Moshi ni kati ya miji inayoaminika kuwa na wageni wengi hasa kipindi cha siku kuu za Mwaka mpya, lakini hali huwa tofauti siku ya Krisimasi. Wageni na wenyeji wengi ambao husababisha mji kuwa na pilikapilika huishia kwenda milimani 'Kuhesabiwa' na kuacha mji kutokuwa na watu kama wapo basi ni mmoja mmoja tu kama taswira hizi za leo zinavyoonesha. Juu ni kwenye mzunguko wa makutano ya barabara za Boma,Double road, na Railway road
Mji mtupuuu..
Magari hamna kabisa leo
Noeli day Moshi town
Barabara ya Boma road.
Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Asante saana mdau uliyetuma hizi taswiraz kweli kwetu pasafi ajabu pamoja na pilika zoote za sikukuuu mji unang'aa kwa usafi hadi raha na una vutia saaana.... hapo watu wamesepa wamekwenda mlimani kuhesabiwa si utani christmas na wanafamilia inanoga kweli kweli, heri ya christmas wachaga woote na wadau wote wa misupuz blog
    mdau manka ottawa

    ReplyDelete
  2. kaka mithupu pole na kazi na nakutakia christmas njema, ombi lang ni kukuomba wewe pamoja na wadau wote wa blog ya jamii kama mnaweza kupost picha mbalimbali za tanzania katika skyscrapercity, pia kuna thread la dar arusha mwanza, dodoma na zanzibar, katika utalii pia unaweza kutuhabarisha na chochote kinachoendelea huko kwetu, picha za utalii please dumbukiza humu http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=803392
    na vikanguaanga vya dar dumbukiza humu http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=430948
    Tanzania Infrastructures development & Discussion dumbukiza hapa http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=1139953, pia nilikua nauliza hivi libeneke la taswira limekufa? au kunani? kaka michuzi pia nilikua nakuomba kama unaweza kutupatia picha ya dar usiku ukiwa jengo la mwalimu pale ilala kuelekea CBD (MAENEO YA POSTA), karibuni skyscrapercity tanzania

    ReplyDelete
  3. Home sweet home...duh...thanks Michuzi....

    ReplyDelete
  4. Duu, Yaani hawa wachagga wana hama mjini kabisaa... wote wana kimbilia mlimani!! ndio maana hakuna snow mlimani kilimanjaro kwa sababu wana haribu mazigira. Ninge shauri serekali iwanyime wa chagga kutokwenda kwao kwa muda wa miaka miwili. Nadhani itasaidia saana kurudisha snow kwenye mlima na mazigira kurudia hali yake ya kawaida.

    ReplyDelete
  5. WACHAGA WAMEFULIA SIKUIZI!

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  6. HAHAHAH WACHAGA MICHUZI WAMEFULIA HAKO NDIO ONLY KASEHEMU KAZURI AMBAKO MENGI BONITE BOTTLE WALIKASPONSER KWENYE HICHO KIMNARA NENDA SEHEMU NYINGINE UTAKIMBIA BORA KIGOMA HIKI KIMKOA, KIMECHOKA KINOMA SASA HIVI SI UNAJUA TENA WACHAGA SASA HIVI HAWAPO WENGI KWENYE MADARAKA NA KUJIPENDELEA MIHELA YA SELIKALI KUJENGA KWAO TU, SIRIASI JAMANI HUU MKOA SASA HIVI HAUWEZI KUUFANANISHA HATA KIDOGO NA MBEYA, MWANZA BORA HATA ARUSHA, DODOMA NAYO DIO HIO INAZIDI KUWA BOMBA, MOSHI INAENDANA NA MTWARA MAY BE NA LINDI

    ReplyDelete
  7. Huyo mpiga picha amechukua kisehemu hicho kisichokuwa na watu. Watu wako kobao.

    Kwanza siku hizi si wachagga wengi tunaenda kuhesabiwa, labda familia ambazo bado zina upendo.

    Kama mchagga unajiweza kifedha , wakati wenzio kwenye familia hawana uwezo, haki ya nani mkikutatana huko mlimani hutarudi ulikotokea. Wachagga tunaogopa hilo. Siku hizi kuuana kwa ndumba ni nje nje. Mtacheka mtafurahi lakini rohoni mdogo wako, kaka au dada ana lake jambo.

    Hata mama mzazi anaweza kukufanya mbaya kama anaona labda baada ya kuoa matumizi kwake umepunguza.

    Hicho ndio tunaogopa huko uchaggani

    ReplyDelete
  8. I really admire the cleanliness in Moshi, i hope Madiwani wetu wanaiona hiyo na wataichukua kama changamoto katika miji mingine! BIG UP MOSHI PEOPLE.

    ReplyDelete
  9. Anaesema bora kigoma au lindi kuliko moshi ni muongo na ana wivu nani asiejua mji wote wa moshi ni msafi na watu hawatupi taka onyo, onyesha na kwenu basi tupaone ila ujue ukubali ukatae wachagga tupo juuuuu....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...