KAMPUNI ya Vanedrick Tanzania Limited imeandaa tamasha maalum kwa ajili ya kumpongeza rais Jakaya Kikwete na wabunge wote wa mkoa wa Dar es Salaam.
Tamasha hilo limepangwa kufanyika Novemba 21 kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam huku wachezaji mbali mbali wa Ligi Kuu wataunda timu ya Dar All Stars chini ya Jamhuri Kiwelu 'Julio' na watashuka dimbani kumenyana na timu ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes'.
Akitangaza kikosi kitakachoivaa Zanzibar Heroes Julio alisema makipa ni Ally Mustapha 'Bartez' na Ivo Mapunda wakati wachezaji wengine ni manahodha Jerry Tegete na Musa Hassan 'Mgosi'
Wengine ni Fredy Mbuna, Juma Jabu, Haruna Moshi 'Boban' Rashid Gumbo, Ibrahimu Mwaipopo, Meshack Abel, Juma Seif, Salum Abubakari, Monja Liseki, Nsa Job, Pius Kisambale, Himid Mao, Amri Kiemba, Mohamed Kijuso, Adam Kingwande, Athuman Idd 'Chuji', Kelvin Yonda, Kally Ongala, Salum Sued na Ramadhani Chombo 'Ridondo'.
Wakiongea mara baada ya kutangaza kikosi hicho manahodha wa timu hiyo Mgosi na Tegete waliwataka watu kujitokeza kwa wingi kwa kuwa wana imani mechi hiyo itakuwa na mvuto na pia wachezajji watafahamu uwezo wao.
"Ni mechi muhimu sana kwetu kwa kuwa kila mmoja atajua uwezo wake na pia ni nafasi nzuri kwa timu ya Zanzibar Heroes ambayo inashiriki Chalenji, mchezo huo utakuwa moja ya maandalizi yao na watajua makosa yao na kuyarekebisha kabla ya mashindano ya Chalenji yatakayofanyika Novemba 27,"alisema.
Julio alisema kingilio katika mchezo huo ni shilingi 10,000 kwa viti maalum, shilingi 8,000 jukwaa la kijani na shilingi 3,000 kwa mzunguko.
Please wadau, naomba matokeo ya kura za Unaibu Spika mjengoni, Dodoma
ReplyDelete