Ndugu Watanzania wenzangu na wote
wenye mapenzi na nchi yetu mlioko hapa ITALY

Tumejaaliwa kupata fursa ya kusherehekea sikukuu ya Idd El-hadji huku tukisubiria sikukuu ya Noeli na Mwaka Mpya.

Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania Italia na viongozi wote wa jumuiya na matawi yake, na kwa niaba yangu binafsi napenda kushirikiana nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kufikia kipindi hiki muhimu.
Katika kipindi chote tangu jumuiya yetu ianzishwe tumekuwa tukijitahidi kuwajibika kwa kushirikiana na Ubalozi wetu Rome kwa namna mbalimbali. Napenda kuchukua nafasi hii kuushukuru ubalozi wetu na Mh.Balozi ALI KARUME kwa ushirikiano.

Katika kipindi hiki pia tumejitahidi kupigania kuimarisha mshikamano wa Watanzania na hatimaye kufanikiwa kufungua matawi ya Jumuiya ya Watanzania sehemu mbalimbali . Ni matumaini yetu kuwa Watanzania watailinda na kuiinua Jumuiya yao kwa mafanikio yao na Taifa letu kwa ujumla.

Watanzania tuna sifa kubwa ya kuheshimiana, kuvumiliana na kushikamana bila kujali itikadi zetu za kisiasa, imani zetu za dini au kabila au rangi. Ni matumaini yetu tutaendelea kudumisha mshikamano wetu siku zote tukifanya kazi kwa bidii ili tuchume ugenini na kuweza kuijenga nchi yetu.

Katika kusherehekea sikukuu hizi muhimu natumaini tutakuwa na fursa nzuri ya kutembeleana na kuimarisha mshikamano kati yetu.
Nawapeni nyote mkono wa Eid El Hadji, mkono wa sikukuu ya Noeli na kuwatakia kheri ya Mwaka Mpya ujao.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
ABDULRAHAMAN A.ALLI
Mwenyekiti (JUWATAI)
Kagutta N.M

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mmmmmh!!!!!!!!!! mbona haieleweki nani mwenye kikoda hapo? haa!! haa!!! mambo ya napoli

    ReplyDelete
  2. Barakatul Eid minal faedheen...yaa abdulrahman, mbona hukutuambia waislamu tulioko Tanzania umetuombea michango ipi kuimarisha dini huku nyumbani na pia nilidhani ungefanya hafla fupi ya kumwalika mheshimiwa balozi na kuwachangisha jumuia yenu huko ili zije ziwafae waislamu wa huku. Mfano mimi msikiti wetu wa Kinyerezi mnembwe unahitaji msaada mkubwa tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...