MGAO WA MAJI DAR

1. Kutokana na kuchelewa kwa mvua za vuli kumekuwa na upungufu wa maji kwenye vyanzo vikuu vya maji kwa Jiji la Dar es salaam; Mto Ruvu na Kizinga

Maji kwenye Mto Ruvu yamepungua kutoka kina cha wastani cha mita 2.10 hadi mita 1.18 hali iliyopelekea kupungua kwa uzalishaji maji kutoka 84% Jumapili (07/11/2010) hadi 59% jana (Alhamisi 11.11.2010).

Kwa sababu hii, kumekuwepo na upungufu wa maji katika maeneo kadhaa ya Jiji, maeneo ya Bunju, Boko, Mbezi, Mwenge, Kawe, Mikocheni,Kijitonyama, Sinza, Msasani na Kinondoni tayari yameshakumbwa na upungufu wa maji hasa nyakati za mchana (saa 5 – 10).

Kutokana na hali hii kumekuwa na mgawo wa maji ili maji yanayozalishwa yaweze kusambazwa kwa wote na kwa uwiano sawia. Mgawo wa maji utaendelea hadi mwishoni mwa mwezi Novemba mvua zinapotarajiwa kunyesha.

Ratiba ya mgawo imeandaliwa na itasambazwa kwenye vyombo vya habari ili watumiaji wajue watapata maji wakati gani.

Taarifa zitaendelea kutolewa kadri hali itakavyokuwa ikibadilika.

2. Kumekuwepo na wauza maji ( wa magari na Bajaj ) wanaotumia rangi zinazo shabihiana na rangi rasmi za DAWASCO.

DAWASCO inapenda kuwataarifu wakazi wa Jiji kwamba haina uhusiano wowote na wauza maji hawa, na wala haina uhakika wa wapi yanakochotwa maji yanayouzwa.

DAWASCO inawatahadharisha wananchi
kuyahakiki maji wanayonunua kabla ya kuyatumia.

IMETOLEWA NA DAWASCO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kinyerazi tuna mabomba ya wachina tu yametandikwa miaka minne iliyopita lakini maji ya DAWASCO hatujawahi kuyapata isipokuwa kwa kununua kwenye ma-bowser. Peerhaps tangazo hili halituhusu

    ReplyDelete
  2. KWA TAARIFA YENU DAWASCO KINONDONI HAKUNA MAJI LEO NI SIKU YA 5 SASA HUO NI MGAO AU?

    ReplyDelete
  3. Mi nawashangaa sana, kwetu mburahati hatuna maji about mwezi mmoja sasa, sijui huo mgawo unamhusu nani.

    ReplyDelete
  4. Changanyikeni hatuna maji tangu mwaka 1982 ( nisaidieni kupiga hesabu ni miaka mingapi au rather ni siku ngapi) .

    Kwahiyo huo nao ni mgao au?

    na walitandika mabomba ya wachina kwa mbwembwe na mihemko yote tangu mwaka jana . Watu walichimba mifereji kwa sururu na kufukia mabomba lakini ndio nadhani yatageuka tena mazalia ya panya, nguchiro nk. kama yalivyogeuka mabomba yetu nje ya nyumba!

    Mhuuuuuuuuuuuuuuuuuuu! ( hapo nimehema)!

    ReplyDelete
  5. Ukonga,Pugu hakuna maji kabisa sasa ni zaidi ya miaka 20 kwa hiya mgao hautuhusu wenyewe tumekwisha zoea maisha ya ujima. maji yetu ni ya kununua kwenye magari tunajaza ma-sim tank tunaendelea na maisha.

    ReplyDelete
  6. DAWASCO mnatoa taarifa baada ya kukata maji siku 5 bila taarifa yoyote. Mnachefua!taarifa ilitakiwas itoke kabla ya mgao kuanza kwa sababu dalili za kwisha maji lazima zilikuwa zinaonekana.
    Kinondoni leo ni siku ya 6 maji yametoka leo usiku kidogo tu yamekatika, ukishuka hapo kati ya Morocco na Victoria maji hayajawahi kukatika, ni uwiano gani huu wa mgao mnaousema!

    ReplyDelete
  7. tena hao dawasco hawapo serious,mm wa Tegeta Block F wiki ya 4 sasa hatuna maji,halafu wanajifanya kutoa tangazo la mgao saiv..wanakeraaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  8. Karne ya 21 ya Sayansi na Technolojia bado DAWASCO wanazungumzia mvua za vuli. Dar inaweza kabisa kupata maji kutoka mto Wami, Pangani na hata Rufiji....Ni uvivu wa kufikiri. Ni uzembe wa watendaji wetu

    SHAME ON YOU DAWASCO AND THE GORVENMENT!!! MNA MAWAZO MGANDO!!!

    ReplyDelete
  9. Kweli hii taarifa nashindwa kuelewa ilitakiwa kutoka lini. Sinza tumekuwa hatuna maji kwa muda wa mwezi mmoja na nusu sasa. Hivi tulitakiwa tupewe taarifa wakati ule ama sasa? Sielewiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...