Heshima kwenu wakuu,
Tafadhali naomba kupitia blog zenu tuwasaidie watanzania wenzetu ambao hawajui kuwa si ruhusa kiusalama kufanya shughuli yoyote ile chini ya Tanesco Transmission lines.
Nimeambatanisha picha hii ambayo nimeipiga maeneo ya Tabata (Kinyerezi) ambako kuna makazi mengi mapya lakini uvunjaji mkubwa wa sheria hizi umeanza kufanyika. Aidha mamlaka husika, Tanesco ikiwa mojawapo hazijawaelimisha wananchi juu ya hili.
Katika picha hii wananchi hawa wanaendelea kujenga majengo ya biashara na makazi chini ya HT Line.Miaka 5 au zaidi baadaye Tanesco au Tanrods itawabomolea majengo yao.Hii ni hatari kwa uchumi wa nchi kwa kuwa ni pesa zinatumika hapa.
Aidha Tanesco wanatakiwa kufanya utaratibu wa kuweka alama za kuwataarifu wananchi kutoendelea kujenga.Watu wengi wanapoteza rasilimali zao kutokana na Mamlaka husika hazitoi elimu ya kutosha kwa wananchi na pia zimekuwa kimya uvunjaji wa taratibu.
Asante

Wewe mtoa mada unaonekana uko bias. Ni kweli kabisa kwamba hairuhusiwi kujenga chini ya High Tension, kama ambavyo hairuhusiwi kupitisha high tension juu ya nyumba za watu. Inabidi ujue nani alitangulia badala ya kuanza kulaumu watu, kumbe pengine TANESCO ndio wamewaingilia. Kwa hiyo, aliyemuingilia mwingine ndo amefanya makosa
ReplyDeleteKijana weee hao TANESCO hata kama maeneo yako planned lakini nguzo ikiwa upande na waya zinaning'inia wao hawajali mpaka itokee ajali.
ReplyDeleteMimi naishi Mbezi beach ni planned area nimewaita weeeeeeee leo sijui ya ngapi lakini hawajaja. Wanasubiri ajali ndiyo wakimbizane?
WABONGO BWANA, MNAAMBIWA KITU CHA MAANA, MNAJIFANYA WAJUAJI....HAYA SHAURI YENU, ILA TU MJUE KWAMBA UKIJENGA CHINI YA NYAYA ZA TANESCO, NYUMBA ZENU ZITABOMOLEWA....MTOA MADA ANATAADHALISHA TU, HAYUKO BIAS WALA NINI.
ReplyDeleteHii inaonyesha wazi jinsi halmashauri walivyolala, wanakunywa chai na chapati nene ofisini, hawakagui maeneo kutazama vitu kama hivi visitokee, mwokozi ni Mama Tibaijuka..ngoja tu!
ReplyDeleteWatanzania tunatakiwa tuanze kubadilika sasa.
ReplyDeleteMdau huyu ametoa wazo la busara sana ili kuokoa pesa nyingi za watanzania wengi wasiojua taratibu na sheria hizi.
Aidha mdau ameainisha wazi wajibu wa mamlaka husika kuzuia uvunjaji huu wa sheria ambao huko mbeleni utaigharimu serikali au wakazi husika.
Tanesco au Manispaa ya Ilala walitakiwa wawe wameona hili na kuweka alama za tahadhari/ taarifa ili wananchi wasiendelee kujenga chini ya High Tension.
Ni aibu kubwa kuona kuwa mamlaka hazitachukua hatua huku zikiwa na taarifa kamili (location & details) mpaka ajali itokee baadaye.
Mtu yeyote mwenye akili timamu akipewa taarifa na kuona alama nyekundu za kuzuia ujenzi kwenye eneo lake ni wazi hataendelea kujenga ili kuepuka hasara zaidi mpaka mgogoro utakapotatuliwa.
Kwa kweli mdau amenisaidia, nilitaka kuuziwa kiwanja kama hiki chini ya High Tension jana tu kwa bei nzuri tu.