Naibu waziri wa Viwanda na Biashara mteule ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akizindua mradi wa nyumba zilizojengwa kisasa wakati alipoizindua kampeni ya ujenzi wa nyumba bora kwa wakazi wa jimbo hilo unaojulikana ‘Operesheni Ondoa Tembe’ ili kuboresha makazi ya wananchi wake ambao asilimia kubwa wamekuwa wakiishi katika nyumba hizo za asili
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya nyumba tembe ambazo kapania kuziondoa jimboni humo.Naibu waziri wa Viwanda na Biashara ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akiwa na mkewe Faraja wakitembelea matembe ambayo yatabomolewa katika operesheni hio. Naibu waziri wa Viwanda na Biashara ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya nyumba zinazojengwa kisasa wakati alpoizindua kampeni ya ujenzi wa nyumba bora kwa wakazi wa jimbo hilo unaojulikana ‘Operesheni Ondoa Tembe’ ili kuboresha makazi ya wananchi wake ambao asilimia kubwa wamekuwa wakiishi katika nyumba hizo za asili



Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Singida Kaskazini, Mh. Lazaro Nyalandu amezindua kampeni ya kuondoa nyumba za Tembe jimboni mwake ijulikanayo kama ‘Operesheni Ondoa Tembe’.Operesheni hiyo ilizinduliwa na mbunge huyo pia ni Naibu waziri mteule wa Viwanda na Biashara, katika Kijiji cha Msange kata ya Ilongelo, jimboni humo ambapo aliwataka wananchi kuanza kubadili mfumo wa nyumba wanazioihi ili wawe na nyumba bora zaidi.
“ Kama tutashirikiana kwa pamoja inawezekana, hivyo kwa kuanzia kila mmoja aanze kufikiri kuwa na nyumba ya kisasa na tutahamasishana ili tuweze kubadilika” alisema Nyalandu.
Aliwaeleza wananchi wake kuwa nyumba za aina hiyo ambazo huezekwa kwa udongo pamoja na kuwa ni za asili lakini bado zina matatizo kwani hazina mwanga wa kutosha na hata hewa kwa watu wanaoishui huko.Nyalandu alisema opereshani hiyo itafanikiwa kwa juhudi za wananchi hao kwa kuhamasishwa na viongozi nasi kwamba yeye ndiye atakayelipa gharama hizo kama baadhi ya watu wanavyodhani.
“Hii ni operesheni ambayo inamgusa kila mmoja na hivyio tutashirikiana na viongozi wa kata na vijiji kuhamasisha wananchi kujenga nyumba bora ili kusiwe na tembe katika miaka kadhaa inayokuja” alisema.Akitembelea baadhi ya nyumba bora ambazo zimeanza kujengwa, Nyalandu alipongeza wananchi walioanza ujenzi wa nyumba hizo na tayari mwenyewe ameanzisha ujenzi wa nyumba ya kisasa ambayo itakuwa mfano kwa wapiga kura wake.
Mbunge huyo kijana alisema alianza kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora katika kipindi kilichopita na watu wengi wamehamasika na kuanza kufyatua matofasli na kuchoma ili kuwa na nyumba bora na kusema kuwa operesheni hiyo ityasaidia kuboresha maisha ya watu.
Mkoa wa Singida ni moja ya mikoa ambayo imekuwa maarufu kwa ujenzi wa nyumba za tembe ambazo mbali na kuezekwa kwa udongo juu pia madirisha yake huwa madogo na hivyo kufanya wakazi wake kupata Mwanga mdogo ndani na pia hewa huwa haba. Mikoa mingine ni Dodoma na Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Nyalandu, ushauri wa bure nakuomba uchague baadhi ya nyumba za Tembe zibaki kwa ajili ya Ukumbusho wa kizazi kijacho. Wakija wajue kuwa awali babu zao waliishi katika nyumba za aina gani.

    ReplyDelete
  2. Naona ujumbe wa kuondokana na nyumba za tembe umeeleweka na sasa unafanyiwa kazi kumbe kila kitu kinawezekana ila tu utashi ulikuwa haupo.

    Hongera Mbunge kwa kuhamashisha kampeni ya "Ondoa Nyumba Za Tembe"

    ReplyDelete
  3. Shukrani Chadema kwa kufikisha ujumbe wa umuhimu wa Watanzania wote kuwa na nyumba bora.

    ReplyDelete
  4. mh naibu waziri naomba usiishie hapo tu maana kampeni ni juzi tu pls naomba hiyo kazi uliyoianza basi uende nayo kwa miaka mitano ijayo usiwe na nguvu za soda maana kampeni zako ulikua unazunguka na helkopta so pls usitunagushe

    ReplyDelete
  5. Idea nzuri lAkini isiwe nguvu ya soda as usual

    ReplyDelete
  6. Nia ya Mh. Waziri ni nzuri na ya kupongezwa. Ila ana changamoto kubwa mbeleni sababu mafanikio ya zoezi hilo yanatakiwa yaende sambamba na unafuu wa bei za vifaa vya ujenzi. Unless kama kuna mpango madhubuti wa serikali kulifanyia kazi hilo, otherwise naona kutakuwa na ugumu wa mafanikio kutokana na umasikini uliokithiri kwa kwananchi!.

    ReplyDelete
  7. Mheshihimiwa, hiyo ni shughuli ya Chama au Kiserikali!!??

    ReplyDelete
  8. This is a very fundamental idea or rather effort for the assistant minister. Keep it up Hon. Nyalandu and let your constructive idea be a challenge to other Members of Parliament. House is one of the basic needs of any human being. So gear it up.

    ReplyDelete
  9. Nadhani bado hajawa naibu Waziri,ni mpaka hapo atakapoapishwa ndio itakuwa rukhsa kwake kumwita jina hilo. kwa sasa mwaweza kumwita naibu waziri mteule tu.Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  10. Jaman jaman kinachohitajika ni jinsi ya kuboresha hizo tembe badala ya kufikiria jinsi ya kuzitokomeza;teknologia ya tembe ina mengi ya kujifunza,hali ya hewa ndani,watoto wazuri wanaozaliwa humo nk. nk

    ReplyDelete
  11. Kuna haja ya kutunza hizo nyumba zetu za ki-jadi kwani zinalingana na hali ya hewa ya huko. Sio ajabu, wataambiwa kujenga nyumba za bati katika mazingira ya joto na mvua za mawe!

    Nyumba za tembe zinaweza kuwekewa madirisha makubwa. Ili kuweza kuzifanya ziwe za baridi ndani yaani, kupunguza joto ni lazima kuwe na nafasi ya kuingiza hewa chini hapo kwenye msingi na paa la tembe liwe na "chimneys" za kutolea hewa, kulingana na ukweli kuwa hewa baridi hushuka; hewa joto hupanda.

    ReplyDelete
  12. Hatuna maji hatuna umeme. Nyumba hazikaliki kama hakuna maji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...