Ili kuhakikisha wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars wako imara na wana afya bora wakati wa mashindano ya CECAFA, TFF itawalinda wachezaji hawa dhidi ya ugonjwa hatari wa MALARIA.
Hivi karibuni wakati wa mazoezi yakujiandaa na mechi kati ya Liverpool na Chelsea, mwili wa mchezaji Didier Drogba ulipoteza nguvu kwasababu ya ugonjwa wa MALARIA na akashidwa kucheza mechi hiyo. Cha kushukuru ni kwamba dalili za MALARIA ziligundulika mapema, akatibiwa na sasa amepona anaendelea kucheza kama kawaida.
Sasa timu ya Chelsea, kwa kushirikiana na mshirika wao mkuu wakutoa misaada “Right to Play” wameamua kuusaidia kampeni ya United Against Malaria (Tushirikiane Kutokomeza Malaria). Kampeni ya Tushirikiane Kutokomeza Malaria unajumuisha viongozi maarufu, wanasiasa, mashirika mbalimbali na wachezaji maarufu. Watu hawa waliungana pamoja kabla ya mashindano ya Kombe la dunia-Africa ya Kusini ili kupigana vita dhidi ya ugonjwa wa MALARIA unaoua mtoto mmoja wa Afrika kila baada ya sekunde thelathini.
CECAFA imechukua kampeni ya Tushirikiane Kutokomeza MALARIA kama kauli mbiu yao kwenye mashindano ya mwaka huu.
Kuhakikisha ugonjwa hatari wa MALARIA haushambulii kambi ya Kilimanjaro Stars, TFF itagawa neti za kuzuia mbu wa MALARIA kwa kila mchezaji katika kambi yao. “Kuanzia sasa sisi TFF tutaanza kupanga utaradtibu wa kupambana na MALARIA tukishirikiana na UAM na wa Watanzania wenzetu” alisema Sunday Kayuni. Neti hizi zitakazotolewa na TFF zimetolewa na kampuni ya AtoZ.
Nae mchezaji Didier Drogba alisema “Neti ya mbu inaweza kuonekana kama kitu kidogo lakini neti huweza kuokoa maisha ya watu wakiwa wamelala kutokana na mbu waambukizao MALARIA. Neti ni muhimu sana kwenye nchi ambazo zinasumbuliwa na ugonjwa hatari wa MALARIA”.

Mimi bado sijaelewa ni vipi watu wawili walio chumbani mmoja akiwa amelala na mwingine ameketi akijisomea mbu anamuacha aliyeketi na kumuuma aliyelala au akimuuma aliyeketi hatamuambukiza malaria bali atakayeambukizwa ni yule aliyelala! Bado ninaamini kuwa kuwauwa mbu huko waliko kwenye mazalia yao ni muhimu zaidi kwanza kisha chandarua. wataalamu nielewesheni mimi.
ReplyDeletehuyo jamaa anaitwa SAAD MAARUFU KAWEMBA
ReplyDelete