Ankal naomba wadau wanisaidie,
mwezi uliopita nilifanya mtihani wa NBMM(final stage) na nilibakisha somo moja,kwa kweli nilijiandaa vzr.Sasa siku ya mtihani nilipoingia kwenye chumba cha mtihani wkt tumepewa dakika 10 za kujisomea nikakuta kuna baadhi ya maswali nayafahamu vzr tu,sasa nilipoanza kufanya swali la kwanza nilijisikia hali ya joto then mwili ukaanza kutoa jasho nikajisikia kama nalegea kiasi ya kwamba hata ili karatasi nilikuwa nayo ikaloa kwa kwali nilijikalia mpaka mwisho sikuandika kitu.Kitendo hiki kinaniuma sana mpaka leo naomba wadau wanisaidie hasa wenye utaalamu kwamba nn kilitokea na nifanye nn ili hili lisijitokeze tena.
ahsante
mwezi uliopita nilifanya mtihani wa NBMM(final stage) na nilibakisha somo moja,kwa kweli nilijiandaa vzr.Sasa siku ya mtihani nilipoingia kwenye chumba cha mtihani wkt tumepewa dakika 10 za kujisomea nikakuta kuna baadhi ya maswali nayafahamu vzr tu,sasa nilipoanza kufanya swali la kwanza nilijisikia hali ya joto then mwili ukaanza kutoa jasho nikajisikia kama nalegea kiasi ya kwamba hata ili karatasi nilikuwa nayo ikaloa kwa kwali nilijikalia mpaka mwisho sikuandika kitu.Kitendo hiki kinaniuma sana mpaka leo naomba wadau wanisaidie hasa wenye utaalamu kwamba nn kilitokea na nifanye nn ili hili lisijitokeze tena.
ahsante
MDAU WA DAR
sounds like the nervous breakdown to me.
ReplyDeleteInaitwa panic attack. Next time unapokwenda kufanya mtihani, take a deep breath and relax kabla hujaanza, inasaidia kuikabili.
ReplyDeleteMuhimu inatakiwa uonane na daktari wa mental health.
Soma link hii itakupa mwanga zaidi:
https://health.google.com/health/ref/Panic+disorder
Hapo hakuwa na mkono wa mtu usiende kupiga ramli wala nini.Kilichokupata ww kimeshawapata wengi duniani.Inaelekea ulipatwa na anxiety attack.
ReplyDeleteni presha ya woga tu mdau! take it easy next time
ReplyDeletePole sana mdau wa Dar.Kwa experiance yagu mimi nadhani ulipata mshtuko wa moyo,ni vyema kumuona mtaalamu wa mambo ya afya,ujiangalie kila kitu.Sukari/colestrelo nk,Pole sana.
ReplyDeletestress tu hiyo
ReplyDeleteZAUNUNU
pole sana mdau ungetuambia umri wako na jinsia yako,maana mara nyingi hizo k=huwa zinawatokea wanawake waliofikia au kukaribia menapouse.but jaribu kuongea na dactari wko kwa ufasaha zaidi ila mimi hiyo huwa inanitokea na umri wangu ni 48 yrs ni mwanamke
ReplyDeleteDuh, hako lazima ni ka-mzizi tu? Kuna mtu anakuwekea mtima nyongo. Nenda kamuone babu.
ReplyDeleteMuone daktari, hata mimi huwa napata panic attack kwenye mitihani au job interviews. Kwahiyo ninachukua dawa siku nikiwa na hivyo vitu na sipati matatizo kabisa. Ni matatizo ya ubongo, lakini haina maana ni kichaa!
ReplyDeletesitanii lakini kilichonipata mimi ni kuwa sijui kama ni panic au anxiety lakini sikuweza kuamua kuanza sauli lolote kwa muda halafu hafla tu nilijikuta nafika kileleni (ejaculate). Yaani nilijishangaa kweli kweli.
ReplyDeletePanic attach nadhani.Kuna rafiki yangu mmoja tulikuwa katika group presentation(watu 3) alikuwa kajiandaa vizuri sana lakini ilipofika zamu yake jamaa aliongea sentensi moja then ghafla akanyamaza baada ya hapo hakuweza kusema chochote ilibidi tufunge presentation yetu manake part yake ndo ilikuwa ya mwisho.Baadae jamaa anasema hajui nini kilimfunga manake kila kitu kiliyeyuka na hata kuzungumza hakuweza.So it really happens na ni kwa watu wengi tu.
ReplyDeletehuyo ni jini subira ambaye mara nyingi hapendi kuona kiti wake akifanikiwa kimaisha cha msingi kula sana pilipili mbuzi kabla ya kuingia kwenye mtihani maana anaogopasana pilipili na kisha jipake viks kingo kwenye mikono utaisikia baridiii na utafaulu vizuri sana.
ReplyDeleteNakushauri uende kwa Mchungaji Gamanywa, Askofu Deo Lubala au T.B. Joshua (Nigeria- Lagos)Immediately. You have a great future and Satan is the one behind all the experience you faced on that day.
ReplyDeleteThat was an attack from the devil. The devil knows that your future is great that's why he did that to stop you from excelling to your greatness. Run to Jesus Christ immediately because only He alone can solve your problem.
ReplyDeleteThat's just the biginning, then emotional breakdown and then misfortune throughout your life.
Nevertheless, there is a solution to your problem in Christ Jesus. I recommend you visit "Synagogue Church of All Nations" in Lagos Nigeria and see Senior Prophet T.B. Joshua and you will come back with your testimony. If you cannot afford the trip, see PAstor Gamanywa or Pastor Deo Lubala (Sinza Mori).
Pole mdau. Shauku ya kumaliza pamoja na kukuta maswali unayoyafahamu vilikufanya upate msongo wa mawazo(stress) ambayo ikakusababishia mwili ushindwe kujizuia. Hali hii huwa inaisha, jambo la msingi wakati mwingine usipanie sana unapoenda kwenye mtihani, pumnzika vya kutosha kabla ya kwenda chumba cha mtihani, hata kama ikiwezekana siku moja kabla kifanye uko bussy na shughuli zingine usahau kama vile kuwa na jamaa zako wa karibu. Hii itakusaidia kuondokana na tatizo kama hilo wakati mwingine. Ushauri wa mwisho nenda kwa madaktari wa saikolojia watakupa msaada wa kutosha. Kila rakheli.
ReplyDeletepole. Hila mimi nazani wewe ni kilaza tu . Mimi nazani ulisha nunua mtiani ukaukariri , sasa ulipo fika kwenye chumba cha mtiani , mambo yakapotea kichwani. pole sana mambo ya kukeremisha yanawenyewe kaka. usione watu wanamaliza adi master , si wote wanaakili , sema wanajua kumeza !
ReplyDeleteMdau PAris
Mtihani uko hivyo, inatokea!. Sio lazima umuone Daktari, labda iwe inakutokea kila wakati. Unaweza kujenga control though self help au ukamuona Daktari. Schalary material 'Anxiety Attack' yatakupa mwanga zaidi. Ukianza kuwasikiliza hao akina Mchungaji sijui nani au akina Shehe Yahya umekwisha! Utamaliza fedha zako huko wakati matatizo hayo ni ya kawaida tu!
ReplyDeleteMdau, hali ya kutoka jasho jingi na mwili kulegea kwa ghafla wakati mwingine hutokana na sukari kuwa chini, that is low sugar level, especially kama hukula vizuri hata kama you are not diabetic. Hali hii ilishawahi kunipata, ingawa si katika mtihani.Kama wadau walivyosema inaweza pia kuwa ni anxiety tu, lakini ni vizuri pia ukafanya uchunguzi zaidi. Ila next time ikitokea jaribu kula kitu chochote cha sukari kama pipi au juice,ili kurudisha nguvu.
ReplyDeletesound like ulipanic sana, ila kuna kipimo cha hypertension ambacho ni 24hours tape monitor tunaweza kukufayia (ETT), hapa tunaweza ku-diagnose whats going wrong on you, for sure hili ni swala la STRESS huitaji pastor, whats pastor for when it come to SCIENCE based knowledge jamani, hawa mapastor wanaleta shida tuu, just like wengine viongozi wa dini wanasema condom transmit HIV, we dont need them, let SCIENCE KNOWLEDGE STAND NOW IN 21ST CENTURY.
ReplyDeletenduggu yangu pole sana kwa yaliyokukuta nadhani kama wadau wengi walivyosema hiyo ni panic attack na zaidi sana wengine wamejaribu kukushauri utafute uponyaji kwa Mungu nalo ni jambo zuri vile vile kwani ukiwa na imani na Mungu hupata uponyaji hata wa akili...jambo la namna hii limewahi kumtokea rafiki yangu tulikuwa tunasoma nae miaka ya nyuma alishindwa kabisa kufanya mitihani ya form 6,siku ya mitihani alikuwa hoi kama anayetaka kufa sasa,tumekuwa maadui mpaka leo maana ukimkumbushia ili aeleze nini kilitokea hataki hata kukuona,basi imebaki simulizi mpaka leo na akiniona anabadilisha na njia licha ya kuwa jambo hili lilitokea miaka mingi ya nyuma.
ReplyDeleteNaomba address yako nikutumie dawa za kuondoa mchecheto au kama una jamaa Uk muombe akununulie hizo dawa Boots phamacy
ReplyDeleteNakueleza kutokana na experience panick attack (anxious disorder) saa nyingine ni manic depression. Mimi sikua na manic depression but I had a panic attack na ilini control sana na kupoteza muda mwingi sana na ilichukua kama mwaka kwa madaktari kujua ni nini kinanisumbua. Na madoctor wengi bongo hawajui hii kitu. Sijui siku hizi. Uoga ni kitu cha kawaida lakini too much ni disorder. Kama iko serious na inakuja mara kwa mara mwone doctor wakishaondoka kuwa huna matatizo ya moyo au kisukari basi mimi ningekuambia tafuta therapist au vitabu vitakavyokuwezesha kuumaliza huu ugonjwa. Mimi sia advocate utumie dawa kabisa... Mimi nilikua naogopa kwenda kwenye misiba, kukaa kwenye makundi makubwa ya watu na mpaka ikafikia nilikua naogopa kutoka nje kwenda mahali popote peke yangu. Nilivyopewa dawa ya week moja tu na nilichukua kama miezi sita kurudi kwenye my normal life...Naona yako inakuattack ukiwa na stress basi ni rahisi kuicontrol..Nilivyokuja huku nilijikuta naanza kuogopa madaraja makubwa, kusafiri na ndege na height. Nilikwenda kumwona therapist na akanielekeza vizuri sana jinsi ya kucontrol. Ukienda upande wa madawa utaishia kuishi kwa dawa tu. Na siku ukisafiri na kuzisahau basi utasumbuka sana. Just learn how to control your feelings na punguza stress. Fanya mazoezi sana, kula balance diet na kaa na watu wenye positive thinkings na wewe kuwa na positive thinking. Chochote unachofanya kumbuka sio mwisho wa dunia na kama ni mitihani jiandae kadri ya uwezo wako na weka kwenye kichwa kuwa unachofanya umeput effort ya 110% sasa whteve the result kama ni bad kuna kesho...Positive attitude zitakuondolea hii kitu...Mimi nakwambia baaada ya kumwona therapist ni miaka kama 15 haijanipata na sasa hivi kila siku kwenda na kurudi lazima nikatize madaraja mawili makubwa hapa NYC na wala siogopi kabisa na wala sijali ni saa ngapi napita na pia public speech na presentation siku hizi mimi ni champ...
ReplyDeleteJust sali sana na kuwa na positive attitude na pia fanya mazoezi na kula balance diet kama huwezi kula balance diet basi tumia vitamins...
Na pia hii kitu ujue niya kurithi wachache sana wanapata hii baad ya kuexperience trauma. Hata kama hujaona ndugu yako mwingine anayo hii labda wanayo lakini iko kwenye mild form.
Mkuu pole sana. Hicho moja kwa moja ni kipapai. Kuna mtu hapendi maendeleo yako alikuwekea kitu njiani ukakikanyaga bila kujua wakati unaelekea kwenye mtihani
ReplyDeleteNDUGU YANGU KWANZA POLE SANA. HAPA KUNA MASIHARA SANA. NAAMINI KITU KIMOJA AMBACHO ULIKABILIANA NACHO. WEWE BINAFSI ULIKUWA OVER CONFIDENCE, NA PILI ULIKUWA UNAYAFAHAMU MAJIBU KIASI YA KWAMBA KILA UKIFIKIRIA UNAHISI BADO. SIKU INGINE NINGEKUSHAURI KITU MUHIMU SANA. DAKIKA WANZO KUPENI ZA KUJISOME KABLA YA MTIHANI MIMI NINGEKUSHAURI ACHANA NAZO MARA NYINGI HUWEZI UKA CONCETRATE KWA MAZINGIRA HAYO SANA SANA ZITAKUTIA MCHECHETO. NI MARA MIA UTOKE NJE UKALE fresh air KAMA WANARUHUSU.
ReplyDeleteKapalilie makaburi ya ukoo wenu na hiyo ni kinga tosha dhini ya wenzio ofisini wanaoogopa wewe kuchukua cheo chao.
ReplyDeletenyonywa tuzu kabla hujaanza mtihani next time
ReplyDeleteKWELI ULIPANIC NA HATA WAKATI UNAANDIKA MSG UNAONYESHA ULIPANIC KWANI KWA SASA HAKUNA BODI INAITWA NBMM ILA NI PSPTB, POLE SANA
ReplyDeleteWadau mie nikiwa ha ahadi na demu nikimuona tu naanza kutetemeka, je ugonjwa huu ni sawa na wa mdau
ReplyDeleteKuna wadau wamesema aidha ni panic,anxiety au kupungua kwa sukari mwilini. Kati ya hayo moja wapo laweza kuwa jibu sahii hussusani la kupungua kwa sukari. Wanafunzi wengi vyuoni TZ hukumbwa na tatizo hilo hasa kipindi cha kujiandaa na mitihani. Wakati nasoma nimeshuhudia baadhi ya wanafunzi kuanguka na kupelekwa hospitalini na majibu kutoka hospitalini yamekuwa ni upungufu wa sukari. Unapo jiandaa na mitihani una tumia nguvu nyingi sana na hivyo hata sukari mwilini inatumika sana.
ReplyDeleteSijafurahishwa na majibu wanayotoa baadhi ya wadu ambayo ni ya matusi, wanaharibu maana ya kutumia blog hii kama sehemu muhimu ya kubadilisha mawazo na utalaamu mbalimbali. Kama huna jibu tafadhali usiandike kitu hulazimishwi. Kwa mwenye Blog hii naomba uwe unapembua na kutupilia mbali mawazo ya hovyo maana si muda mrefu wadau hawata toa hoja kupitia chombo hiki kwa kuogopa matusi.
Mdau wa jini subira umeniacha hoi, nimejicheka kweli!
ReplyDeleteMFADHAIKO WA AKILI,YAONEKANA WAZAZI WAKO WALIKUWA WAKALI SANA AU ULIPATA DHULUMA KATIKA MALEZI YAKO
ReplyDeletekuna wadau kama 5 hivi walioelekeza diagnosis yao kwa majini na waganga mmenichekesha sana.
ReplyDeleteNilikuwa sitaki kuchangia lakini nimeamua kuchangia kwa sababu ya michango ya anon kadhaa, kwa kifupi ushauli wa waliokuambia uende kwa mganga wa kienyeji ni uongo mkubwa wala hakuna cha mbaya wako wala nini. Na kwenye maombi waweza kwenda kwa kuwa maswala ya dini hutujenga kuamini tusivyoviona na hatimaye kutujenga.
ReplyDeleteTatizo hilo hutokea watu wengi sana ila tu huwa hawasemi. mimi binafsi lilishawahi kunitokea mara mbili, yaani nilishawahi kuijakulate mara 2 kwenye chumba cha mtihani, na nina rafiki yangu nilipomsimulia na yeye akasema pia ilishawahi kumtokea.
Ila hali ya ijakulation ikiisha naendelea na paper kama kawaida, pole sana kwa kuwa hukuweza kuendelea na mtihani ila mimi niliendelea baada ya bao na nilifaulu na sasa nakula bata na ajira yangu.
Hali hiyo inatokana wa kutokujiamini, na sana sana huchangiwa na wazazi wakali katika kipindi cha kukulea. wala usiende Hospital wala kumeza dawa, hakuna cha sukari kushuka wala nini.
Cha msingi, jichanganye tu na watu katika mazingira tofauti tofauti, jenga mazingira ya kujiamini kwa kuchangia hoja mbalimbali hadharani hata ukikosea usione noma songa mbele tu. Jenga kujiamini usomapo kitu chochote kwa ajili ya mtihani na kama hali hiyo ikirudia uko kwenye mtihani ijakulate, ijakulation ikiisha endelea na mtihani kwani utapoteza dk kama 3 tu hafu haliya kawaida itarudi kama kawaida.
Usihofu kaka/dada kwa tukio hilo Hauko peke yako.
hii imewahi kunitokea. nilikuta swali ambalo nililisoma jana yake na silikumbuki vizuri. badala ya kusoma swali na kukumbuka logic nataka nicopy na kupaste. nilipanioc kama nusu saa baadae nika relax na kufanya mtihani. next time take a deep breath kama mara tatu hizi utatulia. ukiweza kunywa maji.
ReplyDelete