NA MWANDISHI WETU, MUSOMA
MCHAKATO wa kumsaka Kisura wa Tanzania 2010/11, umemalizika mkoani Mara mwishoni
juzi ambapo wasichana wawili walifanikiwa kupita katika mchujo uliofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Mativila, mjini hapa, hiyo ikiwa ni awamu ya kwanza ya mchakato huo.
Akizungumza mjini hapa jana, Mshauri wa Kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency, Agnes kiondo, aliwataja wasichana hao kuwa ni Lilian Busa na Gaudensia Joseph, ambao walikidhi vigezo vinavyotakiwa katika mashindano yao.
“Wasichana waliojitokeza walikuwa ni wengi, lakini hao wawili ndio waliokidhi vigezo…lakini hata hivyo tumefarijika na jinsi zoezi lote lilivyokuwa,” alisema Kiondo. Kiondo alivitaja vigezo vinavyotakiwa katika shindano hilo kuwa ni urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27) bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.
Alisema kuwa baada ya kufanya mchujo huo mkoani hapa, mchakato huo ulihamia mkoani Kagera jana na leo msafara wa timu ya TBA utaelekea mkoani Shinyanga na kesho Tabora kwa ajili ya mchakato huo, kabla ya kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
“Baada ya Dar es Salaam, tutahamia kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Arusha na Karatu, na baadaye kwenda Dodoma, na kumalizia mchakato huo katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma,” alisema Kiondo.
Kiondo alisema kuwa fainali za mashindano hayo ambayo taji lake linashikiliwa na Diana Ibrahim kutoka Mara, inatarajiwa kuwa Machi mwakani 2011 katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.
Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, kuwa ni Family Health International (FHI), TBC1, Kiromo View Resort Hotel, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...