Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermes Mwansoko akiwasilisha mada leo jijini Dar es salaam juu ya umuhimu wa Sera ya Utamaduni katika kuchangia maendeleo mbalimbali nchini.
Baadhi ya wadau wa semina ya siku moja wakifuatilia kwa makini mada kuhusu umuhimu wa sekta ya utamaduni katika kuimarisha uchumi na kupunguza umaskini. Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam na kuhudhuria na wadau mbali kutoka UNESCO na wadau wa ndani.
Mshauri wa Masuala ya Utamaduni wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu , Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Moji Okuribido akitoa mada leo jijini Dar es salaam juu nguvu ya utamaduni katika kuchangia maendeleo mbalimbali na kupunguza umaskini kwa wananchi wa eneo husika.


Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika limesema kuwa sekta ya utamaduni ina nafasi kubwa ya kusaidia kuleta maendeleo na kupunguza umaskini kwa wananchi ikiwa itaijumuishwa kikamilifu katika mipango mbalimbali ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mshauri wa masuala ya Utamadani wa UNESCO kanda ya Afrika Bibi Moji Okuribido wakati akitoa mada kuhusu nguvu ya utamaduni katika kuleta maendeleo.

Bibi Okuribido alisema kuwa ni vema wapangaji mipango wakakuchukua maoni ya jamii husika na utamaduni wao wakati wakiandaa miradi mbalimbali kabla ya kuanza kuitekeleza ili suala la utamaduni wa sehumu husika hapa baadaye usiwe kikwazo katika utekelezaji kwa jamii.

"Ni vema wakati wa kutekeleza miradi kusikiliza mtazamo wa jamii kuliko kuamua mambo ambayo wakati mwingine yanakwamishwa kwa kuwa hayaendani na utamaduni wa eneo husika" alisisitiza mshauri huyo wa UNESCO.

Aliongeza kuwa suala la utamaduni linapaswa kuwa kiungo katika mipango ya maendeleo kwa kuwekeza kwa muda mrefu kwa sekta hiyo ikiwemo kuweka miundombinu inayosaidia kukua kwa utamaduni nchini.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Malikale, Ndugu Donatius Kamamba alitoa wito kwa sekta mbalimbali kuangalia tathmini ya athari za utamaduni kabla ya kuanzisha miradi ili kufanya inapoanzishwa iungwe mkono na jamii kwani itakuwa imetokana na mtazamo na taratibu za utamaduni husika.

Alisema kuwa baadhi ya miradi na mipango imeshindwa kudumu kwa kuwa suala la utamaduni halikupewa kipaumbele kabla ya uanzishwaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wenzetu wanajua kuwa utamaduni unanafasi kubwa ya kulete maendeleo katika jamii...lakini sisi wenyewe watanzania tumebobea sana katika kuiga utmaduni wa nje ye nchi,tuhamke sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...