JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA
KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA
MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAI
Hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imegundua kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunzaji wa siri za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi. Mawasiliano hayo yamefikia hatua ya kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya Simu na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za mawasiliano binafsi ya simu bainA ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.
Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinasema;
(1) “Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii”
(2) “Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria”
Kifungu cha 123 (1) kinasema:-
Mtu yeyote ambae bila sababu za msingi atasababisha kuingilia au kuzuia kupokewa kwa mawasiliano yeyote ya kielektroniki anafanya kosa and akipatikana na makosa atatakiwa kulipa faini ya shilingi za kitanzania zisizopungua milioni tano au kwenda jela kwa muda wa usiopungua miaka miwili au adhabu zote kwa pamoja”
Kanuni ya 12 ya Kanuni za Mawasiliano

za mwaka 2005 za Tanzania (Kulinda Wateja) inasema:-
“Mtoa huduma za Mawasiliano haruhusiwa kuingilia kati, kusikiliza au kutoa taarifa zozote za mazungumzo ya mteja yeyote yaliyopitia kwenye mtandao wa mtoa huduma, isipokuwa kwa ruhusa kulingana na mahitaji maalumu kwa mujibu wa sheria zilizopo”
Kutolewa kwa taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa simu za mkononi ni lazima kunafanywa na mtu mwenye ujuzi na uelewa wa jinsi ya kupata taarifa hizo na wenye ruhusa ya kufanya hivyo katika mtandao wa Kampuni husika ya kutoa huduma ya mawasiliano; ama peke yake au kwa kushirikiana na wenzake kwa kuingia kwenye mtandao kwa makusudi kwa lengo la kuingilia mawasiliano binafsi ya watu, ambayo ni uvunjaji na kinyume na matakwa ya kifungu cha 123 cha Sheria Na. 3 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.
Mamlaka ya Mawasiliano inayakumbusha Makampuni ya simu kuweka uzuizi na kuhakikisha siri za mazungumzo binafsi ya wateja zinahifadhiwa na hazitolewi kwa yeyote isipokuwa kwa mujibu wa sheria na; kuhakikisha yanafanya uchunguzi kugundua walioiningilia mazungumzo binafsi ya wateja.
Wananchi wanapewa tahadhari kuhusu kutafuta au kutaka kupata taarifa za mawasiliano ya siri kutoka kwa watoa huduma na kuzitumia taarifa hizo binafsi za mawasiliano pasipo kufuata utaratibu ulioruhusiwa kisheria.
Kwa taarifa ambazo zimechapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Mamlaka ya Mawasiliano inafanya uchunguzi wa uvunjwaji huo wa sheria kwa kutoa taarifa binafsi za wateja kinyume na sheria. Baada ya kuwabaini wahusika, Mamlaka itachukua hatua za sheria kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria hiyo.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
22 Desemba 2010

Michu, waambae hao wapuuzi wafuatilie waliochakachua simu zetu kwa kusambaza meseji za chuki wakati wa kampeni. Tanzania ni yetu sote siyo MCC tu ala!
ReplyDeleteKama yale mazungumzo ya Mh. Zitto Kabwe na Mr. Zoka wa usalama wa Taifa nayo ni kuvunja sheria hii??
ReplyDeleteJe hawa jamaa waliomnukuu Dk. Hosea nao wamevunja sheria hiyo??
Ankal Michu.....nionee huruma unirushie haya maswali yangu maana ni mara chache sana huwa unanikumbuka, mimi sichafui hali ya hewa Ankal.
Haya ndiyo matatizo ya Marekani kumbana WikiLeaks! Sasa tutakuwa hatupati tena 'siri. za mikataba mibovu na ufisadi serikalini! Damn!
ReplyDeletewa kondya sana!
ReplyDeleteNina support government hapa. Hii tabia ya kuingilia mawasiliano ya watu ni ya kishenzi. Hii sheria inanikumbusha ile iliyoko U.S. inayoitwa "privacy act". Ninyi wafanyakazi wa makampuni ya simu acheni tabia chafu ya kuanika habari za watu nje nje. Sasa mtakwenda jela.
ReplyDeleteTz people we are stil living under the black curtain, dont just look at the end of the river but find out the source, people are tired with unlawful system now what they are looking is accountability of people with the remote control, thnk why just no of prominent figure? Why not normal mwananch? The way of evil shal never prosper. TCRA have to take responsibility to reveal traitors of our prosperity plans.
ReplyDeletehii sheria inalinda maovu.
ReplyDeleteSheria Inasemaje pale mazungumzo yanahusu uvunjaji wa sheria kama kupanga wizi, mauaji, uhujumu uchumi, ujangili, uhaini nk. Nini sheria kuhusu Whistle blowers!!!. mkurugenzi tufafanulie pia
ReplyDeleteHii inamaanisha kwamba kitendo cha gazeti moja la kila wiki kutoa taarifa ya mawasiliano ya Mh. ZK na hao wadau wake ni kinyume cha sheria.
ReplyDeleteMdau aliyetoa zile namba anahitaji kuadhibiwa.
Ikiwa kutakuwa na special case kama ya kupanga ujambazi au ugaidi basi kwa kawaida kunakuwa na kibali maalumu kinachotolewa ili kushughulikia hilo jambo.
ReplyDeleteSiku moja tutakuja ona mawasiliano baina ya mama na baba yamewekwa hadharani kama hakuna control yo yote ya mawasiliano.