Asalaam aleykum Ankal mkuu wa libeneke na nanihii.

Sina mengi isipokuwa nataka nizungumzie matumizi ya neno “hapana budi”. Nimeona watu wengi kwenye blog hii hawajui matumizi ya neno hili lakini bado wanalitumia sana. Kwa mfano kuna mtu alisema ”ili CCM ikomae kisiasa ni budi kuwaheshimu CHADEMA” Hii tungo ni mbovu na kuna watu wengi sana ambao wanatumia ” kishazi” hiki namna hii.

Mifano

Lugha sahihi. ”Ili CCM ikomae kisiasa, hapana budi kuwaheshimu CHADEMA”
Lugha mbovu ”Ili CCM ikomae kisiasa ni budi kuwaheshimu CHADEMA”

Lugha sahihi ”ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo, hapana budi kufanya kazi kwa bidii”
Lugha mbovu ”Ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo, ni budi kufanya kazi kwa bidii”

Watanzania tuna tabia ya kukosoana pale mtu anapozungumza kiingereza kibovu, wakati hatujali kabisa matumizi yetu ya kiswahili kibovu.

Asanteni.

Ambari Kavu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ninaunga mkono haya aliyosema huyu bwana Ili maendeleo yaje Tanzania, CCM haina budi kuheshimu CHADEMA.

    ReplyDelete
  2. kiswahili ni muhimu na si kiengereza, kicheko ha-ha-ha-ha.

    ReplyDelete
  3. Duh! kazi kwelikweli.

    "Haina budi" ndiyo nini?

    neno sahihi ni "hapana budi"

    Budi peke yake, haipo. Kwenye kiswahili hakuna neno "budi".

    Hivyo basi "hapana budi" ni neno moja na hakuna kitu kama "ni budi" au "haina budi"

    ReplyDelete
  4. Michuzi mwenyewe hapa anachakachua lugha kama nini. Mdau naoma utufafanulie kama hiki ni Kiswahili fasaha.

    1. Chuo Kikuu cha University of Dar Es Salaam.

    2. Barabara ya Morogoro Road.

    3. Daraja la Salander Bridge.4

    4. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport.

    ReplyDelete
  5. Basayev ShamilNovember 21, 2010

    Asante sana Bwana uloileta hii kadhia hapa.Wajua chanzo kikuu cha haya makosa niwatu wa vyombo vya habari,kuna watu wamepewa nafasi zakutangaza habari wakati hawajui kiswahili.Mimi huwa yanikera sana hali hii...na pia hawa jamaa zetu watokao miji ya bara wamekua wakipewa nyadhifa mbalimbali ktk majukwaa na nyanja zakiswahili na wao pia huchangia sana kuharibu kiswahili.Utakuta mtu aitwa nyambari alafu eti ndie mtaalamu wakiswahili pale chuo kikuu cha Dar..hivi kweli mm kwakukisoma tu Kiingereza ntakua mtaalamu wakiingereza zaidi y mwingereza?Kiswahili wenyewe ni wapwani hivyo hapana budi wengine wajifunze kutoka kwao.Mfano mzuri ni haya maoni niliyoatoa kuna tofauti kubwa yahiki kiswahili nilichokitumia mimi na maoni yatakayotolewa na mtu atokae bukoba..Situkani mtu lakini maana yangu watu wende Mtang'ata na kwengineko wakajifunze kiswahili na sisi wapangani tutakwenda Bukoba tukitaka kujua kihaya.Nimetoa mfano wa watu Mtang'ata kwa sababu wao ni miongoni mwa watu ambao hawana lugha nyengine zaidi ya kiswahili kwa maneno mengine kiswahili ndicho kikabila chao.

    ReplyDelete
  6. Swali langu ni hili, neno "budi" maana yake ni nini?

    ReplyDelete
  7. Hili neni linatokana na lugha ya kiarabu "la budi" yaani "inabidi". basi kama likitakiwa lifatane kama lilivoigwa toka ktk lugha husika mdau wa mada yuko sahihi, hapa "la" si "hapana"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...