Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, Mb. akihutubia siku ya kilele cha maadhimisho ya Haki za Binadamu katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam jana ambapo alikemea vikali ubaguzi wa dini katika jamii ya Kitanzania. Aidha alitoa mwito kwa wabunge wote kupatiwa elimu ya haki za binadamu kwani hiyo ndiyo shughuli yao ya kwanza kama watetezi wa wananchi.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Jaji mstaafu Ramadhni Maneto (kushoto) akishauriana jambo na Mhe. Spika Anne Makinda. Kulia ni mtaalam na mchambuzi wa mifumo ya Computer wa Tume hiyo.
Spika Makinda akibofya kitufe cha kuashiria uzinduzi wa mfumo wa kisasa wa mawasiliano wa kukusanya, kuchambua na kushughulikia malalamiko ya wananchi pale haki zao zinapokuwa zimeng’ung’unywa kwa namna moja au nyingine.
Spika Makinda akimkabidhi mtoto Miriam Edward Thomas (12) zawadi baada ya kutumbuiza katika umati mkubwa kwa wimbo wake wa Haki za Binadamu. Miriam ni mlemavu wa macho tangu kuzaliwa lakini kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa na wanaharakati wa Haki za Binadamu amapata matibabu katika Hospitali ya CCBRT na sasa anao uoni hafifu ambao unamsaidia kujimudu katika mambo mablimbali. Miriam aliyeandamana na Baba yake mzazi alikuwa ni kivutio cha kipekee katika maadhimisho hayo.
Uongozi wa Tume ya Haki za Binadamu pamoja na wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaosimamia harakati za haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja na mtoto Miriam na Spika Makinda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inaonyesha dhahiri kwamba Miriam anayo talent kubwa lakini Mwenyezi Mungu amemjaalia kuwa mlemavu wa macho.

    Hongereni kitengo cha Haki za Binaadamu kwa kumsaidia binti huyu na Mungu awape nguvu za ziada kusaidia wengine kama yeye.

    ReplyDelete
  2. Ana miaka 12 kweli au kakosea mwandishi. Mbona anaoneka mdogo sana?

    Whatever the case Mwenyenzi Mungu atamjalia atafika mbali tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...