Washiriki wa Shindano la Giraffe Unique Model wakiwa katika pozi la picha.


Zoezi la kuwasaka wanamitindo wenye sifa za kipekee, limekamilika jana katika hoteli ya Giraffe Ocean View baada ya wanamitindo kumi kupatikana katika mchujo wa awamu ya pili ambapo mchujo wa awali ulifanyika jumamosi iliyopita.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Unique Entertainment,Methuselah Magese amesema kazi ya kuwasaka wanamitindo hao ilikuwa ngumu sana kiasi ambacho iliwachukua mpaka kusafiri kwenda mikoa ya jirani kama Tanga,Dodoma na Pwani.

Giraffe Unique Model ni shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ambapo jumla ya washiriki kumi watapanda jukwaani siku ya tarehe 24 Desemba katika katika fainali za shindano hilo zitakazofayika katika hoteli ya Giraffe Ocean View,Mbezi Beach jijini Dar.

washiriki waliopita katika mchujo huo ni Dorah Mhando,Ritah Samwel,Bilkis Suleiman,Carina Suleiman,Asia Dachi,Calorine Mwakasaka,Diana Mainason,Mariam Rabii,Purity Walele na Jackline Giyabe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mkubwa mwenzangu asante sana Mkubwa.

    Sasa usitusahau tu Wakubwa wenzio pale watakapokuwa kwenye "BICH WEA"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...