Uongozi wa Tamasha la Filamu la Nchi za Majahazi (ZIFF) umepanga kufanya tamasha dogo la siku tatu ili kutoa muamko kwa tamasha kubwa la ZIFF la Julai mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (jana) jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa ZIFF Bw.Martin Mhando amesema, tamasha hilo litaanza tarehe 31 Disemba mwaka huu hadi Januari 2 mwakani Ngome Kongwe Zanzibar. Ameongeza kuwa tamasha hilo litajumuisha filamu za kitanzania peke.

“ Tunafanya hivyo tukiamini kuwa tamasha litatoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii.”alisema Bw.Mhando.
Pia mkurugenzi huyo amesema, filamu zinaweza kuiuza nchi pale sehemu au maeneo yake yanapotumika kutengenezea filamu pamoja na miradi mbalimbali.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema tamasha hilo litaonyesha filamu sita za kitanzania na filamu mbili bora kati ya hizo zitaenda kuonyeshwa katika tamasha kubwa la filamu Afrika_FESPACO huko Burkina Faso.



Katika kupendezesha tamasha Mkurugenzi huyo amesema kutakuwa na makundi ya muziki kama THT,pamoja na wanamuziki Mwasiti,Marlaw,Barinaba,wengine watakakuwepo ni Pipi,Amin na Mataluma.

Vilevile Tamasha hilo kushirikiana na Deustche Welle imepanga kuendesha workshop juu ya utengenezaji filamu ili kuboresha filamu na kukuza tasnia ya Filamu Tanzania .

Bw Mhando amesema Tanzania imefanikiwa kutoa filamu yenye jina la “Nani”ambayo imefanikiwa kuingia katika filamu za kimataifa huko Postdam Ujerumani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tanzania kifilamu tunaweza kufanya bora ,punde tutakapo acha kutunga filamu kama za kizamani za kinaigeria,hizo movie zote za kitanzania ukiangalia unajua mwisho wake baada ya dakika 10 tuu.tunatakiwa upeo wetu wa utunzi uamke na maedita wawe wamekwenda shule pia na kujua vipande gani muhimu na vipi vikatwe.tanzania tunamandhali nzuri nyingi tuu za kuigizia filamu, ila watunzi awajayashitukia bado.

    matamasha kama haya ni mwamko mzuri kwa film industries i guess.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...