Meneja Miradi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Clayton Kimber (kulia) akimuonesha moja ya miradi inayoendelea kujengwa katika kiwanda cha TBL, Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SABMILLER Plc, Graham Mackay (katikati) anayemiliki zaidi ya viwanda 60
vya bia Duniani. Mackay anayeishi Uingereza alitembelea Kampuni hiyo leo kuona utendaji kazi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SABMILLER Plc, Graham Mackay (kushoto) anayemiliki zaidi ya viwanda 60 vya bia Duniani, akizungumza na Mpishi Mkuu wa bia za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Gaudance Mkolwe baada ya kuitembelea kampuni hiyo leo jijini Dar. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja (kulia) pamoja na Trevor Gray ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SABMILLER Plc, Graham Mackay anayemiliki zaidi ya viwanda 60 vya bia Duniani, akiangalia bia aina ya Castle alipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es
Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...