Ankal pole na kazi.
Ninaomba wanajamii wenzangu na wazazi wenzangu mnisaidie kufahamu hili: Ni kwamba ninatafuta shule ya awali (Primary school) kwa ajili ya mwanangu. Ninaomba sana kama kuna yeyote anaefahamu shule nzuri iliyopo maeneo ya kati ya Mbezi mwisho na Kibamba tafadhali nifahamisheni ikiwezekana na contacts za shule/walimu wahusika. Ningependa mtoto wangu asome maeneo ambayo ni jirani na nyumbani anakoishi ili kumpunguzia bugudha ya kusafiri kwa muda mrefu kwenda shuleni.
Mwenye ufahamu wowote kuhusu hili tafadhali niandikie kupitia anuani hii youjiebj@live.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. KELAND NURSERY & PRIMARY SCHOOL is the best in Dar.
    Contact 0713236938
    0784236938

    ReplyDelete
  2. Shule ya awali sio primary school mdau..... Primary school ni shule ya msingi.

    ReplyDelete
  3. Mimi Preference yangu Mwanangu asivuke Moro Road Kila siku. Hivyo wewe angalia upande ulipo. Kuna St Felician P & N School upande wa Kushoto, Pia kuna ile ya Kanisa Katoliki Mbezi Luis

    Vile vile kuna Nyingine nyingi upande wa Kulia towars Morogoro

    ReplyDelete
  4. kuna ya kanisa katoliki parokia mbezi luis, on your left to Moro, then pale mbezi mwisho kituoni kuna Barney iko km mt 200 toka pale kituo cha mbezi mwisho upande wa kulia moro road ukiwa unaelekea moro,
    pitie hizo

    ReplyDelete
  5. waepushe wanao na fataki kwa kuwasomesha karibu na Nyumbani, ni mwitikio bora wa kuiga,kuwazuia watoto na fataki.

    ReplyDelete
  6. Unaishi wapi?

    Shule za namna hiyo ziko nyingi nchini Tz labda, unatafuta ya aina ya apartheid )ya wazito)!

    ReplyDelete
  7. Kuna St. Felister iko makondeko upande wa kushoto kama unaelekea morogoro na kuna st ann iko mbezi mwisho upande wa kituo kwa ndani kidogo

    ReplyDelete
  8. We anonymous wa Thu Dec 02, 08:54:00 PM, soma maandiko ya mtoa hoja kwanza kabla hujaandika takataka zako! Umesikia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...