
Familia ya marehemu Bw.Hassan M.Mbulalina, tunatoa shukurani zetu za dhati kwa wote waliojitokeza kutusaidia na kutufariji wakati wa kumuuguza na hatimaye katika kipindi cha msiba wa baba yetu mpendwa aliyefariki 30/09/2010 na kuzikwa 1/10/2010 mjini Dodoma.
Familia inawashukuru madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa juhudi walizofanya kunusuru maisha ya baba yetu.
Aidha familia inatoa shukurani za pekee kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO). Kwa kuwa si rahisi kumtaja kila mmoja hivyo basi tunaomba wote mpokee shukurani zetu za dhati na Mungu awajalie mafanikio katika shughuli zenu za kila siku.
Arobaini itafanyika 14/11/2010 nyumbani kwa marehemu kilimani-Dodoma.
“INNALILAH WAINALILAH RAJIUN”
jamani poleni kwa msiba wahusika, michuzi lete matokeo ya uchaguzi bwana nini lakini...au machozi yanakulenga ccm inaelekea kubaya...huku nje hatuoni local news,tunakutegemea habari motomoto utupatie bwana ah!
ReplyDeletewewe mtoa maoni wa hapo juu jaribu kuheshimu msiba wa wenzako ..usiandike masuala ya uchaguzi wa kipumbavu kabisa kupitia msibani wewe mjinga mmoja na huko kuweko nje usione ni kitu kikubwa au cha ajabu
ReplyDeletewenzako tumeshakaa huko na tumerudi kwetu wewe usijigambe kukaa nje wewe ni mtumwa tu na utabakia kuwa mtumwa wa watu
kwani huna tabia wala heshima mjinga mkubwa wewe
huyo jamaa kweli kakosea, hapo suala la uchaguzi haikuwa sehem yake lakini haikuwa na haja ya kutoa matusi yote hayo kwani inaonesha ujinga wa huyo mtoa matusi,huu uchaguzi sio wa kipumbavu kama ulivyosema,ungemrekebisha tu.tunaombwa tusibadilishe mada jamani bado tunamsikitikia mzee wetu.
ReplyDeleteyani mi nadhani huyo wa kwanza ni jini labda,manake katika hali ya kawaida huwezi ukaunganisha mautumbo yako ktk swala la msiba.he or she is stupid.
ReplyDelete