Balozi wa Tanzania nchini Japani Mh. Salome Sijaona akimkabidhi kombe Bi. Tomomi Kosugi baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya 20 ya kutoa hotuba kwa lugha ya Kiswahili ya kuwania tuzo la mwasisi wa Chuo Kikuu cha Soka cha nchini Japani Bw. Daisaku Ikeda.
Mdau Anna Kwambaza wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani akichati na baadhi ya wadau wa lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Soka.
Francis Mossongo, Afisa ubalozi wa Tanzania nchini Japani na Raphael Mwenda, Afisa ubalozi wa Congo-DRC katika mnuso pamoja na wadau wa Kiswahili chuo cha Soka.
Baadhi ya washiriki wa shindano hilo la Kiswahili wakipiga makofi mara baada ya mmoja kati yao kutangazwa ni mshindi.

Balozi wa Tanzania nchini Japani Mh. Salome Sajaona leo amepongeza uamuzi wa Chuo Kikuu cha Soka cha nchini Japan kwa kutambua umuhimu wa kuienzi lugha ya Kiswahili nchini Japani na hasa katika Chuo kikuu hicho.

Akizungumza wakati wa mashindano ya kutoa hotuba ya Kiswahili kuwania tuzo la mwasisi wa Chuo cha Soka, Bwana Daisaku Ikeda, Balozi Salome alisema lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha muhimu duniani na inatumika kama chombo cha mawasiliano na katika Afrika Mashariki Kiswahili ni lugha ya upendo, amani, mshikamano na umoja, akitolea mfano wa Tanzania ambako imeweza kuunganisha makabila zaidi ya 120.

Ujumbe wa mwaka huu katika mashindano hayo ilikuwa: "Kutoka Japani, tusambaze mbegu za amani kote duniani; nuru ya jua inamaanisha nini kwangu mimi?"

Balozi Salome alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanachuo wa Soka kuendelea kujifunza Kiswahili na kufanya ziara katika nchi za Afrika Mashariki ambalo ndiko chimbuko la Kiswahili ili kujiimarisha zaidi katika lugha hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wajapani wanaendeleza lugha ya Kiswahili wakati BAKITA, Idara za lugha Mlimani, wizarani Bongo waheshimiwa wamelala usingizi mzito, utafikiri nchi haina wenyewe!!!

    ReplyDelete
  2. Msaada tutani!......Chuo kikuu cha "SOKA" ! naomba ufafanuzi, soka mpira au soka jina?

    ReplyDelete
  3. inapendeza na inafurahisha!kwa dizaini hii lugha kiswahili inakuwa juu hongera sana.

    ReplyDelete
  4. Do you want to learn swahili? visit our website www.swahilitrainers.com
    Karibu

    ReplyDelete
  5. "Balozi Salome alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanachuo wa Soka kuendelea kujifunza Kiswahili na kufanya ziara katika nchi za Afrika Mashariki "
    Jamani Balozi Sijaona wewe unawakilisha Tanzania upo kwa ajili ya Maslahi ya Tanzania sasa kwanini Unasema waje Afrika Mashariki badala ya kuwa specifically kuwa waje Tanzania?? Ndio, Tanzania ni kati ya nchi za Afrika Mashariki sasa tusipowatajia wataenda Kenya. Tuwe tunapenda kuitaja Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...