


WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 31,kutoka Jumuiya ya Ulaya ( EU EOM) na Umoja wa Afrika wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki, utulivu na amani.
Waangalizi hao walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana(leo) kuhusu taarifa ya awali ya uchaguzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, David Martin alisema uchaguzi huo ambao ni wa nne kufanyika nchini tangu mfumo wa vyama vingi kuanzishwa Tanzania, hadi sasa kwa ujumla umefanyika kwa amani na mpangilio mzuri.
“ Siku ya Uchaguzi Mkuu ilijitokeza kwa utulivu mkubwa na kwa ujuml a waangalizi wa uchaguzi wa Ujumbe Maaalumu wa Jumuiya ya Ulaya(EU EOM) ulikadria mchakato mzima wa uchaguzi huo kuwa ama ulikuwa ‘mzuri’ au ‘ kuridhisha’ katika asilimia 95 ya vituo vyote vya kupigia kura walivyovitembelea upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar,” alisema Martin.
Aliongeza kuwa kwa ujumla taratibu muhimu katika vituo vya kupigia kura zilitumwa kwa ulinganifu kwa kila kituo cha kupigia kura nchini kote, licha kuwepo mapungufu machache.
Martin alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilisimamia chaguzi kwa namna ya kitaalamu, hivyo kwa sehemu kubwa ziliwapatia watu watu wote haki ya kupiga kura.
Aliongeza kuwa ujumbe huo utabakia nchini kuzidi kufuatilia kwa karibu zaidi zoezi la kuhesabu matokeo ya uchaguzi, utangazaji wa matokeo na matukio yoyote yatakayojitokeza baada ya uchaguzi.
“Taarifa hii ni ya awali .Taarifa ya kina ya mwisho itatolewa baina ya miezi miwili na miezi mitatu baada ya mchakato mzima wa uchaguzi kukamilika,” alisema.
Kwa upande wake Kiongozi wa waangalizi hao, kutoka AU, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Sierra Leone, Dk. Ahmad Tejan Kabbah alisema uchaguzi huo umefanyika wa amani na umefanyika kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa Tanzania .
Aliongeza kuwa umefanyika kwa kuzingatia Azimia la Durban Demorasia katika Chaguzi za Afrika la Julai mwaka 2002.
“ Waangalizi wa Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi umefanyika kwa huru, haki , uwazi na uadilifu(Credible) .
Naye Katibu Mtendaji wa International Conference of the Great Lakes Region (ICGLR) Balozi Liberata Mulamula amesema wiki hii kwamba wameridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi mkuu Tanzania na kwamba ukiondoa matatizo madogo madogo yaliyojitokeza sehemu mbili tatu, ulikuwa huru na wa haki.
Balozi Mulamula amesema uchaguzi wa Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama wa ICGLR ambao wengi watakuwa na uchaguzi katika kipindi hiki. Ameisifu serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na kuruhusu kila mwananchi aliejiandikisha kupiga kura bila wasiwasi.
Waangalizi hao ,waliwapongeza wananchi wa Tanzania, Vyama vya Siasa, wagombea , NEC, ZEC na vyombo vya usalama kwa kuwezesha uchaguzi huo ufanyike kwa amani na kuwashauri wagombea kukubali matokeo yanayotangazwa na NEC.
Uchaguzi ulikuwa wa haki na amani wakati hatujapata matokeo uchaguzi, hii ni siku ya nne hata nusu ya matokeo ya urais hatujui yanakwendaje, je vurungu zikitokea kwa kutoridhika upande wowote watasemaje kuhusu hiyo amani. Nadhani hu siyo muda mhafaka wa kusema hivyo mpaka wasubiri matokeo yasomwe na tume waone kama kuna haki au hakuna
ReplyDeleteHIVI KWANINI MAGAZETI YA KENYA DAILY NATION,NA STANDARD KWENYE MITANDAO YAO WAMEWEKA PICHA ZA FUJO ZA MBAGALA MTU MMOJA KAFA TARIME,UCHELEWESHAJI MATOKEO UTALETA VURUGU YANI NEGATIVE TU,KANA KWAMBA WANATAMANI FUJO ITOKEE WHY?KUNA PICHA NZURI YA HISTORIA YA NCHI YETU MAALIM SEIFU ANAKUMBATIANA NA RAIS MTEULE DR.M.SHENI BWANI HOTEL WOTE WAKIWA NA TABASAMU LA MATUMAINI MAPYA YA KISIWA CHA MARASHI YA KARAFUU,HAWATAKI HATAKUZUNGUMZIA HILO,SISI NI WATANZANIA TUNAJIVUNIA UTAIFA WETU KAZI KUBWA ILIOFANYWA NA WASISI WETU HATUA BUDI KUIDUMISHA BADO TUNAO WAZEE WETU,SALIM,MWINYI,WARIOBA,NASORO MOYO,SALIMINI,MALECELA, AMOOR,MKAPA,KIMITI,NK HAWAWEZI KUKAA KIMIYA KULIONA TAIFA LINATUMBUKIA KATIKA MATABAKA MIMI MJALUO YULE MKURIA,ALIKADHALIKA UDINI.TANZANIA WE ARE BETTER OFF WITHOUT KENYA INAWEZEKANA TUMEWAKARIBISHA UWANI SASA WANATAKA KUINGIA CHUMBANI HATUJA LALA WANAGU MTA....,MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.ZIDIMU FIKRA ZA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE NA SHEIKH ABEID KARUME,WATAKUFA NACHO KIBA CHA ROHO.
ReplyDeleteSASA HAWA WANATOA MAONI YAO WAKATI BADO KURA ZINAENDELEA KUHESABIWA. KWANI ZOEZI LA KUHESABU KURA SI SEHEMU YA UCHAGUZI? SIELEWI KWA NINI WAMETOA TAMKO LAO KUWA CHAKULA KIMEPIKWA VIZURI WAKATI WANAONA CHOMBO BADO KIPO KWENYE MOTO KINACHEMKA NA VIUNGO VYAKE HAKIJAIVA. WASUBIRI VIKISHAWEKWA MEZANI, WATU WAKISHAKULA NDIO WASEME, 'WELL, CHAKULA KILIKUWA KITAMU'.
ReplyDeleteWAAMGALIZI HAO WAMEKOSOA MAMBO KADHAA YALIYOJITOKEZA KATIKA KAMPENI NA UCHAGUZI IKIWA NI PAMOJA NA KASORO KATIKA ZOEZI LA UCHAGUZI.
ReplyDeleteWAANGALIZI WA ULAYA WAMESEMA VYOMBO VYA DOLA VINGALI NA ITIKADI ZA MFUMO WA ZAMANI WA CHAMA KIMOJA NA HIVYO KUTOTOA SAWA HAKI KWA VYAMA VYOTE VYA SIASA.
PIA WAMETOA KASORO YA KUKOSEKANA KWA BAADHI YA MAJINA YA WALIOANDIKISHWA KUPIGA KURA, AU BAADHI KUHAMISHIWA NJE YA VITUO WALIVYOJIANDIKISHA.
PIA WAMEKOSOA UCHELEWESHAJI WA MATOKEA HASA KATIKA JIJI LA DAR AMBAPO MIUNDOMBINU NI YA UHAKIKA KULIKO VIJIJI AMBAKO MAWASILIANO NI DUNI.
TUWE WA KWALI KATIKA MASULA YA KIMATAIFA NA TAIFA LETU.
Asante Michuzi
Kuna Wakati mpaka najiuliza hivi Mwenyezi Muumba atawaacha hivi hivi?
ReplyDeleteMie wala sisemi mengi, endeleeni kuuita wa huru na amani ila ndani mioyoni mwetu tunajua na tutaendelea kuamini haukuwa wa huru, Zanzibar inachukua masaa kujua matokeo ila Kawe Masiku!
Michuzi, uzuri wa dhamira huwa haidanganyiki, kula mshahara kaka, kula pesa kaka ila deep inside moyoni mwako unajua uhalali wa unachopost na kuandika, uzuri wa dhamira, hata ukimlipia ada mwanao na akaja kuwa ana maisha bomba, dhamira bado itakukumbusha kuwa ile pesa uliyomsomeshea, ileeeee enzi ileee, haikuwa halali na hutaifuta dhamira mpaka utubu na uamini umesamehewa. Poleni sana wachakachuaji! Mmefanya kazi sana! ila hakuna ufalme ambao umesimama daima ukiwa haufuati maamuzi ya watawaliwa! Inauma sana na siamini kama sisikiki na mbingu. Segerea mnamtangaza mbunge ambaye yupo chini ya polisi kakamatwa kwa kuharibu uchaguzi...Michuzi Mwogopeni aliyetuumba na kutuweka duniani, kumbukeni mali si kila kitu, utu ndio kitu cha thamani. Mtu anaweza kufa akiwa jangwani, akiwa na begi la dhahabu, hakuwa na maji japo alikuwa na begi la dhahabu. Malaria inaweza kukuua hata kama una mali na VX ila huna dreva tu wa kukukimbiza hospitali, vyoyote vile ili ufike popote unahitaji watu, unahitaji uwe wazuri kwao nao wawe wazuri kwako. Naumia sana ila vitabu vya dini vinasema tuzitii mamlaka. Nazitii ila ukweli naujua.
Waangalizi wa Kimataifa wa Umoja wa nchi za ulaya wamesema Chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala wa vyombo vya serikali katika kampeni na uchaguzi.
ReplyDeletePia wameshtushwa na ucheleweshwaji wa matokea kitendo kinachotafsiriwa kama ni ukokotoaji wa matokeo halali. (Soma IPP Media na Gazeti la Mwananchi).
Waangalizi wa Jumiya ya Madola wamesema hapakuwa na uwanja sawa katika kampeni kwa vile chama cha CCM kimetumia pesa nyingi sana katika kampeni na vyama vingine havikuwa na pesa ya kutosha kufanyia kampeni. Na pia mfumo wa sheria uliopo bado unapendelea chama kimoja cha siasa kwa maana hiyo inatakiwa iwepo sheria inayoendana na mfumo wa vyama vingi.
Wamesema mkanganyiko wa daftari la wapiga kura ni kasoro inayotakiwa kufanyiwa kazi na pia dosari ya ucheleweshaji matokeo hufanya watu washindwe kustahimili kusubiri kitu kinachoweza sababisha watu kuanza vurugu.
Kwa mantiki hiyo tuwe tunaelewa lugha za watu wa kimataifa kwani huwa hawakuelezi kitu moja kwa moja ila wanatumia lugha ya kifalsafa.
Wewe Wed Nov 03, 03:49:00 PM mbona na sisi huwa tunapozungumzia vurugu za uchaguzi huwa tunatoa mfano wa Kenya na kuziacha vurugu za Zanziba kama vile hazikutokea? ukweli ni kuwa zilitokea na zilikuwa kubwa watu waliuawa na wengine walikimbilia Kenya. Tuache kulalamika ukweli unapotolewa na wengine, tulikataa kuwa kanda ya ziwa watu hawali mapanki wakati ni kweli wanakula na si Tanzania pekee hata Kenya vivyo hivyo. Ukweli unapotolewa husaidia kuleta ufumbuzi badala ya kuuficha.
ReplyDelete