Mgombea Ubunge wa CHADEMA katika Jimbo la Musoma Vincent Nyerere ameibuka na ushindi baada ya kujizolea kura 21,335 na kuwazidi kwa mbali wapinzani wake wengine wane.

Katika uchaguzi huo Vedastus Mathayo wa CCM amejipatia kura 14,072, Mustafa Wandwi wa CUF amepata kura 253, Chrisant Nyakitita wa DP nae amepata kura 52 pamoja na Tabu Machibya wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 19.

Matokeo hayo yametangazwa rasmi na msimamizi wa jimbo la musoma mjini, Nathani Mshana ambapo wakazi wa Musoma hasa wapenzi wa CHADEMA wamekuwa wakisherehekea ushindi huo tangu jana usiku.

Mbunge mteule Vicenth Nyerere ameahidi kushikiana na vyama vyote vya siasa kuhakikisha jimbo la Musoma mjini linapata Maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...