Balozi wa Tanzania nchini Japani Mh. Salome Sajaona leo amepongeza uamuzi wa Chuo Kikuu cha Soka cha nchini Japan kwa kutambua umuhimu wa kuienzi lugha ya Kiswahili nchini Japani na hasa katika Chuo kikuu hicho.
Akizungumza wakati wa mashindano ya kutoa hotuba ya Kiswahili kuwania tuzo la mwasisi wa Chuo cha Soka, Bwana Daisaku Ikeda, Balozi Salome alisema lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha muhimu duniani na inatumika kama chombo cha mawasiliano na katika Afrika Mashariki Kiswahili ni lugha ya upendo, amani, mshikamano na umoja, akitolea mfano wa Tanzania ambako imeweza kuunganisha makabila zaidi ya 120.
Ujumbe wa mwaka huu katika mashindano hayo ilikuwa: "Kutoka Japani, tusambaze mbegu za amani kote duniani; nuru ya jua inamaanisha nini kwangu mimi?"
Balozi Salome alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanachuo wa Soka kuendelea kujifunza Kiswahili na kufanya ziara katika nchi za Afrika Mashariki ambalo ndiko chimbuko la Kiswahili ili kujiimarisha zaidi katika lugha hii.

Wajapani wanaendeleza lugha ya Kiswahili wakati BAKITA, Idara za lugha Mlimani, wizarani Bongo waheshimiwa wamelala usingizi mzito, utafikiri nchi haina wenyewe!!!
ReplyDeleteMsaada tutani!......Chuo kikuu cha "SOKA" ! naomba ufafanuzi, soka mpira au soka jina?
ReplyDeleteinapendeza na inafurahisha!kwa dizaini hii lugha kiswahili inakuwa juu hongera sana.
ReplyDeleteDo you want to learn swahili? visit our website www.swahilitrainers.com
ReplyDeleteKaribu
"Balozi Salome alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanachuo wa Soka kuendelea kujifunza Kiswahili na kufanya ziara katika nchi za Afrika Mashariki "
ReplyDeleteJamani Balozi Sijaona wewe unawakilisha Tanzania upo kwa ajili ya Maslahi ya Tanzania sasa kwanini Unasema waje Afrika Mashariki badala ya kuwa specifically kuwa waje Tanzania?? Ndio, Tanzania ni kati ya nchi za Afrika Mashariki sasa tusipowatajia wataenda Kenya. Tuwe tunapenda kuitaja Tanzania.