NDUGU MICHUZI NA WAPENZI WOTE WA BLOG HII YA JAMII.
NAOMBA MNISAIDIE KUMTAFUTA BABA YANGU MPENZI KWA JINA ANAEJULIKANA LA AMARI ADAM SALIM AMBAE ALIONDOKA NYUMBANI TANZANIA KATIKA MIAKA 25 ILIYOPITA KUELEKEA NCHI ZA ULAYA.
HAIJULIKANI ULAYA GANI ALIYOKWENDA ISIPOKUWA MARA YA MWISHO ALIWASILIANA NA BABA YAKE (BABU YANGU) AKIWA NCHINI UTURUKI MIAKA KUMI NA TANO ILIYOPITA.
BABA YAKE (BABU) MZEE ADAM SALIM YUKO HAI NA ANAISHI DAR ES SALAAM. BWANA AMARI ANAKUMBUKWA SANA NA FAMILIA YAKE HASA BABA YAKE MZAZI ANAMKUMBUKA KWA MAJONZI MAKUBWA SANA.
TUNAOMBA MTU YOYOTE AMBAE ANAEJUA TAARIFA ZAKE AU ANAJUA ALIPO TUSAIDIE KWA KUWASILIANO .
SAKI-07759745334 UK
Email saki.adam@yahoo.co.uk
jamani hivi nyie watu ambao mnaenda ughaibuni unakaaje kimya siku zote hizo huna mawasiliano na ndg zako ?mnawatesa wazazi kwa mawazo
ReplyDeletewatu wakisafiri ndo tatizo lao wanafikiria kila mtu atawalilia shida. Huwenda ndugu zake wako njema kuliko yeye anasota tu huko ulaya.
ReplyDeleteMzazi muhimu kaka fanya hima wasiliana nae na hivyo yuko hai pls pls pls.
China
Bandugu safari siyo mchezo, unaweza kukumbwa na mambo kama ya sinema ya 'Midnight Express' ughaibuni.
ReplyDeleteHivyo badala ya kulaumu, tuiombe jumuiya ya 'waswahili' huko Uturuki labda kuna jamaa anaweza kufahamu mtanzania mwenye umri wa miaka 50, ambaye aliondoka Tanzania mwaka 1985 akiwa na umri upatao miaka 25 awasiliane na kijana wake/mzee wake.
Mdau
San Salvardo, Brazil.
Wadau tusiwalaumu sana hawa walioondoka. Hata wao hawakutaka maisha yaende kombo. Nchi zetu mnazijua, wanashtuka tu wamepoteza mwelekeo.
ReplyDeleteNinachomshauri mtafutaji ajaribu kutafuta picha yake aweke hapa. Alafu itakuwa rahisi kumtafuta.
mdogo wangu pole sana. Miaka 25 sio mchezo huyu baba yako kama yungali hai basi ni lazima yuko katika matatizo makubwa kiasi cha kushindwa hata kuwasiliana nanyi miaka yote hiyo.
ReplyDeleteJaribu kuweka picha yake ya miaka hiyo labda watu wataweza kumfananisha, kwani kwa miaka yote hiyo ni lazima atakuwa amebadilika.
Ugumu zaidi ni kuwa hata hamjui ni nchi gani aliyokwenda.
Usikate tamaa, zidi kumtafuta
Hayo maoni ya mtu wa kwanza na wapili huko juu yanaonyesha kiwango cha elimu cha watanzania.
ReplyDeleteKwa ufikiri huu, kumbe ndiyo maana mnawaogopa wakenya.
Ahsante michuzi kwa blog yako naamini huyo anayemtafuta ndugu yake atampata. Nami nilikuwa nina ombi namtafuta ndugu yangu anayeitwa ONESMO RABIEL KIMARO kama kuna anayemfahau au yeye mwenyewe ataisoma meseji hii, nilijaribu kumtafuta mara ya mwisho 2005 nilipoambiwa yupo Dar bila mafanikio. Email yangu nkansee1@yahoo.com.
ReplyDeletePOLE SANA NDUGU YANGU. MUNGU ATAKUASIDIA APATIKANE. ILA KWA USHAURI WANGU ITABIDI UBABANDIKE PICHA YAKE MAANA WETU WAKISAFIRI NJE YA NCHI MARA NYINGINE HUBADILISHA MAJINA KWA SABABU NYINGI TU Eg ZA KIKAZI, KIDINI AU HATA KINDOA
ReplyDeleteNyinyi watoa maoni wa kwanza na wa pili kama hamna la maana la kuchangia bora mnyamaze. Msisahau hata nyinyi ni binadamu ambao mnaweza kupata mitihani katika maisha. Wahenga wamesema 'hujafa hujaumbika'. Usifurahie majaribu ya wenzako.
ReplyDeleteww ulitoa maoni kusema mtoa oni wa kwnza na wa pili tusifurahie majaribu ya mtu hakuna anayefurahia wote tupo ktk harakati za kumtafuta kwa mawzo mbalimbali,ww ndio huna mawzo na hayo mamisemo ni misemo tu hata kwenye kanga yapo,ndio kwani uongo unakaaje nchi za watu siku zote hizo!tena ukome kuwaambia watu hawana mawazo ndio nyie nyie mnaozamia nchi za watu hamna hata kazi
ReplyDelete