Maafisa Habari Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa pembeni ya Mto Kiwira wilayani Rungwe kwa ajili ya kujionea maajabu ya Daraja la Mungu ambao maji ya mto huo yanapita katikkati yake. Maafisa hao walifanya ziara ya mafunzo kwa lengo la kujifunza na kujionea kivutio hicho kinavyoweza kusaidia kuongeza pato la Taifa.
Baadhi ya Watendaji Waaandamizi kutoka Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo na Maafisa Habari Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika Maporomoko ya Malasusa kwenye Mto Kiwira juzi wilayani Rungwe . Ziara hiyo ya mafunzo ilikuwa ni sehemu ya kikao kazi chao kilichofunguliwa juzi na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Pili Rajab akielezea kufurahishwa kwake na maajabu ya baada ya kuona Ziwa Ngozi(nyuma yake) lilipo katikati milima na kulifanya lifanane na Ngorongoro Crater. Mfanyakazi huyo na Maafisa Habari wa Serikali walikwenda Wilayani Rungwe juzi kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya vivutio mbalimbali vilivyopo hapo.
Baadhi ya Maafisa Habari Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa picha ya pamoja mara baada ya kufikia kilele cha Mlima Uporoto ambao unazunguka Ziwa Ngozi. Ziara hiyo ya mafunzo ilifanyika juzi kwa lengo la maafisa hao kwenda kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vya wilayani humo kwa ajili ya kuvitangaza ili visaidie kuongeza pato la Taifa.
Daraja la Mungu ambalo mto Kiwira unapita
katikati yake katika wilaya ya Rungwe.

Sehemu la Daraja la Mungu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Jamani watu tuwe tunafikiria kabla ya kuandika. Aliyepost hii habari anasema "Daraja la Mungu ambapo maji ya mto huo yanapita chini". Naomba ndugu wa blog mnisaidie, kwani mimi sijawahi kuona daraja ambalo maji yanapita juu yake.

    ReplyDelete
  2. lipo daraja ambalo maji yapo juu,nadhani lipo Ujerumani

    ReplyDelete
  3. You never know may be.

    ReplyDelete
  4. daraja ambalo maji yanapita juu lipo hapa udachini nchini uholanzi daraja lipo chini ya bahari watu wanapita humo na magari na juu meli zinaendelea na safari kama kawaida.

    mdau wa mahakama kuu ya dunia.

    ReplyDelete
  5. mm nadhani limeitwa daraja la mungu in the sense kwamba halikujengwa na mtu. naona kama ni mawe tu naturally yametokea kuwa juu na mto kupita katikati yake!!!

    ReplyDelete
  6. Mother nature in effect.The river cultivate the rock to form that bridge.In other word you can say it's just erosion.The soft(bottom) part of the rock was eroded away by the river.

    ReplyDelete
  7. MADARAJA YA MAJI KUPITA JUU YAPO na yanaitwa aqueduct. Anony wa juu anashangangaa wakati hivi vitu vipo , uwe unafanya utafiti kabla ya kuongea. Hebu bandika huyo link uone; http://www.truegiantsnorthwales.co.uk/aqueduct/

    ReplyDelete
  8. Wandugu lazima tumshukuru michuzi kwa hizi picha.Si wengi wamefika hapo, mimi nimefika na nimeona maajabu hayo.
    Sehemu hiyo ya mto ina maajabu mengi sana.Juu(ustream) ya daraja la Mungu kuna maanguko yaendayo kasi sana kiasi cha kutendeneza "the bernoulli effect".
    Kila aliyejaribu kuvuka hapo alivutwa na upepo na kutumbukia mtoni.
    Juu zaidi ya mto huo kuna "kijungu" au birika ambamo mto mto unaingia na atelezaye kuingia humo hatoki mpaka "wazee" wa hapo wawe consulted.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...