Juhudi za Bodi ya Utalii za kuitangaza Tanzania zinaendelea kwa nguvu zote huko Uingereza. Hii ni lkujitangaza katika jezi za Blackburn Rovers. Picha na Ayoub Mzee



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kwanza nianze na kuwapongeza bodi ya utalii Tanzania kwa juhudi zao. Ila kuna dosari moja ambayo hasa sie watanzania tunaisahau kila siku, nayo ni maandalizi kabla ya kufanya kazi, hata kama jamani unataka kuingia uwanjani kucheza huwezi kunyanyuka kwenye benchi moja kwa moja uwanjani lazima upashe misuli moto. Kinachonisikitisha ni kwamba hao tunaowatangazia wanatakiwa kupata hizo taarifa kwenye website iliyotajwa hapo juu..wakati mwingine website hiyo ipo wakati mwingine haipo, hiyo ni kasoro kubwa sana, kwani mtu akiikosa mara moja ujue harudi tena kuitafuta. Kingine, kwenye hiyo website wameweka lugha mbali mbali, ila ukibonyeza ni page ya mbele tuu ndiyo yenye lugha husika, page nyingine ni kiingereza, sasa mie najiuliza, kabla ya kufikia kutangaza koteeee...kwa nini wasingefanya maandalizi kwanza? Kwanini hiyo website isingekamilika kwa at least 90% ndiyo waanze kuitangaza, kwani ni aibu na wanaonyesha hawakua makini katika kupanga. Mungu ibariki Tanzania. Mdau Oceania.

    ReplyDelete
  2. naona wanawekeza nguvu nyingi huko Uingereza. ningeshauri waje hata huku nchi za benelux kwa vile kuna watu wengi wanaopenda sana kwenda Tanzania ila hawana ufahamu wa kutosha kuhusu jinsi ya kwenda.

    mbali na matangazo vile vile waingie ubia na mashirika ya ndege ili wapunguze nauli zao kwenda bongo. hili suala la nauli linatufanya watani zetu watupige bao. marafiki zangu wengi huniambia kuwa nauli za tanzania zipo juu sana na wakaamua kwenda Kenya.

    mdau

    ReplyDelete
  3. sasa mbona bwana michuzi na ayoub mnatuchanganya? tupeni taarifa za uhakika. Taarifa inasema sponsor ni blackburn, ilhali picha ya pili inaonyesha dhahiri bango linasema birmingham city. Sasa tuamini lipi picha au taarifa? au tanzania tumeweza kusponsor timu mbili?

    ReplyDelete
  4. Mkataba ni wa shilingi/ dola/ pounds milioni ngapi? Nomaly mikataba yote huwa inawekwa wazi, ila naona haya maelezo na mengine yote niliyoyasoma hayajazungumza hilo. Unaweza kuta kuna ufisadi mkubwa sana ndani yake. To me this is not a proper move to a very poor country like Tanzania. Thamani ya mkataba ingeweza kuboresha huduma ya afya na elimu kwa kiwango kikubwa sana.

    ReplyDelete
  5. brother michuzi hii taarifa mbona mimi naona kama imepakwa mafuta sana?

    Unataka kutwambia kuwa blackburn na birmingham city watakuwa wakivaa jezi zenye sponsor yetu wakicheza mechi kuanzia sasa? Unataka kuniambia kuwa tumeweza kuwalipa fidia masponsor wao walio nao sasa na kuchukua nafasi yao? Unajua ni kiasi gani inagharimu kusponsor timu lakini seuze kulipa fidia ya sponsor unaemuandosha ilhali muda wake haukufika?

    Ayoub ripoti kiuhakika sio kutudanganya, eleza ni vipi blackburn na birmingham city wamekubali kutangaza tanzania kwa kupitia timu zao.

    ReplyDelete
  6. Si official website ya birmingham wala blackburn iliyoripoti kuwa sponsor wa shati zao wamekuwa TTB. Whats going on here?

    ReplyDelete
  7. Mdaua Kaongelea kweli mmoja Hapa Nchi kama Ujerumani.Uengereza na Italy ndio zinazokuja sana watalii nchini Tanzania bila hayo matangazo wanakuja muhimu ni kwenda Nchi kama East European na South America au North America katika majimbo yao.

    Pia website muhakikishe zinafanya kazi sio tunapoteza tu pesa Nyingi sana kutangazia viwanja kama hivyo Britain. Far East pia Singapore matajiri wengi. na Pia tusinganganie Mt kilimanjaro tu Lake Victoria kwau bavu wetu na Mwanza Mbuga za wanyama hasa ya mikumi na Mafia pia. Mdau MZ.

    MZ.

    ReplyDelete
  8. Sina muda wa kukaa na kuweka maelezo marefu, ila naomba kusema tu kuwa taarifa hii inapotosha inahitaji kuripotiwa tena. ahsante sana

    ReplyDelete
  9. Naomba kuungana na wachache hapa waliohoji ukweli wa habari hii.

    Kwanza kabisa ni vigumu sana shirt sponsorship ya timu yeyote ile kubadilishwa katikati ya msimu bila ya sababu nzuri sana kama kuingia administration sponsor wa awali. Unaweza kufikiria ghadhabu za wapenzi wa club waliolipa pesa tele kwa jezi mpya na ghafla jezi zao ni out of date na hazifanani na timu wanayo isupport.

    Pili hii habari kwanza tuliambiwa ni birmingham city na sasa tunambiwa ni blackburn. Hata picha zilizowekwa hapa zinaleta conflict na habari tunayosoma.

    tatu takriban mara zote timu zilizo daraja moja huwa hazitakiwi kuwa na shirt sponsor mmoja, kuepusha conflict of interest katika ligi, hii ndio maana hata kuna wakati arsenal walipocheza champion league na timu fulani ambao pia wanasponsiwa na fly emirates, walibidi kuweka nembo nyengine walipocheza nyumbani na walipkcheza ugenini ile timu ya kule iliweka nembo nyengine.

    Nne siamini kama shirika la utalii la tanzania lina pesa kiasi hico cha kuweza ku-sponsor timu mbili za premier league. Na kama wameweza basi im am smelling a rat!!! itakuwa ni story ya radar part two!!!!!

    ReplyDelete
  10. Hivi Walengwa ni nani katika hii kampeni??!! Je ni wapenzi wa Blackburn/Stoke huku UK au ni wanaoangalia kwenye TV katika nchi mmbalimbali? Je ni wangapi kwa wastani wanaangalia mechi za timu hizi hapa UK na pia nje?!
    Je TTB wametumia gharama kiasi gani na wanategemea kupata nini?
    Je TTB inajua watu wanaotoka maeneo haya wapenzi wa soka ni watu wanaotembea nje ya nchi??! Maana sio la kushangaza hapa mtu wa East London haendagi West London. Na watu wengi wa maendeo haya kipato chao ni cha chini na ndio maana viwanja kama Blackburn havijai japo ukubwa wake ni elfu ishirini tu sasa hao ndio uwaambie ticket kwenda Bongo ni zaidi ya £500 wewe anakushangaa umewezaje kuja hapa. Ukiwa hapa london unaweza kwenda Pub Arsenal au Liverpool inacheza na ukakuta hamna anaeangalia kwa sababu hapa upenzi ni wa kikabila hivyo watu hawaangalii timu ambayo si ya kwao.
    Tusiwe tukawa sisi ndio tunafurahia jina letu kuonekana kwenye TV au jezi bila kuelewa tunafaidika vipi. Maana unaweza ukawa na mzigo wako wa simu mpya za Blackberi basi ukaenda kule kwetu kule mitaa ya nanihii kutangaza......badala ya kwenyewe wanaoweza kuzinunua.
    Akili ni mali kila mtu ana.............
    Mzawa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...