Mbunge wa Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa na Mbunge wa Rungwe Mashariki Profesa Mark Mwandosya na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kyela Mashariki Mh. Richard Kasesela wakipozi wakiwa Ikulu ndogo ya Chamwino mwishoni mwa wiki. Vichwa hivi vinasifika ka usongo walio nao katika kuongeza maendeleo ya elimu, afya na kilimo huko Rungwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. aligombea ubunge au alikuwa anaomba ridhaa ya kugombea ubunge kupitia CCM?na huo uheshimiwa Mr.Kasesela kautoa wapi?
    acheni hizo.

    ReplyDelete
  2. kasesela hawezi kuwa mheshimiwa. yeye ataitwa ndugu, kijana, bwana nk.nk lakini uheshimiwa hana.Michuzi inabidi tukupeleke pale kurasini ukajifunze ka-diplomasia kadogo...

    ReplyDelete
  3. Waheshimiwa wadau,
    Chama kinaamini kwamba binadamu wote ni sawa na kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Kwa misingi hiyo, Richard Kasesela naye ni mheshimiwa.

    ReplyDelete
  4. Nami naunga kidole Richard Kasesela sio Mheshimiwa kwa kuwa hakufanikiwa kuupata huo uheshimiwa. Nafikiri wewe unae bisha jaribu kulitafsiri hilo neno la mheshimiwa katika lugha yoyoye ya kigeni mfano kiingereza au kifaransa ndipo utakapojua kama bwana richie sio mheshimiwa.

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi, kwa heshima na taadhima naomba nifikishe masikitiko yangu kwa jinsi vile unavyotumiwa na baadhi ya watu ambao wanajaribu kung'arisha nyota zao za kisiasa ingawaje nyota hizo zimefulia na hazisafishiki. Bila ubishi, hii picha umeletewa na huyo Richard Kasesela ambaye anahangaika mno kujikweza kisiasa. Alijaribu kumng'oa Prof Mwakyusa lakini akagonga mwamba. Sasa leo kwa unafiki mkubwa anakutumia picha uiweke hapa barazani eti akijilinganisha na watu wa hadhi na heshima na waliolitumikia Taifa kwa uadilifu kama hao maprofesa. Huyo Richard hafai kuitwa kichwa cha Rungwe na tena wala si kichwa cha Mbeya. Braza Michuzi jaribu sana kutafakari kabla ya kutundika mapicha haya ya ajabu kutoka kwa viraka kama Richard Kasesela ambaye sasa anahaha kutafuta ubunge wa kuteuliwa.

    ReplyDelete
  6. Waheshimiwa ni wawili na vichwa ndiyo hivyo hivyo katika picha hiyo

    ReplyDelete
  7. asanteni wadau nimeyasikia, na pia sina haja ya kuitwa Mheshimiwa kwani Mungu ndiye mtoa heshima kwa hiyo msipate taabu buree. Nafurahi sana Bwana Asenga kwa kupiga pich hii nikiwa na wazee wangu. Pia Mimi kwa kurekebisha kidogo niligombea Rungwe Magharibi ambapo nimejifunza mengi hasa kuishi na kila aina ya watu wabaya na wazuri, wanaokutakia mema na wenye wivu. wanao kuchukia hata kama hujawatendea lolote na wanao kupenda.
    Mwisho kabisa siwezi hata tone kujilinganisha na Ma Profesa hawa waliofanya kazi na kuweka historia, nami nafuata nyayo zao, ila kikubwa ni wote tunashirikiana kuijenga Rungwe.
    Tukumbuke Uongozi unapangwa na Mungu na si mwanadamu, mwanadamu hutumika kuthibitisha mapenzi ya Mungu,
    Asanteni kwa maoni yenu
    Wenu mtiifu
    Richard Kasesela
    Mwenyekiti
    Pan Africa Business Coalition (PABC)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...