Rais Jakaya Kikwete akipiga makofi mbele ya kombe la Tusker CECAFA Challenge Cup 2010 mara baada ya kuzindua rasmi michuano hiyo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo,wengine kutoka kulia mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya CECAFA, Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Richard Wells na kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko SBL Caroline Ndungu, Mkurugenzi wa Mahusiano SBL Teddy Mapunda pamoja na Rais wa TFF Leodger Tenga.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Richard Wells huku wakiwa wameshikilia kombe la Tusker Challenge.

kikosi cha Kilimanjaro Stars.

kikosi cha Zambia.

Nahodha wa timu ya Kilimanjaro Stars,Shadrack Nsajigwa (14) akimuongoza Rais Jakaya Kikwete kuwasalimia wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars leo.

Kiungo wa Kilimanjaro Stars, Mohamed Banka (kulia) akichuana na mchezaji wa timu ya Zambia, Thomas Nyirenda.

Mshambuliaji wa Kilimanjoro Stars, Gaudence Mwaikimba akijaribu kuwatoka walinzi wa timu ya Zambia, Venecious Mapande (kushoto) na Brian Musonda wakati wa mchezo wa michuano ya kombe la Chalenji uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Zambia ilishinda 1-0.

Ni huzuni tupu katika benchi la timu ya Kilimanjaro Stars.

Kocha wa Kilimanjaro Stars Jan Poulsen (kulia) akipeana mkono na kocha wa Zambia baada ya mpira kumalizika. Picha na Francis Dande wa Globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Semeni wadau, "Hili ni kosa la Maximo. Maximo hafai!"

    ReplyDelete
  2. Ancal ulizaliwa karibu na muembe nini? maana kwa ujanja nakufagilia yaani umeiminya masg yangu ila umenifurahishasana kwa kutoa hii habari ya kufungwa na zambia!
    unajua bwana baadhi ya wadau tumechunguza tumeona kwamba kumbe suala la kufungwax2 wadau wanalitaka wenyewe kwa kumpangia kocha wachezaji badala ya kumuacha kocha angalie mwenyewe, ndio maana hatuta kaa kamwe tukapata kusonga mbele, mechi moja tuu kocha alipanga timu na wadau wakamuona amevaba kumbe mwenzao ana ujuzi wake! ni ile mechi kati ya Tanzania na Algeria Timu ilipangika, sasa angalia timu ikipangwa na wadau ni mivurugano isiyofaa.

    Tumuachie kocha timu na si kumshinikiza kupanga timu hata yeye mwenyewe anajua hapa sijui!!!


    Tunaomba sana chama cha mpira pamoja na waziri MCHIMBI wainusuru stars walau ili KOMBE libaki TZ.

    ANGALIA HATA WATZAMJI HAWAKO WENGI UWANJANI KWANI TIMU INAKATISHA TAMAAAA!!!



    tatizo ni sisi wenyewe NA SI KOCHA!!!!!!!!



    Mdau usa! thax alot michuzi!!!

    ReplyDelete
  3. Yaleyale nilisema nikaonekena sijui. Tanzania tutafute kitu cha kufanya. Aibu basi hata raisi yupo lakini bakora tunakula.

    Kisiju

    ReplyDelete
  4. Sikio la kufa halisikii dawa.
    na lakuvunda halina ubani,
    mpira umetushinda jamani.
    tugeukie kwenye riadha tu.
    Tazama majirani zetu Ethiopia na Kenya wanavyo jitangaza.

    ReplyDelete
  5. Wandugu, yaani Banka anakipiga? hapa tumeisha hatuna kocha hajui anachofanya, sasa mliokuwa mnamchukia Maxmo kazi kwenu

    ReplyDelete
  6. Mwaikimba sio kwamba mpira hawezi bali ana gundu

    ReplyDelete
  7. tatizo si coach bali na system mzima , haiwezekani makocha wote wanaokuja wanachemsha. wabongo mzizi wa fitina sana ,na wanaendekeza njaa kuliko utaifa wao.
    mdau paris

    ReplyDelete
  8. TAnzania ni hivi , kuna wale wanapenda maendeleo , na kuna wale wasiyopenda maendeleo watafanya kila fitina kuwavuruga wapenda maendeleo.
    watanzania ni watu wabaya sana , believe me , wanafiki sana.na awaoni mbele wao wanaendekeza njaa tu !

    Mdau Paris

    ReplyDelete
  9. Inasikitisha lakini haiumizi,
    kwa huu mwendo tunaokwenda itafikia muda watazamaji watakuwa watu wa TFF na vyombo vya habari labda na wale wanaopata complimentary.
    tatizo si kocha isipokuwa ni msingi wa wachezaji wetu hawajatayarishwa.
    hakuna nchi yeyote inayoonekana imepiga hatua katika michezo bila ya kuwekeza katika soka la watoto na vijana kwa madaraja ya umri wao.
    tutakuwa tunajidanganya na kupata ushindi wa "kuulopu". lakini ukweli wenyewe hakuna tutakachofaulu kwa mfumo wetu huu, kila kitu kinaeleweka nini tufanye. muhimu hapa tuamue kutekeleza yale yaliyomo kwenye makabrasha ya programu. kwas kuanzia tuanzie na ile aliyoiacha Profesa Victor kama bado ipi hapo TFF.
    Na huu ubabaishaji nina imani unafanywa makusudi kwa sababu unatoa mwanya wa ulaji, na ndio msingi wa wote wanaokimbilia nyadhifa katika tassisi mbalimbali.
    TUBADILIKE

    ReplyDelete
  10. Assalaam Alaikhum,wewe mdau Paris naona itakubidi ubalishe lugha yako.unaposema NANUKUU Watanzania watu wabaya sana, wanafiki sana,awoni mbele na wanaendekeza njaa tu na unachanganya lugha ktk Kiswahili hakuna neno (believe me) wewe ndie unayefaa kupewa sifa zote hizo ulizozitaja na sifa moja umeisahau wewe ni mtoto wa kikopo chupa yoyote utakayoingizwa utanyoosha kidole kutuashiria kuwa na wewe upo kama usingekuwa unaendekeza njaa yako usingefika huko Paris,nimecheza mpila wa miguu ktk maisha ya UJANA najua sababu za kushinda na kushindwa usiropoke na kutuka Watanzania je Wazazi wako wametoka wapi wao nisababu ya wewe kuja DUNIANI na kukupa ELIMU halafu UNAWATUKANA UTAOKOTA MAKOPO WEWE!!!!MDAU USA.

    ReplyDelete
  11. Wabongo ngojeni Zenji ikuonesheni kazi. Nynyi si kwa mpira bwana ni kwa pombe, mademu, na kuinyanyasa Zanzibar tu chini ya Muungano.
    Mdau
    Zenji

    ReplyDelete
  12. Tarehe Sun Nov 28, 12:43:00 PM, Mtoa Maoni: SULTAN

    wewe mdau wa USA, niliyosema sijakosea , oana mwenyewe unanitisha kwa uchawi eti nitaokota makopo, mimi namwamini mungu wala si nguvu za giza, mimi ni mtanzania na nawajua watanzania wenzangu , siwote , hila walio kuwepo madarakani awana uchungu na uzalendo kwa nchi yao. wana endekeza njaa sana. so upende usipende huo ndo ukweli. Si kwamba makocha awajui kufundisha , hila system ndo inaongoza vibaya , mmekalia majungu na fitina.

    Mdau paris

    ReplyDelete
  13. wewe mdau wa USA , acha uchawi wako humu , unataka kumokotesha mwenzako makopo kisa katoa mtazamo wako.
    wewe dini gani kwanza unafikiria uchawi hivyo?

    ReplyDelete
  14. Tehee hee hee. Mpira wa bongo bila kuingiza kamati ya ufundi hauendi. Kuna mdau kaonywa ataokota makopo humu tehee heee hee.
    Babu alipoanza kazi watu walidai kwamba ameibadilisha timu inacheza kitimu zaidi. Wako wapi wale watu? Wakati ule mlikuwa mnaona mabaki ya kazi ya Maximo. Kocha yeyote anayejua kazi yake hawezi kukubali kupangiwa listi wala kuchaguliwa wachezaji. Maximo alifanya hivyo ikadaiwa ni kichwa ngumu lakini tulikuwa hatufungwi ovyoovyo nyumbani. Sasa hivi kila anayekuja anatupiga kimoja anapumzika.

    ReplyDelete
  15. Ndoto ya mchana.SwedenNovember 28, 2010

    Kitu gani Watanzania wanakiweza?itakuwa ni majungu na umbea,ubabaishaji,ombaomba,ufisadi,umasikini na uvivu.
    Michezo,maendeleo imewashinda.Ukiwa nchini na nje ya nchi utayaona hayo.Ndio maana wengine tunakuwa hatuna muda na wabongo huku nje ya nchi,wengi wao hamna cha maana mnachoongea zaidi ya kutaka kupika majungu na umbea.Nchi zingine wana msimammo zaidi kuliko Wabongo.
    Ndoto ya mchana,Sweden.

    ReplyDelete
  16. Nawakubali mnaosema kuwa wabongo ni wanafiki na watu wa majungu. Naongeza kuwa hata hawajui wanachokitaka na hujifanya kujua kila fani hadi wasizo na ujuzi nazo, matokeo yake aibu tupu.
    Maximo alipiga kazi ya kufa mtu, wachezaji wabongo mabomu, hilo tukubaliane nalo, ndiyo sababu hata wakienda kufanya majaribio nchi za nje hawachukuliwi. Kwa ufupi wanahitaji nguvu ya ziada kuwafundisha kwa kuwa ni wabishi na wanajua kila kitu kama wengi tuliomo humu kwenye mablogu.

    Haya, mmefukuzisha kazi maximo bila kujua chimbuko la matatizo yenu, sasa mnaanza kulalamika nini?

    Mkitaka kabumbu bongo, tuanze na new generation, yaani watoto ambao bado hawajajifunza ubishi naa kujiona, hapo tutaweza kuwafundisha na wakacheza soka bomba mno.

    ReplyDelete
  17. Aden Rage aliwahi kusema kuwa watanzania tunataka mafanikio ya haraka haraka katika soka bila kukubali kuwa inatakiwa 'sacrifice'. Alitoa mfano wa mtu anayetaka kwenda peponi bila kufa - kitu ambacho hakiwezekani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...