Wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya Ugannda 'The Craners' kwa mikwaju ya penati 5-4 na kupata tiketi ya kuingia fainali ya mashindano ya Tusker Challange Cup katika mchezo uliopiga jioni ya leo ndani ya Uwanja wa Taifa,jijini Dar.
Kocha wa Makipa wa Kilimanjaro Stars,Juma Pondamali akiyarudi magoma na Ramadhan Shamte mara baada ya ushindi mnono wa timu hiyo dhidi ya Uganda.kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itamenyana na Ivory Coast katika fainali ya mashindano ya Tusker Challange Cup hapo jumapili ya Desemba 12.Waliofunga upande wa Uganda ni Issack Isinde, Dan Walusimbi, Emmanuel Okwi na Andy Mwesigwa
Kilimanjaro Stars waliofunga ni Nsajigwa Shadrack, Stephano Mwasika, Shaaban Nditi, Salum Machaku na Erasto Nyoni.
kwa picha zaidi
BOFYA HAPA
kwa picha zaidi
BOFYA HAPA



ANGEKUWA YULE MBRAZIL ASINGEMUWEKA KASEJA KWA KUDAI KUWA NI MFUPI.ILA JAMANI YULE MBRAZIL ALIKUWA NA NIA NZURI KWELI??
ReplyDeletekaka misoup poa sana kwa up to date zako afadhali kaka tz oyeeeeeeeeee
ReplyDeleteMAXIMO huko aliko nafikiri anapata habari hizi. MAXIMO hakuwa kocha alikuwa mbabaishaji tu anawaacha wachezaji wa maana na kuwaweka wachezaji wake wa mchangani. Kosa la MAXIMO ni kumuacha Kaseja, kipa ndio ngao ya timu ukiwa na kipa mbovu atafungwa na kocha utaoneka huna maana.
ReplyDeleteTunaomba mwenye data atuletee waliotufungia penalti zetu. Pia tukipata kikosi kilichokipiga itakuwa bora kwa sisi tunaofuatilia kutoka Ughaibuni. Wasiwasi wangu ni kuwa kuna jamaa wa China utamsikia akisema kwa nini tunauliza. Amekuwa kama bidhaa na madawa ya Kichina
ReplyDeleteJamani Kama Mmeona Rais Kikwete kama yupo Mpirani Tunashindwa Mfano Wa Karibu Mechi ya Kwanza
ReplyDeleteSasa Ndugu Michuzi Tafadhani Umshawishi Rais Kikwete kuangalia Fainali Kwenye TV na Tutashinda Naomba Sana kombe lisiende IVORY COAST.
Jamani Kama Mmeona Rais Kikwete kama yupo Mpirani Tunashindwa Mfano Wa Karibu Mechi ya Kwanza
ReplyDeleteSasa Ndugu Michuzi Tafadhani Umshawishi Rais Kikwete kuangalia Fainali Kwenye TV na Tutashinda Naomba Sana kombe lisiende IVORY COAST.
KenRon - New York
JK alikwenda kwenye mechi na Ivory Coast Januari 2010 tukafungwa. Akaenda tena na Brazil Juni 2010, tukafungwa, na juzi juzi kwenye mechi na Moroko tukafungwa tena; na hata kwenye mechi ya ufunguzi na Zambia tulilala pia.
ReplyDeleteJamani, kila mtu afanye analoweza ili huyu kiongozi asije uwanjani Jumapili. Kombe ni letu hilo ila lazima tukubali rais wetu huyu ni kama Mzee Ruksa, akija tu mnalala.
Michuzi weka hii, Tanzania yetu sote.
Kikwete alikuwepo uwanjani Taifa Stars ilipopambana na Burkina Faso tukampiga mtu bao. Labda kama ni gundu la Kilimanjaro Stars peke yake.
ReplyDeleteAcheni hisia zenu za kishetani,Bukinafaso na Stars ya Maximo alikuwepo uwanjani na Bukinaa wakalala si ndie alikuwa uwanjani??? mm sioanishi kufungwa na kuwepo JK uwanjani, ni kama wanaosema turoge ili tushinde,bila mazoezi hata ukiroga ni bure tuu utabugizwa mia na mganga utamuona mbaya
ReplyDelete