Muhimbili Wanahitaji
Fluoroscopy X-Ray Machine
Na Da'Chemi Che-Mponda
Wadau, nimehangaika na baba yangu hapa Muhimbili siku kadhaa sasa ili afanyiwe Cystourethrography. Bado hajafanyikiwa, mashine inaharibika kila saa. Kuna backlog ya wagonjwa wanaohitaji kufayiwa x-ray na hiyo mashine lakini haijawezekana.
Jana ilikuwa sikukuu hivyo walikuwa wamefunga. Ile juzi tulimtoa baba wodini Mwaisela na kumpeleka kwenye X-ray. Kakaa masaa kadhaa ndo wakasema mashine imeharibika na fundi anitengeneza.
Alitokea Acting Head wa Idara, Dr. Flora Lwakatare, alisema kuwa wana mashine mbili za fluoroscopy. Moja ndo mbovu kabisa na nyingine ndo hiyo inayoleta matatizo mara kwa mara. Alisema wametarifu Waziri kuhusu tatizo lao lakini bado hawajapata mashine mpya.
Haya leo, tumemtoa baba wodini kumpeleka huko kwenye x-ray. Mashine ikaleta matatizo. hivi sasa wanasema fundi anakuja kutengeneza. Isipowekezekana leo basi mapaka juamatatu. Tunaomba mungu kuwa watafanikwa kutengeneza mshine na itaweza kufanya kazi.
Na sasa ni zaidi ya saa moja imepita, babu ambaye alitolewa wodi nyingine kwa ajili ya vipimo alizimia na kuanguka hadi kwenye sakafu! Nesi aliyemsindikiza baba yangu kamhudumia yule mzee mara moja. Wamerudisha wodini. Inasikitisha kweli kuona wagonjwa wamelundikana pale x-ray.
Kwa kweli huduma hapa Muhimbili umekuwa mzuri, ila ndo tumekwama kwenye hiyo x-ray. Je, serikali ina mpango gani wa kuleta mashine hiyo? Maana wagonjwa wanateseka.


Pole Dada Chemi. Hiyo ndiyo Bongo. Wataalamu wengi watakuwa wamekimbilia Bungeni. Pia, kama huduma hizo zinapatikana kwenye hospitali binafsi, Khabari ndo hiyo Dada Chemi!
ReplyDeletePole sana,mpelekemzee India apate matibabu ya hakika.Thereare daily flights Qatar, Emirates to india.8hrs only.My prayers for mzee for fast recovery.
ReplyDeleteOld and sick patients MUST be provided with wheelchair within the hospital.Why should a patient get injured in hospital wards and that too at NATIONAL HOSPITAL?Questions ,Questions and more but no answers.Pole to mzee
ReplyDeleteHalafu kinachosikitisha ni ukweli kwamba bei ya hiyo x-ray machine ni ndogo kuliko bei ya Landcruiser VX moja! Waheshimiwa hawaoni umuhimu kununua hiyo mashine kwa sababu wao wakiumwa wanaenda south afrika, India au Ulaya kutibiwa ..... kwa pesa ya serikali .... so sad.
ReplyDeleteDada yangu, hapa sisi hatupendi kazi.We work from Monday to Friday and not more then 4hours a day.So we have 20hrs /week.The fundi can not work on weekends even in emergency.Here nobody is accountable to anybody.Most of the time govt. workers are in seminars and endless meetings.Feel so sorry for your Dad.
ReplyDeleteDada Chemi, pole sana na matatizo. Nadhani tunaweza kuanza kwenye hiyo machine kwa msaada. Tafadhali ukirudi usa tuwasiliane, kwani tunaweza kusaidia.
ReplyDeleteMdau
sygonlove@yahoo.com
POLE DA CHEMI, MUNGU AMPE MZEE NGUVU APONE HARAKA.
ReplyDeleteKWA NINI MICHUZI USIANZISHE HARAMBEE KUPITIA BLOG YAKO ILI WATANZANIA POPOTE WALIPO DUNIANI WACHANGIE KUNUNULIWA KWA HIYO X-RAY MACHINE?
HAYA MAMBO YA KUISUBIRI SERIKALI ITIMIZE WAJIBU WAKE WAKATI WATU WANAZIDI KUTESEKA MUHIMBILI NI UJINGA.
SOAMES PHARES,
READING, UK.
Inasikitisha sana lakini ukweli ndio huo. Watu wanakufa Bongo kwa magonjwa yanayoweza kuzuilika. Weekends na holidays ati kunafungwa na hawafanyi kazi. Kwa lipi waliloridhika? nchi zilizoendelea hakuna kufungwa kazi ni 24/7 na usipofanya vizuri anapewa mwingine. Nchi yetu twabebana kazi kapewa mtoto wa mjomba utamfukuza vipi?
ReplyDeleteIt is sad lakini kama alivyosema huyo hapo juu ingekua gari, na semina zisizo na mwisho basi lingetafutwa haraka haraka...Na wakiumwa wao wamepandishwa pipa na wasio na hela ndio unakufa kabla ya siku yako...
Tuone awamu hii itakaa vipi.
ReplyDelete@sygonlove mambo ya misaada mi siyahusudu kabisa kwa vile wakipelekewa hawavithamini wala kuvitunza. Watoe hela ndio wataona uchungu wa jasho lao na watavitunza. Kila siku ni misaada mingapi inakwenda lakini within a year hakuna kinachofanya kazi. Vitu havifanyiwi service wala nini mapaka kiharibike ndio ndio wanafix au ndio kupitisha bakuli lingine.
Miaka 49 bado mtoto anatambaa tu, lini atakua na kujifunza kujitegemea? I hate this baby
Mimi ningekupa ushauri wa bure yaani ni bora ukamuone waziri wa afya huyo ndo atakuwa na majibu yote maana si wewe tu hata mimi nilikuwa na Mgonjwa wangu hapo alihitaji Dialysis machine ili aweze kutibiwa figo ikashindikana mpaka akafariki na wengi wanafariki kwa kuwa wana matatizo ya figo na dyalisys machine hakuna yaani machine ya kuchuja uchafu na kutoa ili kusaidia figo ziweze kufanya kazi.
ReplyDeleteNa cha kushangaza hiyo machine haicost hata millioni 40 ni chini ya hapo ukipata used lakini inaonekana serikali imelala na pesa za misaada zipo kibao zinapotea tu hivi hivi.
Ni hatari sana kwa kweli nchi yetu tunaishi ki Mungu Mungu kazi zao hata hao Voda com au makampuni mengine kila siku nawaona wanatoa misaada hivi wanashindwa kufuatilia vitu muhimu kama hivi ni maskitiko makubwa!
MIMI NAFIKIRI BUNGE LIJALO WASITOE KABISA HIZO MILION 80 NA LANDCRUISER KWA WABUNGE.INSTEAD WATUMIE HIYO HELA KUWEZA KUSAIDIA WATU AMBAO THEY REALLY NEED HELP. ANGALIA WAZEE WETU WANAVYOPATA MATATIZO HOSPITALINI NA HOW COME HATA WHEELCHAIR ZINATUSHINDA JAMANI.DUH HII NI NOMA KABISA.POLE SANA MZEE CHANGES IS COMING IN A MIN.JAMANI KAMA MNAWEZA KUPATA MORE INOFORMATION YA HIYO MACHINE TUIANGALIE INA COST BEI GANI NA WAYI HATUNA 20 KATIKA HOSPITALI KAMA YA MUHIMBILI
ReplyDeletehiyo ndio bongo darisalama, mambo tambarale!!!!!
ReplyDeletePole dada, please take mzee to Nairobi Agakhan Hospital.You will be amazed what they can do.
ReplyDeleteMbona huko ndiko JK anakoshinda kusalimia wagonjwa kisha mambo ndio hovyo hivyo pole sana dada.
ReplyDeleteSio kwamba mashine au mafundi hakuna. Secta ya afya iliruhusiwa kuendeshwa kibiashara na watu binasfi. Mnategemea katika hali hiyo hospitali za serikali zitakuwa na ufanisi? Unategemea kifaa kifanye kazi muhimbili, au wenye hospitali binafsi watakula wapi? Fikirieni wenyewe kwa makini, kwa nini vifaa vinakaa siku chache tu na kufa?
ReplyDeleteChemi dada, at the end you asked when will the govt. get anew machine.
ReplyDeleteThe answer is simple, we shall call a seminar at some nice resort away from Dar. and invite non medical people to advise us on the issue. After that there will be follow up meetings and pretent to be real busy like nobody. The allowances will be hefty.
When we finally order the machine it be delivered after two years. After unpacking lo and behold the machine is not the one we ordered.god bless and protect us all.
MISWAADA KIBAOOO BUNGENI..JAMBO DOGO SANA KWA WIZARA LAKINI ANAGLIA FEDHEHA NYINGI ZINATUKUTA. NASHINDWA SANA KUELEWA NI KITU GANI KINAWASHINDA KUTATUA MAMBO KAMA HAYA. SIONI KAMA FEDHA INA CONCERN HAPA. IDARA YEYOTE IKIWA NA POOR MANAGEMENT MATOKEO YAKE NDIO HAYA. HII YOTE NI KWASABABU WAKUBWA HAWAPATIKANI NA HAYA MATATIZO. LAKINI MUNGU ATATUONYESHEA UBAYA WAO HAPA HAPA DUNIAN.
ReplyDeletePELEKA A WHEELCHAIR ZA MISAADA UWONE KAM HUTOZIKUTA ZINAPIGWA BEI MITAANI. NA USISHANGAE ZIKAGEUZWA BAJAJI HOSPITALINI.
ReplyDeleteWAMEKAZANIA KUJAZA MATUMBO TUU.
Mr. Phrase, this is a national hospital...the gov't is supposed to take care of the issue, but sadly, they've different priorities and there is no accountability.
ReplyDeleteI feel sorry for your dad...chemi, but that's our bongo. Now imagine people who can't afford to travel to India or south Africa for better treatment...it's a very sad situation. Health care in Tanzania is bad.
pole dada and hope your dad and others in need will be treated soon. here is the link though are Chinese products but are very cheap in comparison to importance of our health and wealth http://www.alibaba.com/trade/search?SearchText=flouroscopy+machine+price&CatId=0&IndexArea=product_en&sq=y&fsb=y&tracelog=seo_product_direct_0820
ReplyDeleteHii ni kwa woote mnaosema "Bongo Nyu Yoku". Mambo kama haya ndiyo yanatufanya kuihama nchi yetu kwa ujumla....tutaja kutembea tu.
ReplyDeleteWenye moyo wa uzalendo kwenda kujaribu kurekebisha upuuzi wa serikali zetu Mola awazidishiye. Lakini please....usituambiye Bongo New York kwa sababu tu ya "Vikwangua Anga" vipya kila siku....that doesn't mean anything. Bora tuishi kwenye nyumba za udongo lakini tupate huduma muhimu zilizo bora.
....kwangu mimi na wanangu Kasongo na Kalunde, bora tubaki ughaibuni tu.
Da Chemi tunaungana nawe kumuombea dua baba yako apone haraka. Amina!
Asanteni.