Michuzi
Mimi ni mtanzania ambaye nafanya kazi ughaibuni kwa sasa.
Nina kibanda changu huko Dar ambacho nahitaji kukimalizia. Nimekutana
na watu wananiambia ni cheaper kwenda kununua vifaa vya ujenzi China
(kama nina pesa) badala ya kuvinunua Dar.
Nafikiria kwenda China kununua vifaa hivyo lakini tatizo nililonalo ni kuwa sijawahi fika China na sijui pa kuanzia. Ningeshukuru sana kama wadau wa blogu hii wangenisaidia habari (information) ifuatayo
1. Mahali huko China apambo naweza kupata vifaa vifuatavyo
a) Materials za kutengenezea madirisha na milango ya aluminium
(vikiwemo frames, vioo na accessories zote)
b) Fittings za ndani kama vile masinki ya bafuni, jikoni na chooni,
bathtubs, heaters, shower trays + accessories, mabomba na vitu kama hivyo
c) Vitu vya umeme kama vile taa za kuning'iniza (chandliers), taa za
kawaida, switch za aina mbalimbali na taa za mapambo
d) Mapambo mbalimbali ya ukutani
e) Makabati ya jikoni (Kitchen cabinet set) ambayo iko vipande vipande ambayo naweza kuiunga ikifika Dar
f) Tiles za chooni, jikoni, sebuleni na vyumbani
g) Furniture za aina mbalimbali kama vile makochi, vitanda na kadhalika (e.t.c)
2. Kampuni ya huko China inayoaminika na yenye uzoefu (jina na contact details zao) ambayo naweza kuitumia kunisafirishia vitu hivyo kutoka China mpaka Dar. Vitu hivyo vinaweza kuwekwa kwenye container langu peke yangu au niko tayari kuchangia na watu wengine.
3) Kampuni ya hapo Dar yenye uzoefu wa kutoa vifaa vya aina hiyo
bandarini (clearing & forwarding) toka China
Mwenye huo msaada aniandikie kwa kutumia hii email address:
kwetuughaibuni@gmail.com
NB: MATAPELI HAWAKARIBISHWI KUCHANGIA.

MIE MTOTO WA MJINI BWANA OHOOO..
NTAWAGUNDUA MARA MOJA!
ukivileta bongo angalia watu wa TRA wasije wakakupiga kodi kubwa, cha msingi wewe kwanza nenda kwa mtu anaejua sheria za Tax kwanza, pili ujue sheria kama wakikubambika kodi, pia utafute contact za wakurugenzi kadhaa kurahisisha malalamiko pindi watakapo taka kuchelewesha vitu vyako kutoa, mimi nazungumiza hivyo kutokana na uzoefu wangu ninapoaagiza vitu nje ya nchi, usipofuata maelekezo yangu utajuta nivyema ukafanya hivyo.
ReplyDeletekwa hiyo nyumba moja labda kama unataka kujenga apartment au building for bussmess huna haja ya kwenda china, kila kitu kipo bongo pesa yako tuu.
ReplyDeleteKwenye list yako kuna vitu sioni umuhimu wa kuvinunua nje ya nchi, mfano milango, makochi, vitanda, n.k. Vitu hivi tuna mafundi wazuri tu Dar na viwanda vipo vinatengeneza vitu makini tu. Hivi unadhani China inauwezo wa kutota mbao nzuri kutengeneza fanicha zaidi ya Tanzania? Kumbuka kuwa unatakiwa pia kuthamini na kuinua soko lako la ndani. Kuna watu wanategemea kupata ajira kupitia ununuzi wako wa bidhaa za Tanzania.
ReplyDeleteImekuwa ni tabia kwa kila mtu Tanzania anataka kununua vifaa vya ujenzi nje...inakuwa kama kufuata mkumbo sasa na hakuna sababu za msingi. Nakubaliana na wewe kununua vitu kama masinki, taa, mapambo nje ya nchi kwani hatuna vifaa hivi Tanzania na wale wanaoimport wanaviuza bei ghali. Hivyo Tafakari kwa makini vitu unavyotaka kuvinunua nje na ufanye utafiti wa kutosha kama hivyo vitu havipatikani Tanzania.
Ni ushauri tu ndugu yangu maana natamani sana uchumi wa Tanzania nao ukue na watakaoweza kukuza uchumi ni watu kama nyie kwa kuthamini bidhaa za ndani.
Kama wewe mtoto wa mjini si ugoogle tu? Unashindwa nini kugoogle na kutranslate hayo mambo unayoulizia? Watoto wa mjini walienda bila directions na wakafika na kununua hivyo vitu....
ReplyDeleteHakuna cha bure siku hizi tafuta consultant wapo hapa kibao watakupa all the information unazozitaka kwa bei poa kabisa
Sema mdau, nimekutumia contact za mdau aliyeko China anayeweza kukusaidia angalia kwenye private email yako. Kama ukikwama sema. Mdau Oslo-Norway
ReplyDeleteSasa kama mtoto wa mjini kisha uko ughaibuni na wahitaji msaada tutani wewe kweli uko sawasawa? Rudi nyumbani nunuwa kila kitu hapa hapa kipo. China wanaenda wafanya biashara. Wewe umemention unataka kumaliza kakibanda Jeuri ya kwenda chinahunaaa! fanya mawazo mkato ya busara nunua hapo hapo kwenu nyumbani TZ italipa.
ReplyDeleteKabla ya kufanya safari nenda bongo kaangalie bei mwenyewe sio usuburi kuambiwa.
ReplyDeleteJumlisha gharama ya wewe kwenda China, hoteli(chakula,malazi, usafiri), Ongeza hela ya hasara kama hivyo vioo na masinki yatavunjika kwani hiyo inaweza kutokea, Gharama ya kuvitoa bandarini(Hongo kwa TRA,Bandari pamoja na ushuru) na kama bado gharama ni chini ya 15% ya ile ya bongo basi nenda China.
P.S. Usisahau gharama ya muda wa wewe kwenda china, vitu kusafirishwa kwenda bongo, wewe kusubiri kuvitoa bandarini.
ebwanae bongo mbona @kitu kipo pesa yako tu sasa hiyo pesa kuliko ukawatajirishe wachina si bora ukaleta home ikaongeza uchumi wa nchi kidogo halafu ukasevu na muda pia ,kumbuka gharama ya kuvtoa hivyo uchina 2 Tz ni saw na kununulia hapahapahome hao wachina wapo kibao TZ na wanamaduka ya vitu vyote hivyo pia kuna vinngine bomba kuliko hata vya hao wachina msidharau vyetu acheni hizo
ReplyDeletekaka usije kudanganyika na chochote kila kitu kipo bongo, mwenyewe nina nyumba sio kakibanda na kila kitu nimenunua bongo.... we vipi? kwanza umeondoka lini?? maana usijekuwa ulienda ughaibuni miaka ya themanini ukafikiri bongo michosho kha!! Bora ununue kila kitu hapa mkuu. ni ushauri wa bure tu.
ReplyDeleteKusema kweli kwa sasa hivi Bongo kila kitu kinapatikana, ni pesa yako tu na kujua nini kipo wapi. Tatizo lenu mkiwa huko ughaibuni bado mna mawazo kwamba Bongo bado kama ile zamani kwamba kuna uhaba wa bidhaa. Njoo na pesa yako na utapata kila unachohitaji.
ReplyDeletemimi sioni sababu ya wewe kuuliza hapa,ni mbwembwe tu zimekujaa.kila kitu kipo clear,gharama za kununua hivyo vifaa TZ haziwezi kizidi gharama za wewe kwenda china.use common sense,wewe mtoto wa mjini wa wapi!!
ReplyDeleteushauri wa wadau ni mzuri sana. Tz vifaa vyote vipo cha msingi hela unayo. Na ukinunua hapa utasaidia kunyanyua kipato cha mmoja wetu. Ila kama utaona kwenu ni ughaibuni basi nimekutumia contact za C&F company ili ununue huko uchina ili mswahili mwenzio aambulie japo vijisenti vya clearing.
ReplyDeleteHAUNA LOLOTE MSHAMBA TU WEWE! MASWALI YA KIJINGA.NYUMBA YAKO SASA SISI TUFANYE NINI AMUA MWENYEWE BWANA!!!!!!
ReplyDeleteKWELI MASKINI AKIPATA MATAKO HULIA MBWATA.
ReplyDeleteNA MATOFALI KANUNUE UCHINA PIA HAYO ULIYOJENGEA HAYANA KIWANGO, SI UNAJUA WANAFYATUA WABONGO!!
HII NI DHARAU KABISA. KUNA VITU KIBAO BONGO, MAFENICHA YA MININGA FRESH, UNATAKA SAIPRASI YA UCHINA.
KAMA ULITAKA KUTUTAMBULISHA KUWA UKO UGHAIBUNI WEWE SEMA TU, NA WALA SI YA VIFAA VYA UJENZI.
WATU TUNALIA NA KUKUZA UCHUMI, WEWE UNAFIKIRIA KWENDA KUFANYA MANUNUZI CHINA.
NENDA KAKA, HUNA HAJA YA KUTANGAZA.
NAUMIA SANA NA WATU WANAODHARAU VITU VYA KWAO.
OMBA MSAADA KUTAFUTIWA JAMAA YAKO ALIYEPOTEA, SIYO VIFAA VYA UJENZI.
KWAHERI
KWETU UGHAIBUNI
ReplyDeleteKwanza nakukumbusha kwenu sio ughaibuni, ila upo ughaibuni kwa mihangaiko halafu utarudi kwenu, yaani bongo. Sasa mkubwa ukitaka kujenga nyumba bongo, basi kila kitu mkubwa kiko hapa(unaongea na mtu alie UK, na kajenga nyumba 2).
Kuanzaia mchanga mchanga, cement, vifaa vya kazi, mbao, rangi, makabati, tiles, sinks, shower cubicles and shower trays, etc etc. Ukianza kujenga nyumba na kuagiza vitu mamtoni basi bajeti yako yote itaharibika kwa kutumia hela zaidi kwa vitu ambavyo viko bongo, na wingi,type, quality na kwa bei yako tu, usifikiri kwetu hakuna hivyo vitu.
Yale mambo ya zamani eti bongo hakuna vitu au vya quality wala yamepitwa na wakati. Wewe njoo na mahela tuu!
NAKUTAKIA KILA LA KHERI, NI KUWA NA BIDII TU, BASI UTAJENGA HIO NYUMBA NA IKIWEZEKANA ZINGINE PIA.
Nilivyomuelewa mimi jamaa anataka contacts za mahala huko China ambako anaweza kupata hizo materials ambazo ameziolozesha pili ametaka contacts za wasafirisha wa hivyo vifaa kutoka China kwenda Tanzania na tatu kampuni ya utoaji mizigo hapo Dar, kwa mtazamo wangu so mbaya kumpa ushauri ila kwanza angepewa hizo contacts kisha ushauri ukafuatia.
ReplyDelete