Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Semamba Makinda(Mb.)

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inatoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Anne Semamba Makinda(Mb.), kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi uliofanyika Mkoani Dodoma tarehe 12 Novemba, 2010 hivyo kuweza kuwa Spika wa kwanza mwanamke nchini.

Ushindi wa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) ni kielelezo cha jitihada endelevu za Sekta ya Maendeleo ya Jamii katika kuhamasisha jamii kutoa nafasi na kutambua uwezo walionao wanawake katika kushiriki nafasi mbalimbali za uongozi na maamuzi.

Wakati jamii ikiendelea kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kumthamini mwanamke, bado kuna desturi na mila zenye madhara ambazo zimekuwa zikitweza utu na uwezo wa mwanamke katika kushiriki nafasi za uongozi na maamuzi. Ushindi wa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) umekuwa kielelezo thabiti kwamba Tanzania inaendelea kuwathamini wanawake na kuwapa dhamana; maana wanaweza.

Wizara ya Maendeleo Jamii, Jinsia na Watoto inatambua mchango wa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) kwamba anastahili kuwa Spika wa Bunge maana sehemu zote alizopitia ameonesha uadilifu na ufanisi na hivyo kuweza kuaminiwa kuwa Spika wa kwanza mwanamke nafasi ambayo ni kati ya mihimili mitatu ya uongozi wa taifa.

Wizara inatambua kuwa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) alikuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto kwa kipindi cha mwaka 1990- 1995 kazi ambayo aliisimamia kwa umahiri mkubwa hadi kufikia kuwepo kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto iliyopo hivi sasa.

Wizara inaamini kuwa elimu ikiendelea kutolewa, jamii itaweza kujenga imani kwa wanawake na hivyo kuweza kufikia Mkakati wa kitaifa wa kuongeza Uwakilishi wa Wanawake katika Nafasi za Uongozi na Maamuzi; na wanawake kuendelea kushiriki katika kusimamia na kumiliki fursa za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika ngazi mbalimbali.

Aidha, ushindi wa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) unaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye katika uongozi wake amejenga imani kuwa wanawake wanauwezo na aliowapa uongozi kamwe hawakumwangusha.

Imetolewa na

Hussein A.Kattanga

KAIMU KATIBU MKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Pongezi kwa Mh. Spika Anne Makinda kutoka kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na watoto ni mfano mzuri wa kuigwa na wadau wengi na hasa wanaothamini mchango mkubwa utolewao na wanawake nchini. Pongezi hizi zimekuja wakati muafaka ambapo jitihada za kuwathamini wanawake kama wanaweza katika Uongozi na kufanikisha maendeleo zimepamba moto. Aidha pongezi hizi ziwe ni mfano pia kwa wanawake wengine kuthubutu katika nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchini na nje ya nchi. Tunaamini kuwa uongozi ukiendeshwa kwa kanuni huleta usawa katika utekelezaji na hivyo usawa ukiwepo hujenga UPENDO miongoni mwa jamii, na UPENDO huimarisha Ufanisi na Ufanisi Hufanikisha malengo. Binafsi nimefurahishwa na pongezi hizi ambazo zitawafanya wanaharakati wanaopenda maendeleo kuunga mkono ili kumpa faraja mh. Spika mama Anne Makinda aweze kuongoza Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ufanisi zaidi.Ni imani ya watanzania na wapenda amani kuwepo kwa Mh. Anne Makinda ambaye alikuwa Naibu Spika katika bunge lililopita kutaleta chachu ya kuendeleza yote mazuri ya bunge lililopita na kuimarisha mapungufu ya bunge lililopita na kuwa na Bunge imara zaidi.

    ReplyDelete
  2. lol she so beautifully

    ReplyDelete
  3. Mdau wa 09.01, I second you on that..
    but i think we need fresh blood on some of these position. We have re-circled long enough now.

    Mdau N.A

    ReplyDelete
  4. even more than beatiful!!!)

    ReplyDelete
  5. She's also 100% natural. Ngozi yake na nywele zake ni zile alizopewa na Mwenyezi Mungu. Kina dada, mama Anna makinda anakimbilia miaka 70 lakini anaonekana at least 10 years younger. Kwa hivyo, mkitaka kuzeeka vizuri wacheni kuchubua ngozi zenu na "kupika" nywele zenu. God bless mama Anna.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...