Washiriki wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge Kilometa 196 kwa wanaume wakichuana vikali katika mbio hizo zilizofanyika jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa kamati ya ufundi Taifa Godfrey Jax Mhagama akitoa maelezo kwa washiriki wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge kabla ya mbio hizo kuanza rasmi zilizofanyika jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro, akiinua bendera kama ishara ya uzinduzi rasmi kwa mbio za Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa wanaume na wanawake.
Washiriki wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge Kilometa 196 kwa wanaume wakichuana vikali katika mbio hizo zilizofanyika jijini Mwanza.
Washiriki wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge Kilometa 196 kwa wanaume wakichuana vikali katika mbio hizo zilizofanyika jijini Mwanza.
Mshindi wa mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa upande wa wanaume Hamiss Clement(shinyanga) akimalizia mbio hizo na kuibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia Masaa 5:19:43,kwa kilometa 196.
Mshindi wa mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa upande wa wanawake Sophia Hadson(Arusha)akimalizia mbio hizo na kuibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia Saa 2:32:14 kwa kilometa 80.

Mwandishi Wetu, Mwanza

HAMISI Clement wa Shinyanga leo ( jana) alinyakua taji la' Vodacom Mwanza Cycle Challenge' lililokuwa likishikiliwa na Mussa Milao wa Arusha na kuzawadiwa sh mil 1.5 na waandaaji wa mashindano hayo baada ya kutumia saa 5:19.43.

Clement katika mashindano hayo alishiriki mbio za umbali wa Kilomita 196, abazo zilianzia Nata hadi Nyashimo ambako alitumia baiskeli ambayo si ya mashindano ambako liwaacha mbali wenzake wengi waliokuwa na baiskeli za mashindano.

Mshindi wa pili wa mashindano hayo kwa wanaume ni Richard Laizer aliyetumia saa 5:20.12 ambaye alizwadiwa sh mil 1 huku wa tatu Said Konda wa Shinyanga abaye alitumia saa 5:20.30 ambaye alizawadiwa sh 700,000.

Kwa upande wa Wanawake Sophia Adison wa Arusha naye alinyakua taji la mashindano hayo baada ya kushika nafasi ya kwanza ya mashindano hayo baada yakutumia saa 2:32.14 na kuzwadiwa sh mil 1.1, taji ambao lililuwa likishikiliwa na Beatrice Kennedy wa Dodoma ambaye mwaka huu amenyakua nafasi ya tano ya mashindano hayo.

Mshindi wa pili kwa wanawake ni Martha Anthony wa Mwanza ambaye alitumia saa 2:34.27 ambaye alizawadiwa sh 800,000 huku wa tatu alikuwa ni Ndyashimbi Kurya wa Mwanza alinyakua nafasi ya tatu baada ya kutumia saa 2:36.34.

Adison katika mashindano hayo alishiriki mbio za umbali wa Kilomita 80, kutokea Nata hadi Nyanguge ambako uzoefu ulimsaidia kunyakua taji hilo.

Akizungumza baada ya mashindano hayo, Clement alisema kilichomsadia ni mazoezi ya mara kwa mara aliyokuwa akiyafanya ingawa milima ilimsumbua katika mashindano hayo.

Clement alisema kwa ushindi huo atawashauri wenzake wa Shinyanga kununua baiskeli za mashindano kwa sababu, baiskeli za kawaida zinasumbua, fedha alizozipata atatumia kununulia baiskeli za mashindano.

Naye Adison alisema mashindano ya mwaka kwake yalikuwa na upinzani mkali kwa sababu ushindani ulikuwa ni wa hali ya juu hasa wenye baiskeli za Phoenix ambao walikuwa hawampi nafasi.

Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Steven Kingu alipongeza ushindi wa Clement kwa sababu mara nyingi ushindi huenda mikoa mingine ambako pia alitoa wito kwa washiriki wa mikoa ya Kanda ya ziwa kuwa na baiskeli za kisasa na za mashindano ili wafanye vizuri zaidi katika mashindano ya Kimataifa.

Kingu alisema mara zote Vodacom kila mwaka wanatoa zawadi zaidi ya mwaka uliopita ili kuleta chachu ya washiriki kujiandaa vilivyo kwa mashindano yajayo na kutoa wito kwa mashindano ya mwakani.

Mgeni rasmi katika mashinano hayo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Kanali Mstaafu Serenge Mrengo.

Mashindano hayo yalishirikisha washiriki 403 kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam, Dodoma, Mara na Kagera.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Michuzi huyo jamaa Hamis Clement ni koko! Katumia baiskeli ya kawaida kuwashinda wenye ya 'kuinama' mashindano. Duh kweli kuna watu wana vipaji. Huyo jamaa akipata ya mashindano anaweza liletea sifa sana Taifa kimataifa.

    Mzozaji

    ReplyDelete
  2. Wasukuma nawaaminia kwa mbio za baiskeli.

    Hongera sana Hamisi umewashinda jamaa hata bila ya viatu, UMEIKANDAMIZA baiskeli kisawasawa.

    Amenikumbusha yule mkimbiaji wa Ethiopia wa miaka ya 70 au 80 jina lake akiitwa Abebe. Mara ya kwanza kwenda kwenye marathon ya kimataifa alikimbia bila ya viatu na alipata ushindi wa kwanza. WAzungu walimshangaa sana.

    Nakubaliana na Mzozaji kwamba huyu kijana akijengewa uwezo basi ataweza kufika mbali sana.

    ReplyDelete
  3. no helmet, no special cycle, no shoes, but enough energy. safi saana afya hiyo.

    ReplyDelete
  4. eeh bwana kama kweli jamaa ameshinda kihalari nina zawadi yake, kwani nasikia huwa wanasaidiwa kwa kusukumwa na gari sehemu za maporini halafu wanagawana hela ya ushindi. ila nampa pongezi zake kwani km 196 na phonex, bila viatu,bila chupa ya maji, na pensi tu kwa masaa 5.19 amefanya vizuri,kwa haraka haraka tu yaani km 196 ameendesha min 38km/h, hiyo inamaanisha akiwa na baiskeli nzuri,vifaa vinavyotakiwa kama viatu, commonwealth game ya km 167 road race atakuwa zaidi ya min 47km/h kwa maana hiyo yeye ndiye atakaye chukua medal ya gold, chama cha baiskeli Tanzania, naomba mlifanyie kazi hilo vijana wapo wa kutuletea sifa taifa letu. michuzi naomba kama una contact za mshindi wa kwanza mpaka wa tatu unipatie, au kama wanaweza kuwasiliana nami sio kwa kuwakopa fedha walizoshinda bali ni katika kusaidiana kuendeleza vipaji vyao mimi pia ni muendesha baiskeli hapa ughaibuni. email ni adamsilver00@yahoo.com, Yaani bado siamini km 196 peku peku, na phonex, masaa 5 duh Hamis noma.

    ReplyDelete
  5. halafu yeye obvious ni natural energy. wenzetu hawa red bulls na hard drugs wajanja sana.
    Huyo yuko peku peku, baiskel hiyo lakini kashinda...asert kwa taifa huyo. Wakimtunza na kumpa mazoezi ya nguvu na siye tunaye mshind french tour mwakani. but coach wake atoke hapo hapo bongo msije kuimport ati coach wa kumfundisha tutaloose tu.

    mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  6. Somo zuri kwa kila mtu hapa. Usije ukaacha kufanya kile unachotaka kufanya katika maisha jwa kisingizio cha kuwa huna vifaa. Determination yako itakupeleka popote ulimwengu huu. Hao wengine na mountain bikes zao lakini hawakumwenza huyu aliyekimbia bila helmet, viatu na special gears. YES YOU CAN

    HONGERA

    ReplyDelete
  7. wasukuma kwa bangi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...