NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK-Mchezaji maarufu wa mchezo wa tenisi duniani, Martina Navratilova leo amezindua rasmi maandalizi ya safari yake ya kwenda Tanzania kupanda Mlima Kilimajaro kwa kupanda kwa ngazi hadi ghorofa ya 49.
NEW YORK-Mchezaji maarufu wa mchezo wa tenisi duniani, Martina Navratilova leo amezindua rasmi maandalizi ya safari yake ya kwenda Tanzania kupanda Mlima Kilimajaro kwa kupanda kwa ngazi hadi ghorofa ya 49.
Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa , Balozi Ombeni Sefue alishuhudia kuzinduliwa kwa safari hiyo iliyofanyika katika jengo la Benki ya Amerika Jijini New York.
Martina Navratilova,(54) ambaye amenusurika na (survivor) kansa ya matiti anaupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama “ Laureus Sport for Good Foundation”. Taasisi hiyo yenye makao yake makuu Uingereza husaidia miradi mbalimbali ya jamii hasa miradi inayohusu watoto barani Afrika.
Safari ya Martina Navratilova ya kupanda mlima Kilimanjaro itachukua siku saba kuanzia disemba sita hadi 12 kupitia njia ya Rongai.
“Jambo, habari “ ndivyo Martina alivyomsalimia Balozi Sefue kwa kiswahili mara baada ya kufika kilele cha ghorofa ya 49 ambapo Balozi Sefue alimpokea.
“Nimeisubiri kwa muda mrefu nafasi hii adhimu ya kuupanda mlima Kilimanjaro, siwezi kuelezea furaha yangu ya kwenda Tanzania , nimethibitishiwa kuwa na afya njema na nimedhamiria kufika kileleni ” anasema Martina huku akitabasamu.
Martina Navratilova anapanda mlima kilimanjro , mlima mrefu kuliko yote barani Afrika ukiwa na urefu wa futi 19,341(mita 5,895) na kilele chenye barafu, ikiwa ni miezi michache tu imepita tangu kukamilisha matibabu ya kansa ya matiti.
Mchezaji huyu aliyejizolea sifa na tuzo kemkem kupitia mchezo wa tenisi, ataongoza kundi la watu 28 wakiwamo nyota wa michezo ya Olympiki wa Uingereza Gail Emmas na Mark Foster, pia yumo Bi Linda Buretis ambaye naye ni mnusurika wa kansa ya matiti.
Martina anasema ni wajibu wake kutoa mchango au kufanya jambo linaloweza kuwasaidia watu wengine wenye matatizo mbalimbali kwa njia kama hiyo ya kuchangisha fedha kwa kupanda mlima Kilimanjaro.
Wakati wa mazungumzo yake na Balozi Sefue Martina amesifu juhudi za serikali ya Tanzania katika kuhifadhi mazingira na hususani mbuga za wanyama.
Balozi Sefue pamoja na kumpongeza Martina kwa kupanda na kumaliza kwa ukakamavu ghorofa 49 za jengo la Benki ya Amerika, pia amempongeza kwa uamuzi wake kuja Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro.
Akasema licha ya kwamba madhumuni ya upandaji wa mlima huo ni kuchangisha fedha za kusaidia maendeleo ya jamii, lakini kupitia watu maarufu na mashuhuri kama yeye ( Martina) Tanzania kama nchi itapata nafasi ya kujulikana na kutambuliwa duniani kupitia vyombo vya habari vya kimataifa.
“ Nikushukuru sana kwa kuamua kuja Tanzania, unajua nchi kama Tanzania si rahisi sana kusikika kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kutokana na historia yake na kuwa nchi ya amani, watu wasiojali ukabila, dini au rangi” anasisitiza Balozi Sefue.
Na kuongeza kuwa mara nyingi nchi husikika kama kuna machafuko, vita, misuguano au majanga ya kibinadamu. Hivyo ujio wake Tanzania utachangia sana kuitangaza Tanzania na kuvutia watu wengine maarufu kuitembelea.
Kwa niaba ya serikali ya Tanzania, Balozi Sefue amemtakia kila la kheri katika safari yake ya kupanda mlima Kilimanjaro na kwamba anauhakika atafika kileleni.
Mambo ya Media yametutangazia ukweli wa Mt kilimanjaro upo wapi Kenya washaanza kuona aibu zamani Wa Tanzania tulikuwa hatusafiri na kujitangaza vizui sasa tumeamka hata sehemu nyingi Kenya washaambiwa wafute matangazo wanaoandika Mt kilimanjaro Kenya.
ReplyDelete