Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
Mh. Anna Makinda, akiwasili kazini Dodoma.
Picha na Mo Blog


JINA LA WAZIRI MKUU LILILOTEGEMEWA KUPELEKWA NA IKULU ASUBUHI HII HUKO BUNGENI DODOMA LINATEGEMEWA KUMFIKIA SPIKA ANNA MAKINDA LEO JIONI AMBAPO BAADA YA KULITAMKA ATAWATAKA WABUNGE WALIIDHINISHE.



VILE VILE LEO JIONI NAIBU SPIKA ATAPIGIWA KURA NA KUCHAGULIWA RASMI. BUNGE LIMESITISHWA HADI HAPO JIONI AMBAPO PAMOJA NA KUJULOIKANA KWA WAZIRI MKUU NA NAIBU SPIKA, PIA UCHAGUZI WA WABUNGE WATAOWAKILISHA NCHI KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI PAMOJA NA SADC WATAJULIKANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. ALLAH AKBAR KABIIR WALHAMDULILLAH KATHIIR WASUB-HAANALLAH BUQRATTAN WAASWIILA
    Yarabi nakuomba umpe JK busara katika maamuzi amteu tena Mizengo Kayanza Peter Pinda na aachane na huruma ya kumpooza mtu kisa kakosa huku.

    Wabillah tawfiq

    ReplyDelete
  2. kayanza kayanda pinda anafaa. jk inabidi tu ampe haki yake hata kama walimuumiza mwingine wasiegemee kwa mtoto wa mkulima. PINDA OYEE.

    ReplyDelete
  3. Madaraka matamu bwana, Cheki LIBENZI HILO mama analoshuka..! Dah.... Yaani Sarcozi anatembelea Citroen na Peugeot, Cameron anatembelea Jaguar na Landrover.... Sisi Spika tu anatembelea Mercedes ya £laki mbili!??? yaani zaidi ya Milioni 200 za Kitanzania!??? Eeh Mungu tunusuru na Hawa MAFISADI.

    ReplyDelete
  4. KILLA LA KHERI KIONGOZI WETU RAISI TUNATARAJIA WEREVU NA BUSARA ZAKO ZITATUMIKA KUTUPATIA KIONGOZI MWEREVU,MWADILIFU,MCHAPA KAZI NA MFATILIAJI,KUNA KITU TUNAPIGIA MAKELELE GHARAMA ZA WABUNGE NI NYINGI HIVI KUNA HAJA GANI KUWEPO HIVI VITI MAALUMU?IDADI YAKE INAFIKIA ZAIDI YA VITI 100 NI KUPOTEZA PESA BURE,IKIWA MSHAHARA WA MBUNGE NI MILIONI 12 KWA WABUNGE 100 KWA MWAKA NI KIASI GANI? KWA MWEZI NI BILIONI 1.2 KWA MWAKA NI ZAIDI YA BILLIONI 14 MIAKA 5 NI BILLIONI BILLIONI 70 JEE ZINGEJENGA HOSPITALI NGAPI,ZAHANATI NGAPI,VISIMA VYA MAJI VINGAPI NK TUANGALIE HILI

    ReplyDelete
  5. amin, amin, amin, amin na iwe hivyo anon wa hapo juu....

    ReplyDelete
  6. Kweli ni haki walikuwa wanagombea u-spika. Hilo W211 ni la kuranda nalo baada ya kupiga maneno bungeni.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  7. We anon "Tue Nov 16, 11:15:00 AM" ahsante saana kuelezea hiyo issue. Mimi mpaka leo sijawahi kupata jibu kwanini tuna hao wabunge wote 100 wasiochaguliwa.

    Kwanza gharama zao ni kubwa

    Pili wanawakilisha jumuia ambazo tayari zimewakilishwa, kama ni wanawake lazima wanatokea sehemu ya TZ ambayo hiyo sehemu obviously ina mbunge tayari wa kuchaguliwa. Au kama ni alibino, hata wao tayari lazima maeneo yao yana wabunge waliochaguliwa.

    Tatu tunakaribisha asilimia kubwa ya watu kuingia bungeni bila kuwa na uwezo intellectually wa kuchambua sera. Profile za wabunge maalumu wengi (kipingi kilichopita) nimezisoma, wengi hawana shule ya kutosha. Kama mtu amameliza form four na kufail sijui kama anaweza akaandika muswada wa page 100 akauleta bungeni..

    something isn't right

    ReplyDelete
  8. I've written comments juu ya hivyo viti maalum(kuteuliwa) but Mh Michuzi didnt post.I know he does deserve the right not to or to. Ni upuuzi kweli kuwa na viti maalum wakati hatuna "jamii maalum" nchini. Kila mpiga kura anajua anakwenda kumchagua nani kumwakilisha bungeni lakini bado katiba inampa rais/bunge kuteuwa wabunge maalum.We really need constutional reform.Kuna vitu vyingi vinahitaji kubadilishwa ili hii nchi iende mbele kisiasa na kimaendeleo.Kwa maoni yangu nadhani panahitajika pawe na uchaguzi wa wakuu wa mikoa na wilaya badala ya kuwa na hawa wabunge wa kuteuliwa.Mishahara na malupolupo(maruporupo) wanayopewa hawa wabunge wasiokuwa na kazi yoyote bungeni ingetumika katika chaguzi za wakuu wa mikoa/wilaya.
    **Michuzi post hii kitu tafadhari***

    ReplyDelete
  9. Sonderklasse Hiyo, W221
    Kumbe ndio maana watu huwa wangangania madaraka. Uongozi mtamuu jamani!!

    ReplyDelete
  10. Jamani hizo benzi hatujanunua. Tulipewa msaada na Ghadafi wa Libya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...