Jumuiya ya waliosoma Shule ya Msingi Mlimani (UDSM) inapenda kuwapa taarifa Wana-Mlimani wote kuwa tumeanzisha Blog yetu watotowamlimani.blogspot.com kwa ajili ya kupashana habari mbalimbali kama vile msiba, Harusi, ubatizo wa mtoto, kipaimara, kikao cha harusi etc.

Karibuni mtembelee na kutuma taarifa zozote au picha kupitia anuani hii watotowamlimani@gmail.com ili tuziweke kwenye blog kwa faida ya Wana_Mlimani wote.

Mlimani Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Nafikiri hii blog itakuwa ya wakristo watupu!!

    ReplyDelete
  2. Wazo zuri sana. Ushauri: mnapobandika picha basi weka na mwaka ambao mhusika alihitimu. Hilo litasaidia kuonesha mlolongo wa vizazi (generations)kama vile wa miaka ya 80, 90, 00 , nk.

    ReplyDelete
  3. we anon acha fikra potofu, umeona kwenye tangazo hapo juu mtu yeyote amemention chochote kuhusu DINI? kama huna la kuandika, kaa kimya..
    idea nzuri sana ya hiyo blog ni njia nzuri ya kuwakutanisha wana Mlimani nakujua nini kinachoendelea katika life zao, mfano graduation,msiba,harusi etc
    Hongera wahusika wote.
    Hongera pia sana kwa reunion party mliyofanya..

    ReplyDelete
  4. Sihawahi kuona watu wenye mawazo finyu duniani namna hii. Kwa kuwa wameandika kipaimara, ubatizo na harusi basi mtu anakurupuka na kuandika 'Nafikiri hii blog itakuwa ya Wakristo tupu'. Ama kweli uliyeandika hilo umefilisika kimawazo.Kwani hujaona wamesema kuwa wataipasha jamii habari mbalimbali; ZIKIWEMO...... Kuwa kimawozo wewe anonymous wa 02:12:00. Pole,una akili FINYU mno
    Mpenda maendeleo

    ReplyDelete
  5. Ni jambo zuri sana kukumbukana na kuwa pamoja kama hao wa mlimani. natafuta kujua kama kuna jumiya ya waliosoma 'Shycom". Jamani nijulisheni, kuna kipindi nilisikia Dar ipo lakini sijapata contacts zake. Sisi tulio bara tumebaki nyuma kidogo, tutajiunga na wa Dar kama umoja huo unaruhusu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...