. Sasa mna mwakilishi Tanzania...hiyo kichwa yenu iko tatizo...

    ReplyDelete
  4. Really? Whats the point? Absurdity at its best.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...