Mbunge wa jimbo la Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA
Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II ama Mr. Sugu akila kiapo Bungeni wakati mchakato wa kuapishwa Wabunge wateule ukiendelea.
Mh. Joseph Mbilinyi akipongezwa na Spika wa Bunge Mh Anne Makinda mara baada ya kula kiapo. Picha na Richard Mwaikenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kuna station flani ya redio hapa dar watakuwa wamefunga ngenga zao kwa sasa. Safi sana SUGU.

    M.A-Kafanabo

    ReplyDelete
  2. Sio anne makinda, ni anna makinda full stop sijui hiyo anne mmeiibua wapi na ghafla hata kama ni kiiglish, miaka yoooooooooote tunamjua anakwenda kwa jina la anna !!

    ReplyDelete
  3. JOB DONE SUGU,MUDA AUTOSHI MBIO NDEFU NOTHING IMPOSSIBLE.CONGRATULATION YOUNG MAN UMEWEZA NA UMEONYESHA INAWEZEKENA KUWAKILISHA BILA KUTEGEMEA MGONGO WA MTU INAWEZEKANA.GOD BLESSXXXXXXXX!

    ReplyDelete
  4. Wahenga walisema mwombee mbaya wako maisha mema ili apate kuyaona mafanikio yako. Hilo ni jibu tosha kwa akuombeaye mabaya

    ReplyDelete
  5. Hata mimi nilikuwa nashangaa hiyo Anne imetokea wapi tena

    ReplyDelete
  6. Saaaafi sana, Mh. Sugu! Hakika penye nia pana njia. Ni kula kwa kwenda mbele mjengoni. 'Dudu baya' na wenzake bila shaka mmeona mfano!

    ReplyDelete
  7. Poa Mh. Mbilinyi! Si kama kina 'Mh. Temba'na wnzaker mliozunguka kuipigia kampeni CCM. Kipindi cha uchaguzi kimeisha, kijua chawawakia! Mwenzenu 'Sugu' anpoa mjengoni....

    ReplyDelete
  8. Sugu umeni-impress WELL DONE nakutakia kila la-kheri

    ReplyDelete
  9. Hongera Mh. Sugu. Hadi tunakusoma kwa Michuzi Blog sasa. Michuzi kuwa honest. Wakati wa kampeni uliweka picha ngapi za Mr Sugu? Leo amepata ubunge na hata bunge halijaanza lakini tayari picha kibao za Mr Sugu. Bania lakini ujumbe umefika.

    ReplyDelete
  10. Pamoja na kushughulikia maslahi ya wana Mbeya mjini...Mheshimiwa Sugu tunaomba wezi wa kazi za wasanii nao wapatiwe ufumbuzi...najua huwezi kufanikisha hilo peke yako Mheshimiwa Sugu ila kwa sasa huko kwenye nafasi nzuri zaidi ya ku-lobby ili ufanyike mpango madhubuti wa kulinda maslahi ya wasanii...wakiwemo wale njaa waliovaa t-shirt za CCM!Najua kaka "Mchuzi" huwezi kubania hii...

    ReplyDelete
  11. Ati akawatetee kazi za wasanii wakati mlimshiti wakati wa kampeni, mmeonyesha jinsi mlivyo roho za kwa nini imekula kwenu, mwenzenu mjengoni gari ufll kipupwe ruzuku aah mwenzenu anapeta, nyie ndo mtakoma mtaburuzwa na kazi zenu na mtaendelea kuzulumiwa kwa ajili ya ulimbukeni wenu, sugu wapotezee laivu hadi waje wainame wakulambe mikuu mbele ya waandishi wa habari tena wala ya magazeti ya udaku!

    ReplyDelete
  12. mshahara= 12,000,000/=
    kila kikao=200,000/=
    pesa ya kujikimu kwa mwezi=2,400,000/=

    Mungu akupe nini Sugu waache waseme mpaka mate yawakauke.

    ReplyDelete
  13. mdau kafanabo wa kwanza kutoa komenti lakini wewe si ndie ulimtukana humu kwenye michuzi alipoenda kuchukua form za kugombea ubunge tena ukajidai wewe ni mjomba wake na matusi tele leo unaleta upambe nuksi eeeh.au unafikiri tumesahau?usibanie hii michu

    ReplyDelete
  14. Ninyi mnao sema siyo Anne Makinda, mnachemsha, hata website ya bunge inasema ni Anne Makinda, msimlaum Michuzi.

    Chaki hapa:
    http://www.parliament.go.tz/bunge/index.php

    ReplyDelete
  15. Ephraim Kibonde! unalo hilo limekuganda! utajibeba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...