




MATOKEO RASMI YALIYOTANGAZWA LEO
1. KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO: 96, 933 (1.12%)
2. KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM: 5,276,827 (61.17%)
3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA: 2,271,941 (26.34%)
4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF: 695,667 (8.067%)
5. RUNGWE HASHIM SPUNDA/NCCR-MAGEUZI: 26,388 (0.31%)
6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT/TLP:17,482 (0.20%)
2. KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM: 5,276,827 (61.17%)
3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA: 2,271,941 (26.34%)
4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF: 695,667 (8.067%)
5. RUNGWE HASHIM SPUNDA/NCCR-MAGEUZI: 26,388 (0.31%)
6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT/TLP:17,482 (0.20%)
7. DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA/UPDP: 13,176 (0.15%)
----------------------------------------------
WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303
WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)
KULA HALALI ZILIZOPIGWA: 8,398,394
KURA ZILIZOHARIBIKA 227,889 (2.64)
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ( NEC), Jaji Mstaafu, Lewis Makame leo jioni amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa Tanzania wa mwaka 2010 kuwa ni Ndugu Jakaya Kikwete kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM).
Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yalitangazwa leo majira ya saa kumi jioni na Mwenyekiti huyo katika viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji Mstaafu , Makame alisema kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote.
Aidha Makame alisema kwa mujibu wa ibara ya 47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais akichaguliwa basin a mgombea mwenza wake atakuwa Makamu wa Rais.
“Kwa kuwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM amepata kura yingi kuliko mgombea yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35E, 35F (8) na 81 B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2010.
“Mheshimiwa Kikwete Jakaya Mrisho amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Bilal Mohammed Gharib amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 20,137,303, waliopiga kura ni 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha, zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni sawa na asilimia 2.64 ya kura zilizopigwa.
Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni 8,398,394 sawa na asilimia 97.36 ya kura zote zilizopigwa, hivyo Kikwete amepata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote halali.
Wagombea waliofuatia ni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye ni Slaa Willibrod Peter amepata kuwa 2,271,941 ambazi ni sawa na silimia 26.34 ya kura zote halali, Lipumba Ibrahim Haruna wa chama cha CUF, amepata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06 ya kura zote halali, Mziray Kuga Peter wa APPT – Maendeleo amepata kura 96,933 sawa na asilimia 1.12 ya kura zote halali.
Wengine ni Rungwe Hashim Spunda wa NCCR- MAGEUZI amepata kura 26,388 sawa na asilimia 0.31 ya kura zote halali, Mgaywa Muttamwega Bhatt wa TLP amepata kura 17,482 sawa na silimia 0.20 na Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa wa UPDP amepata kura 13,176 sawa na asilimia 0.15 ya kura zote halali.
Akitoa salamu kwa niaba ya wenzake badala ya Slaa ambaye hakuwepo uwanjani hapo, Lipumba alimpongeza Kikwete na Makamu huku akisisitiza suala ya ushiriki wa watu katika kupiga kura liangaliwe na kusema Rais aliyeshinda ni Watanzania wote.
Alisisitiza suala la elimu bora , ajira, ujengaji wa miundombinu na uvumulivu wa kisiasa ni muhimu, hivyo alimshauri Rais Mteule Kikwete kujiwekea malengo katika kipindi cha miaka 5 ijayo, ambayo ni uongozi wa demokrasi, ujenzi wa uchumi ajira kuboresha miunbombinu, utawala na kupamban na rushwa.
Pia alimkabidhi Rais Mteule Kikwete Ilani ya chama chake kwa ajali ya kusaidia katika utendaji wake wa kazi.
Kwa Upande wake Rais Mteule Kikwete, alitoa shukura za ushindi alioupata na kusema watazifanyia kazi changamoto zilizibuliwa wakti wa kampeni yakiwemo mawazo ya Lipimba.
Alivishukuru vyombo vya habari kwa tendaji wao wa kazi , lakini aliviomba kufanmya kazi zaidi ya kusaidia kutibu majeraha ya nchi ili kurejesha umoja na amani badala ya kuongeza chumvi.
Naye Dovutwa alisema sasa ni wakti wa kumsaidia Rais Mteule kujenga nchi malumbano yamekisha.
Mziray amesema hajakata tama ananjiandaa kwa baade , huku Muttamwega alisema matokeo yameenda vizuri.
Yaani na kuchakachuliwa kote huko bado asilimia ndiyo hiyo. Mhh ama kweli mwaka huu kazi ilikuwepo, ndio maana hata wale waliokuwa wanayasoma, nyuso zao zilionesha kabisa nafsi zao zinawasuta, kwa maana nyingine, nafsi, nyuso na midomo yao vilikosa ushirikiano. All the best najuo utaitia kapuni lakini message sent and delivered maana najua ili itiwe kapuni lazima isomwe kwanza
ReplyDeleteToka Asilimia 80% mpaka asilimia 60% naona tumeenda nyuma hatua tano. Mkapa alianza na asilimia 56% mwaka 1995 akapanda mpaka 75% mwaka 2000. Hapa tumeenda nyuma tena sana. Somo la kujifunza kwa chama Changu cha Mapinduzi. Bila CCM Madhubuti nchi itayumba, hayo ni maneno ya Mwalimu Julius Nyerere.
ReplyDeleteKURA ZIMEIBIWA SANA. KWA MTAZAMO WANGU NA NILIVYOKUWA NAFUATILIA CCM HAKUPATA ZAIDI YA 51% CHADEMA SIO ZAIDI YA 38% LIPUMBA SIO ZAIDI YA 8% ZILIZOBAKI NI ZA VYAMA VILIVYOBAKI.HUO NDIO UKWELI
ReplyDeleteONGERA MH.JAKAYA MLISHO KIKWETE KWA KUTEULIWA KUWA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.
ReplyDeleteYay!!!CCM oyeeeeeeeee!!!Kila la kheri Rais Kikwete kwa miaka 5 ijayo.
ReplyDeleteHongera JK. Sasa tukajenge nchi!
ReplyDeleteCCM.CCM,CCM JUU.ONGERA MH.KWIKWETE WASEMA OVYO NA WAENDELEE KUSEMA.UKWELI NDIO HUO NA RAIS LEO NDIO TUMEMJUA ONGERA BAB KAZA BUTI KATIKA KUTUONGOZA,TANZANIA SIKU ZOTE NI KISIWA CHA AMANI.MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA.ALL THE BEST
ReplyDeletenani ajuaye Kikwete yu mwene.ALL THE BEST atatukisema ukweli utabaki kuwa ndio huo huo,Uchaguzi umekwisha salama so tofauti zetu tuziache na tusonge mbele.Mungu ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Africa.
ReplyDeleteHabari ndiyo hiyooooooooooooooooo.Hakuna zaidi ya KIKWETE CCM JUUUUUUUUUUUUU,KIKWETE JUUUUUUUUUUUUU.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA
ReplyDeleteWatu wenye thinking capacity ndogo huzungumza mambo ambayo hawatotoa ushahidi wakitakiwa kufanya hivyo. Suala la kujiuliza ni kwa nini idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni ndogo kuliko waliojiandikisha? kwa nini nchi inao zaidi ya watu milioni 25 wenye sifa za kupiga kura lakini hawakujiandikisha? sio kuleta propaganda za Dr Silaha katika kila jambo, tutulie tuangalie miaka 5 ijayo tufanye nini?
ReplyDeleteKK
Magamba Coast.
MATOKEO NDIO HAYO ASIYEKUBALI KUSHINDWA SI MSHINDANI CONGRATUATION HON.JAKAYA.MUNGU IBARIKI AFRICA,MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDeleteHongeraa Dr. Slaa! mwaka 2015 kazi ni kulinda kura za majimbo yote
ReplyDeleteWATANZANI SASA TUMALIZE TOFAUTI ZA VYAMA NA TUNACHOTAKIWA TUENDELEE NA YANAYOKUJA MBELE YETU.TUMELIDHIKA NA MATOKEO TULIYOSOMEWA MUDA MFUPI ULIYOPITA.HATA TUKIBISHA HABARI NDO HIYO.TUNAIOMBEA NCHI YETU AMANI NA UPENDO DAIMA .MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA
ReplyDeleteEhee hasira itakayotoka hapo tutajitu. watu wengine kisasi ni nje nje!
ReplyDeleteCCM OYEEEEEEEEE KIKWETE KAZA BUTI TUNATAKA MAENDELEO NDANI YA MIAKA MITANO
ReplyDeleteDuh tumesubiri wee utafikiri uzazi wa mimba ya kwanza, lakini hatimaye matokeo yametolewa na mshindi amejulikana.
ReplyDeleteHongera sana JK mungu akulinde na husda na roho mbaya zao. Akujaalie afya njema na umuri ili uweze kutekeleza yale uliyoyaahidi. Na hiyo mwaka 2015 tunamsubiri mwingine tena agalagazwe kama alivyogalagazwa mchangani Dr Slaa, tofauti ya kura ni kubwa sana. JK umeshinda kwa nguvu na uwezo wake manani, maana alikupangia Mola mwanadamu hawezi kulifuta. Tunajua unapigwa vita hata ndani ya CCM na wengine walikuwa wanaombea miaka mitano hii usipate lakini wa mbili havai moja na muungwana haumbuki siku zote.
Kama wanaweza wapande juu waende wakazibe!
Hongera JK Hongera CCM!
Kuipindua CCM ni kuungana kwa
ReplyDeletevyama Pinzani.
Vyama vingine vinajua kabisa kama
Havitashinda lakini bado vinagombea.
sasa si uharibifu wa kula tu.
where r other WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303
ReplyDeleteWALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)
less than nusu ndio wamepiga kura.....cant be serious
Hongera Mh.JK iliyobaki sasa ni kumwomba mungu akusaidie kutekeleza yale yote uliyo waahidi watanzania wenzako wakati wa kuomba ridhaa ya kubaki hapo kwenye nyumba nyeupe.Nawapongeza wapinzani kwa changamoto zao kubwa kwa chama chetu tawala,kwani wametusaidia kujua watanzania wa leo wanahitaji nini.CCM OYEEEEEE!!!!
ReplyDeleteKura Milion 9 mpaka milion 5? asilimia 80 mpaka 61??
ReplyDeletekuna maswali mengi. Japo ushindi ni ushindi lakini huu kwa watu makini si wakushangilia.
HONGERA JK, HONGERA CCM.
ReplyDeleteNGUVU UNAYO NA NIA UNAYOO JK...KAZA BUTI MHE,,
ReplyDeleteKIDUMU CHAMA TAWALA.....
AKSANTE SANA ANKOL KWA KUTUJUZA KILICHOJIRI NA KINACHOJIRI JIJINI....MUNGU AKUJALIE NGUVU ZAIDI....
NANA
Asante sana Slaa, Lipumba na wengine kwa kuchangia kupunguza kura za ushindi!
ReplyDeleteNdio demokrasia, yakhe!
Na wewe Mrisho, HONGERA!
Baada ya kupata wabunge wengi zaidi CHADEMA sasa kiwango cha ruzuku kitaongezwa tumieni at least 70% kujenga chama vijijini na mikoani na kuwezesha makada. Tumieni pia wabunge wenu wengi vijana kusaka wanachama wengi kwenye vyuo vya juu na High schools. Strategies za operation sangara ziendelezwe.
ReplyDeleteKeep it up!
hongera ndugu kikwete(samahani situmii muheshimiwa kwani siyo jadi ya watanzania ,Baba wa taifa alisema wote ni ndugu,hayo mambo ya muheshimiwa siyajui yametoka wapi),jitahidi kutimiza ahadi ulizotoa kwenye kampeni ,na ujue usipotimiza mgombea wa ccm 2015 tutamuulizia hizo ahadi,umeona mwenyewe ccm ilivyo,umeona mwenyewe ulivyohangaika peke yako kwenye kampeni,umeona mwenyewe chama kilivyo na makundi,umeona mwenyewe tulivyo POKWA na wapinzani majimbo zaidi ya hamsini(mengine yalikuwa ngome ya ccm)umeona hata huo ushindi wako si wakishindo kama 2005,sasa timiza ahadi ili umpe urahisi mgombea ajae,USANII haufai ktk mambo ya utawala hasa kwa mtu kama RAIS
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA
Mungu ni Mwema kwa kutupa rais tukiwa na amani. Poleni mliofiwa na ndugu zenu katika fujo mbalimbali. Hongera Kikwete rais wetu. Tuanze kazi ya kujenga taifa. Ninakuombea uchague wachapa kazi na Roho Mtakatifu akuongoze. Asilimia ya kura si hoja hoja ni kujenga nchi yetu na chama chetu CCM. Mwenyezi Mungu akubariki na aibariki Tanzania na watu wake
ReplyDeleteHongereni washiriki wote wa ugombea wa uraisi kwa kuunga mkono Kikwete.
ReplyDeleteNchi ni yetu wote bwana yeye nyie sisi msiwe na kinyongo chochote ili mradi mpate saidia kwa mambo mhimu.
Leo yeye kesho nyie na mungu anawaona acheni wenye kuumbiwa roho za chuki.
Asusa Mwenzio atangazwa helo helo helo helo.
Yaani alikuwa na imani kabisa atashinda? basi angetangaza tangu mwanzo kusiwe na uchaguzi aapishwe tu. Sie wananchi hatujachagua chama wajua tumechagua watu wanaofaa
Lo!Hata Jaji Makame anampongeza kwaq aibu kwani anajua kilichotendeka.
ReplyDeleteSASA HATA MAJAJI WAKITETEA UCHAKACHULIWAJI WA KURA na watu wa kawaida watafanyaje? NI AIBU TUPU!
JK aliniacha hoi na ule wimbo wake rumba Jaka kikwete 2010,kampeni kweli anaiweza mziki wake ukiwa Ngara unausikia uipigwa kutoka redio za Burundi,si mchezo JK kiboko yao
ReplyDeleteOngera sana Rais Kikwete
CCM bora tu mngelikubali kilichokuwa haki yenu kutoka kwa Wananchi kuliko uhuni wa kuiba kura mlioufanya hadi mnaona hata haya ya kuendelea kutangaza huo ushindi feki katika Majimbo mengine.YOU WILL SUFFER FROM GUILTY FOR THE REST OF YOUR LIFE!
ReplyDeleteHongera JK
ReplyDeleteProf LIPUMBA WEWE UMEAHIDIWA NINI NDUGU YANG!MBONA UMECHEKELEA SANA KINYUME NA MIAKA MINGINE? UNAFIKI/UDINI MTUPU!
ReplyDeleteyaani bwana siasa ni kitu cha ajabu sana eti mkapa leo anafurahia ushindi wa Kikwete haitaji mtu kuwa mjumbe wa NEC kujua kwamba hao jamaa wawili ni maadui kinoma juzi kufunga kampeni ati aliimba wimbo kumsifu ......dah jamani.The reason behind i think alijua kwamba kama slaa atakwenda ikulu wangetafutana vigogo so the only way out ni kujaribu kumsupport and i think he is pretending ili jamaa amsafishe his public image in the next five years.kwakifupi MKAPA-intelligent but also very arrogant,mbinafsi na conservative hana busara hata chembe
ReplyDeletemafisadi oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
ReplyDeleteWee anonymous wa mwisho, usimhusishe Roho mtakatifu hapa. Roho mtakatifu hashiriki kwenye uchakachuaji!
ReplyDeleteUsimkufuru Roho Mtakatifu ni dhambi isiyosamehewa.
Hongera Chadema kwa kufurukuta kiivyo. Sasa angalieni msije kuparurana kwa hiyo Ruzuku. Mkiwacheleweshea akina nanihii mgao wao tu, mtajiju!
ReplyDeleteDr. Slaa is to join and help wholeheartedly president Jakaya Mrisho Kikwete, for Kikwete's success is the success of Tanzanian people...Safi sana Dr. Slaa!
ReplyDeleteHongera Dr.Slaa kwa kazi kubwa, na pole sana kwa kuibiwa. Sasa kazi iliyopo ni kudai TUME HURU mapema iwezekanavyo na KATIBA MPYA. Hapo ndio tutapata mchaguliwa halali wa wananchi.
ReplyDeleteHONGERA MHESHIMIWA RAIS. KWA SABABU YA SERA YAKO YA KUKUZA DEMOKRASIA NDIYO MAANA KURA ZIMEPUNGUA NA WALA SI UMESHINDWA!!! NDIYO MAANA TANZANIA NI MFANO WA UTAWALA BORA AFRIKA. INASIKITISHA DK SLAA HAKUONYESHA UKOMAVU KWA KUKUBALI KUSHINDWA KISTAARABU. HIVI ANGESHINDAJE WAKATI CHAMA CHAKE HAKIJAWEZA KWENDA NCHI NJZIMA? SHAME ON YOU!! HATA ILE HESHIMA NDOGO ULIYOKUWA NAYO UMESHAISQUANDER. ILIYOBAKI RAIS WETU AAPISHWE AANZE KUTUONGOZA KUIJENGA NCHI YETU NA MUNGU AMUIMARISHE. CCM HOYEEEE!
ReplyDeleteMambo ya kufanya kwa vyama vya upinzani ni kuweka mkakati wa ushindi.
ReplyDeleteKuweka mgombea mmoja na si kila chama kuwa na mgombea wake, kudai tume huru, katiba kuangaliwa upya kuona kama inakidhi mahitaji ya sasa na ya baadae. Kushindwa kwa wabunge wa sisiem katika maeneo mengi ya mijini ni wananchi wenye uelewa kukataa porojo za ccm na si tu kukimbilia kusema ni kukua kwa demokrasia.
NDUGU ZANGU USHINDI WA CCM ULIKUA NI WA VEMA NA HAKI MAANA PIA SOTE TUNAKUBARI YA KUWA CCM NI ZAIDI YA KILA KITU,....HAWAKUCHAKACHUA POPOTE PALE MAANA WATU WENGI WANALAUMU SANA JUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI JAMANI VYAMA VINGINE PENGINE HAVINA SELA ZA KUWAKONGA WANANCHI......CCM NI CHAMA BORA NA WANANCHI WANAIKUBARI KWA KILA KITU....NAUNGANA NA WATANZANIA WENZANGU KUMPONGEZA DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE CCM HOYEEEEEE
ReplyDeletechadema mmejipotezea umaarufu sana kwa kuropoka kwenu na kujifanya wajuaji na kuleta mgawanyo wa kidini katika jkamii,watanzania sio wajinga hawawezi kugawa nchi kwa watu wenye udini na ukabila hatujazoea hivyo na wala hatujalelewa na kilichowadanganya ni washabiki wasio hata na card za kupigia kura.halafu wenyewe mnajipanga kuna kundi la walaji na la wasotaji so hamna msimamo,na slaa hii ndi bye bye yako nimekudharau sana na speeches zako
ReplyDeletekuna watu kadhaa wamejiandikisha ili watumie vitambulisho kwenye mabenki na taasisi kadhaa kwa manufaa yao na sio kupiga kura,,
ReplyDeletehata kama Dr.Slaa ningekuwa nampenda, kutotokea kwenye kutangazwa washindi inaonesha ukosefu wa maturity, politics is a game. you win or loose, halafu hakuna chaguzi saafi; juzi juzi UK kuna wanancki wengi zaid ya millions hawakupiga kura, sometimes wamekuwa wakipiga kura watu ambao co wa UK, think about US, Canada hata france?? kote huku kuchafu.. so wabongo tujisifu kwa chakwetu sio kuendeleza utumwa wa mawazo kwamba kila kizuri lazima kipo abroad.
G7
MUNGU IBARIKI AFRICA MUNGU IBARIKI TANZANIA.KILICHOPANGWA NA MUNGU BINADAMU AWEZI KIZUIA.TUMALIZE TOFAUTI ZETU ZA KIASIASA NA SASA TUNATAKIWA TUANGALIE TUTAFANYA NINI KWA MIAKA MITANO IJAYO.HONGERA SANA MH.JAKAYA MRISHO KIKWETE TUNAKUOMBEA AFYA NJEMA,UPENDO NA AMANI KATKA KUIONGOZA NCHI YETU.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.
ReplyDeleteMH.USIBWETEKE NA USHINDI ULIOUPATA WA KUIONGOZA NCHI TENA KWA MARA NYINGINE,USHINDI ULIYOUPATA UMESHUKA KWA ASLIMIA KADHAA UKILINGANISHA NA USHINDI ULIYOUPATA MWAKA 2005.HII INAONYESHA KUWA UTENDAJI WAKO WA KAZI ULIPUNGUA.TUNAWASHUKURU WA PINZANI KWA CHALLENGE WALIZOTOA NA NADHANI SASA UTAONA KUWA KAMA UTACHEZA TENA KWA MIAKA HII MITANO KUNAUWEZEKANO MKUBWA SANA KWA MWAKA 2015 CHAMA CHA MAPINDUZI KIKAPUNGUZA KUWA NA WABUNGE WENGI NA MADIWANI NA VYAMA VYA UPINZANI VIKAWA NA ONGEZEKO LA WABUNGE NA MADIWANI.HII HIWE NI FUNDISHO TOSHA KWA CCM NA MNATAKIWA MJIPANGE KWA MIAKA MITANO IJAYO.MH J.K Hongera kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamuhuri ya tanzania.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.
ReplyDeleteMH.USIBWETEKE NA USHINDI ULIOUPATA WA KUIONGOZA NCHI TENA KWA MARA NYINGINE,USHINDI ULIYOUPATA UMESHUKA KWA ASLIMIA KADHAA UKILINGANISHA NA USHINDI ULIYOUPATA MWAKA 2005.HII INAONYESHA KUWA UTENDAJI WAKO WA KAZI ULIPUNGUA.TUNAWASHUKURU WA PINZANI KWA CHALLENGE WALIZOTOA NA NADHANI SASA UTAONA KUWA KAMA UTACHEZA TENA KWA MIAKA HII MITANO KUNAUWEZEKANO MKUBWA SANA KWA MWAKA 2015 CHAMA CHA MAPINDUZI KIKAPUNGUZA KUWA NA WABUNGE WENGI NA MADIWANI NA VYAMA VYA UPINZANI VIKAWA NA ONGEZEKO LA WABUNGE NA MADIWANI.HII HIWE NI FUNDISHO TOSHA KWA CCM NA MNATAKIWA MJIPANGE KWA MIAKA MITANO IJAYO.MH J.K Hongera kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamuhuri ya tanzania.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.
ReplyDeleteBinafsi nimeridhika! nilitamani icheze kwenye 51% au kama ile ya Shein! sijui mheshimiwa ujumbe ameupata! au itakua yale yale!
ReplyDeleteNYIE MNAOZUNGUMZIA UDINI NA UKABILA WOTE NI WAPUMBAVU. HAMNA CHA UDINI WALA UKABILA HAPA.
ReplyDeleteCUF INA WAISLAM WENGI KWAKUA IMENZIA ZANZIBAR NA CHADEMA WACHAGGA WENGI KWAKUA MWANZILISHI NI WA HUKU, UNATEGEMEA NINI?
TANZANIA HAINA UKABILA WALA UDINI, MNAO SEMA SEMA KUHUSU UKABILA MNACHAFUA SURA YA NCHI YETU. SHINDWENI NA MASHETANI YENU HUKU.
MNATUMIA HIO LUGHA YA UKABILA NA UDINI ILI WATU WAPATE HOFU TU. JAMANI WE ARE ONE,NA SASA KWAKUA RAIS KISHACHAGULIWA, TURIDI KATIKA UJENZI WA TAIFA,NA RAISI WETU JK MUNGU AMJAALIE AFYA NA UWEZO WA KUTIMIZA AHADI.
VYAMA VINGI NDO MAENDELEO ANAE LALA ANAAMSHWA SIO KUNG'ANG'ANIA CHAMA KIMOJA TU.
HONGERA JK, WE NDO UMESHINDA, SO KEEP THE BALL ROLLING
Prof. Lipumba...next time gombea japo ubunge/uwakilisji manake tumechoka kuona jina lako katika kugombea urais.
ReplyDeleteHuu ukabila na udini umeanza lini? JK alipoingia Ikulu na asilimia 80 ya kura alizipata kwa watu wa dini moja au wa kabila moja?
ReplyDeleteNani aliyeingiza mambo ya dini au kabila kwenye uchaguzi huu?
Mbegu ya siasa za makundi za CCM imeanza kupandikizwa kwenye ngazi ya taifa. Watanzania mnachotakiwa kufanya ni kumkataa shetani, na nguvu zake zote na kazi zake zote!