Asalaam aleykum Ankal mkuu wa libeneke na nanihii.
Sina mengi isipokuwa nataka nizungumzie matumizi ya neno “hapana budi”. Nimeona watu wengi kwenye blog hii hawajui matumizi ya neno hili lakini bado wanalitumia sana. Kwa mfano kuna mtu alisema ”ili CCM ikomae kisiasa ni budi kuwaheshimu CHADEMA” Hii tungo ni mbovu na kuna watu wengi sana ambao wanatumia ” kishazi” hiki namna hii.
Mifano
Lugha sahihi. ”Ili CCM ikomae kisiasa, hapana budi kuwaheshimu CHADEMA”
Lugha mbovu ”Ili CCM ikomae kisiasa ni budi kuwaheshimu CHADEMA”
Lugha sahihi ”ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo, hapana budi kufanya kazi kwa bidii”
Lugha mbovu ”Ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo, ni budi kufanya kazi kwa bidii”
Watanzania tuna tabia ya kukosoana pale mtu anapozungumza kiingereza kibovu, wakati hatujali kabisa matumizi yetu ya kiswahili kibovu.
Asanteni.
Ambari Kavu

Ninaunga mkono haya aliyosema huyu bwana Ili maendeleo yaje Tanzania, CCM haina budi kuheshimu CHADEMA.
ReplyDeletekiswahili ni muhimu na si kiengereza, kicheko ha-ha-ha-ha.
ReplyDeleteDuh! kazi kwelikweli.
ReplyDelete"Haina budi" ndiyo nini?
neno sahihi ni "hapana budi"
Budi peke yake, haipo. Kwenye kiswahili hakuna neno "budi".
Hivyo basi "hapana budi" ni neno moja na hakuna kitu kama "ni budi" au "haina budi"
Michuzi mwenyewe hapa anachakachua lugha kama nini. Mdau naoma utufafanulie kama hiki ni Kiswahili fasaha.
ReplyDelete1. Chuo Kikuu cha University of Dar Es Salaam.
2. Barabara ya Morogoro Road.
3. Daraja la Salander Bridge.4
4. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport.
Asante sana Bwana uloileta hii kadhia hapa.Wajua chanzo kikuu cha haya makosa niwatu wa vyombo vya habari,kuna watu wamepewa nafasi zakutangaza habari wakati hawajui kiswahili.Mimi huwa yanikera sana hali hii...na pia hawa jamaa zetu watokao miji ya bara wamekua wakipewa nyadhifa mbalimbali ktk majukwaa na nyanja zakiswahili na wao pia huchangia sana kuharibu kiswahili.Utakuta mtu aitwa nyambari alafu eti ndie mtaalamu wakiswahili pale chuo kikuu cha Dar..hivi kweli mm kwakukisoma tu Kiingereza ntakua mtaalamu wakiingereza zaidi y mwingereza?Kiswahili wenyewe ni wapwani hivyo hapana budi wengine wajifunze kutoka kwao.Mfano mzuri ni haya maoni niliyoatoa kuna tofauti kubwa yahiki kiswahili nilichokitumia mimi na maoni yatakayotolewa na mtu atokae bukoba..Situkani mtu lakini maana yangu watu wende Mtang'ata na kwengineko wakajifunze kiswahili na sisi wapangani tutakwenda Bukoba tukitaka kujua kihaya.Nimetoa mfano wa watu Mtang'ata kwa sababu wao ni miongoni mwa watu ambao hawana lugha nyengine zaidi ya kiswahili kwa maneno mengine kiswahili ndicho kikabila chao.
ReplyDeleteSwali langu ni hili, neno "budi" maana yake ni nini?
ReplyDeleteHili neni linatokana na lugha ya kiarabu "la budi" yaani "inabidi". basi kama likitakiwa lifatane kama lilivoigwa toka ktk lugha husika mdau wa mada yuko sahihi, hapa "la" si "hapana"
ReplyDelete