wakati Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiapishwa uwanja wa Amaan

Ankal, asalaam aliekhum....
Kwa heshima na taadhima nipeperushie swala langu hili. Pia naomba unitafutie picha muafaka ziende na huu waraka wangu. Unajua, kumekuwepo na mawazo na hisia mbalimbali juu ya mustakabali wa ndugu zetu wa Kizanzibari ambao baada ya uchaguzi mkuu uliojaa vurugu wa mwaka 2000 wengi walitorokea nje ya nchi kunusuru maisha yao kwa kile kilichoonekana kukosekana kwa usalama wa maisha yao.
Wiki hii tumeshuhudia historia ikiandikwa visiwani Pemba na Unguja ambapo sio tu uchaguzi mkuu uliendeshwa na kuhitimishwa kwa amani bali pia chama cha CUF kiliyakubali matokeo kwa moyo mkunjufu na kutamka hadharani kuwa kiko tayari kuunda Zanzibar mpya katika serikali ya kitaifa ambayo itaundwa na Rais Shein.
Hii inaashiria kwamba visiwani humo mambo ni shwari na kwamba kila upande umeafiki kwa dhati kusahau yaliyopita na kuganga yajayo kwa umoja wa kitaifa.
Swali: Je, hao ndugu zetu waliokimbilia nje ya nchi wataendelea kuhesabika kama wakimbizi wa kisiasa na kukubalika waendelee kuishi huko waliko kimoja?
Naomba kuwasilisha
Mdau Ilham wa Oman
Mimi ninawazo tofauti kabisa na huu muafaka na tuwe wawazi tusijidanganye. Tatizo la zanzibar ilikuwa ni uonevu uliokuwa unafanywa na CCM wakuwanyima haki yao Wapemba. Na hapa usifikiri haya yote ni kwasababu ya muafaka, Lah hasha ni kwakuwa sasa Zanzibar imeshikiliwa na wapemba Dr Shein na Maalim. Hicho ndio kilikuwa kilio cha wapemba siku zote.
ReplyDeletesasa na nyinyi muliondoka mapinduzi, vipi mbona hamrudi na mapinduzi ni 1964..
ReplyDeleteUkiwepo na wewe wa OMAN unafanya nini huko? huna mada bora upumzike. watu wanafanya siasa amani wewe unatafuta jengine. aliyepata uraia ndio basi hataki. unafikiri wana siasa wameendoka kwa ZNZ tu? hata Bara wapo watu hasa sehemu za sheria na ma bank wengi tu. James.
ReplyDeletewee inakuhusu nn?kwani ni mmoja wao? ndio hao bado ni wakimbizi....
ReplyDeletewewe ilham wa oman kwanza ningekupongeza kwa swali lako zuri na ninayo furaha kubwa kulijibu iwapo michuzi hatobana jibu utalisoma.
ReplyDeleteningependa kwanza ufahamu hakuna mzanzibari aliyekimbia nchi eti kisa kuna vurugu. hawa wazanzibari woote unaosikia wako huku uingereza,sweden, canada n.k woote wamekuja kutafuta mkate wao na sio kuikimbia fujo ya cuf na ccm. kama uamini chunguza kwa kuwailiza ndugu jamaa na marafiki walioko pande hizi je ni kweli wazanzibari huko ulaya wanaomba ukimbizi kama wazanzibari? jibu bila shaka utapewa si kweli. sitaki kuzitaja nchi wanazojilipua kama wakimbizi kwa sababu za kishushu ila nafikiri jibu langu ni sahihi.
mdau u.k
Ninaye rafiki yangu jinake Masudi "Pashamoto" Msele. Huwa hawezi kusema "runinga" (Tv) bali "atahalibu" Kiswahili kwa kusema " luninga"....labda... tumsamehe Masudi maana si mwandishi, mwanahabari au mtaalamu wa lugha.
ReplyDeleteIla tuwakanye wana habari, wataalamu, waalimu na waandishi wanaopaswa kuboresha na kustawisha lugha...na wasiojua kupambanua kati ya herufi L na R. Shurti tumsahihishe aliyeandika..MUSTAKABARI...hiki ni Kiswahili kibovu.
Sarufi sahihi ni "Mustakbal" au "Mustakabali"...
bado tutaendelea kukaa uingereza na huku umarekani hata msemeje, maana hatuna imani na Sirikali yenu...
ReplyDeleteTumeshapewa vibali vya kufanya kazi na kupata mshiko mzuri tuuu kwa hiyo mlie tu.
Mdau
HAO NDUGU HALI WANAIONA WENYEWE NA KUJIWEKA KUWA NI WAKIMBIZI NI HIYARI YAO HAKUNA MADHILLA WALA MASHAKA,KAMA KWELI NI WACHAPA KAZI WARUDI WAJE WAENDELEZE NCHI YAO, KATIKA UMRI WAKO ULIWAHI KUONA CCM NA CUF HUKU ZNZ WOTE WAKO MITAANI WAKISHANGILIA MATOKEO?HADI RAAHHA, LAKINI KUMBUKA WENGI WALIONDOKA NI KUJITAFUTIA MAISHA MAZURI KATIKA HAOHAO WAMETOKA BARA NA SEHEMU KADHAWAKADHA KWA KUTUMIA KADI ZA CUF,TATIZO AJIRA MPK SASA HUKU HAKUNA YA KUELEWEKA WATU WALIFATA MAISHA HUKO
ReplyDeleteNani kakwambia Maalim Seif ndo makamu wa rais mteule? CUF wanatakiwa wapeleke majina matau then Shein atachagua nani awe makamu wa rais,panapokuwa kuna mapungufu ya uelewa wa jambo flani ni vema habari zingine mkazipotezea na si kupotosha uma....Mapinduuuuuuuuuuuuuzi
ReplyDeleteWewe ulioleta huu mjadala imekuhusu nini kama wazanzibari waliokimbilia nje ya kuwa watahisabika au hawatohisabika kama wakimbizi?
ReplyDeleteKinachokuuma ni nini hasa kwa wao kuwepo nje ya nchi? Au unapata hasara gani kwa wao kuwa wakimbizi?
Sikutaka kujibu mada ya huyu mletaji lakini kwa upeo wangu nahisi mtowa mada alikuwa ni mmoja ya hao wakimbizi anaowasema au mzamiaji katika hizo nchi kwa bahati mbaya inawezekana hakufanikiwa kubakia huko au serekali za huko zilimrejesha nyumbani baada ya kugunduliwa kuwa hana kesi pia inawezekana amepokonywa mpezi wake au vyenginevyo kwa hali hiyo amebakiwa na Donge la moyoni kuona vijana wanaoishi huko wanatuma chochote kwa ndugu zao na wazee pia inawezekana ni choyotu cha kibinadamu fulani kafika kule mie sijafika lakini basi kwa vyovyote vile wenzio kule wanaishi maisha tafauti na sisi tuliopo nyumbani maisha ya hap nyumbani ni yakubahatisha unapoamka hukijuwi nini utakula unapoumwa hapo tena ndio unaona kiyama kimefika walioko nje ni kunyanyuwa simu kwa dakitari pole mtowa mada kinyogo kwa binadamu tumeumbiwa nacho
ReplyDeleteWewe mdau wa "Tarehe Thu Nov 04, 06:29:00 AM" unachekesha. Sasa nani alie? Kuwepo kwako na kutokuwepo kwako nchini hakupunguzi wala hakuongezi kitu. Mangapi yamefanikiwa ilhali nyie mmekimbia nchi? Wewe endelea kubaki huko ukipata huo unaouita mshiko mzuri, lakini pia kaa ukijua na huku maisha hayajaganda na watu wanasonga mbele. Uliowaacha wapo form 4 sasa ni graduates na wana kazi zao vile vile. Tena ni kazi za kukaa ofisini na kupulizwa na kiyoyozi sio kubeba box au kuosha vizee vya kizungu. Hivyo, usifikirie kuwa tunawahitajia saana mrudi, bakini hukox2 mlikopewa vibali nasi tuacheni na nchi yetu ambapo tupo huria kufanya kazi bila kuhitaji kibali. Pole sana kwa fikra zako kuwa watu wanakulilieni mrudi...
ReplyDeletewewe upo oman ulikimbia mapinduzi mwaka 1964 sasa mpaka leo ni mwaka 2010 je bado unaishi huko kama mkimbizi au umeona maisha umeyapatia ??????
ReplyDeletekuhusu suala la wakimbizi hamna mkimbizi wa tanzania nchi yeyote duniani hilo unatakiwa ulijue waache watu wajitafutie riziki zao kwa njia zao wanazozijuwa wenyewe
hali ya huko nyumbani tanzania sio hali ya kusema kila mtanzania anaweza kuwa na kazi ya maana na kukidhi mahitaji yake sasa tukisema wote tujazane huko je nani atakaetoa kazi kwa watanzania wote?
waache watu wajisaidie huko nje ya nchi ili waweze kupata mapato mazuri na kuweza kuwekeza kwao na kujenga nchi yao na hata kusaidia familia zao ambazo zina shida ya vyakula madawa na mahitaji mengi muhimu
mimi kwa upande wangu nawaombea ndugu zetu waishio nje ya nchi waendelee kuishi kwa maisha bora na mafanikio
ANKAL naomba mfikishie huyu mdau wa oman apate kujuwa kilichomfanya atoe mada hii ni kwamba hataki kujuwa tamati ya hawa watanzania waishio nje isipokuwa ni wivu wake uliomjaa
unajuwa miaka ya zamani ilikuwa wanzanzibar wengi namaanisha wa unguja na pemba walikuwa wakiomba visa za kutembea oman na wengi wao walikuwa wakiwalilia waoman kuwafanyia stay ya oman ili waweze kuishi oman
sasa waoman wengi walikuwa wakiwatumia sana hawa wazanzibar kwa kuwa walikuwa na shida sana ya kufika huko oman na matokeo yake waliwatumia kwa njia tofauti
wengi wao waliwatumia kiwmili na wengine waliwatumia kuwafanyia kazi za nyumbani
sasa waoman wengi wenye asili ya kitanzania wamekuwa na wivu mkubwa kuona wazanzibar wa sasa au watanzania kwa ujumla hawababaikii tena hiyo oman na sasa wanaweza kuishi nje ya nchi kama uk usa nk...
sasa wao roho zinawauma kuona kuwa hawapati kunyenyekewa tena na watanzania
mdau wa mahakama kuu ya dunia nawakilisha kwa mdau wa oman.
kama walienda kwa gia ya ukimbizi lazima warudishwe kisheria maaana sasa kwao kupo shwari na hakuna mtu anaependa kubeba mzigo wa mtu. Kazi kwenu mliojilipua!!!!!!!!
ReplyDeleteNa kama hamjajilipua wasi wasi wa nini??
Mkataa Kwao Mtumwa.
mdau wa Thu Nov 04, 02:44:00 PM kwa taarifa yako tu hakuna hata mtu mmoja katika huo unaowasema kuwa wamejiripua aliesema katika vyombo vya sheria huko waliko kuwa wanatoka tanzania au zanzibar, kwani kwa muda wote huo wa miaka 15 ya michafuko ya siasa tanzania, watanzania hawakuwa wakikubaliwa kama ni wakimbizi, kwa maana nyengine ulimwengu hauukutambua kama tanzania kuna hali mbaya kiasi cha kuwaruhusu wananchi wake kuishi nchi nyengine kama wakimbizi. watu walikuwa wanajifanya wasomali, waburundi n.k!!!! Fanya utafiti kwanza kablay ya kuropoka ovyo hapa!!!!
ReplyDeletekama hujui unachikisema ni bora unyamaze mtu yoyote anaweza kuwa mkimbizi kwani kuna sababu nyingi za kukufanya uwe mkimbizi hata wamarekani na wangereza na wao wapo ukimbizini kila mtu anasababu iliyomfanya aondoge kwao sikwakutaka au kupenda ana sababu ,kwanchi nyingiUNAPOKUWA MKIMBIZI HUWEZE KUWA MKIMBIZI MILELE KWAMFANO WALIOKIMBIYA ZNZ NI WENGI RAIYA WANCHI WALIZOKIMBILIYA NA WANAHAKI SAWA NA WAKAAZI WA NCHI HIYO
ReplyDelete"Je, hao ndugu zetu waliokimbilia nje ya nchi wataendelea kuhesabika kama wakimbizi wa kisiasa na kukubalika waendelee kuishi huko waliko kimoja?"
ReplyDeleteHili swali ni gumu sana. Unatuuliza sisi au serikali ya Zanzibar au Tanzania...kwani ndio waliwapa stauts ya ukimbizi?
Kutangua ukimbizi ni shauri la serikali zilizokupokea.
Kutangua ukimbizi ni shauri ya hao wanaojidai wakimbizi kutangua ukimbizi wao na kujirudisha nchini kwao.
Wakimbizi wa kisiasa/dini rudini mjieleze kwa nini mlikimbia!
Kuna wakimbizi wengine wa ki-uchumi...kutafuta majani. YHao ni vigumu kurudi!
dada unapokuwa mkimbizi kwamuda jina lako linabadilika unakuwa mkaazi kwamuda uliopangwa na nchi uliyokimbiliya unapofikisha muda unabadilika na kuwa raiya waile nchi unahaki kama raiya mwengine tatizo la tanzania hamuhechimu haki za binadamu na kuwa wagumu hakufikiriya ndiyo mana nnanajisiwa na mafisadi ha hamjuwi duniya enapoelekeya
ReplyDeleteMbona huo ndugu zetu wakali sana au yamewagusa!!!!
ReplyDeletesisi tuliokuwepo huku uk tunamshukuru ALLAH tumepokelewa vizuri na tunawashukuru waingereza, sasa linakuja swali kwako jee! kuna mkimbizi yoyote aliyepokelewa hapo oman? tuache wa kisiasa wapo nduguzenu kama vile wafalestine wanapigwa na waisrail mmewapokea hapo??? kumbukeni MTUME (S A W)Aliondoka macca na akapokelewa Madina, wacheni HUSDA nyinyi Waoman, MTUME (S A W)Anasema haiingii peponi yeyote mwenye chembe ya husda.mdau Leicester.
ReplyDelete