Nahodha wa Timu ya Taifa Tanzania Bara(Kili Stars) Shadrack Nsajigwa akimkabidhi JK Kombe la Chalenji Ikulu jijini Dar leo baada ya timu hiyo kuibuka Bingwa wa michuano ya Chalenji jana.Rais Kikwete aliialika timu hiyo Ikulu kuipongeza. Pembeni yake ni Mama Salma Kikwete na Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Dr.Emmanuel Nchimbi.
JK akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kizima cha Timu ya Kili Stars Ikulu jijini Dar es Salam leo mchana. Picha na Freddy Maro wa Ikulu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Umefika wakati wa wachezaji wetu wanapoenda ikulu,wavae mavazi rasmi kama suti kama wenzetu!!!Si vema waende shaghala baghala namna hiyo.Protocol lazima zizingatiwe.Sio lazima lakini siku mojamoja kama hiyo ni jambo zuri kwa ajili ya heshima

    ReplyDelete
  2. yaaani Taifa starz hongera sana ila sasa msije mkabweteka alafu masiha yakawa mabaya badae kwani mmh kichwa cha wendawazimu kimetibiwa na dawa ya kichina isije ikaja expire wakati wananchi ndio tunaanza kuwa na amani.

    ReplyDelete
  3. Nimefurahishwa na uzalendo wako JK, ila mi nalia na viongozi wetu.... Jamani mmeshindwa kuwanunulia vijana SUTI za kuendea ikulu, mambo gani haya ikulu na jeans!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. "Umefika wakati wa wachezaji wetu wanapoenda ikulu,wavae mavazi rasmi kama suti kama wenzetu!!!Si vema waende shaghala baghala namna hiyo.Protocol lazima zizingatiwe."

    Kwani ni dhambi kuvaa hivyo? kwani wameenda uchi wa mnyama!

    Eti, "kama wenzetu!!!" Akina nani hao? Hao ni wenzako kweli ama unawaiga tu?

    ReplyDelete
  5. Kwanini wanunuliwe? Kwani wanacheza mpira bure? Wakati umefika kwa Viongozi wa TFF kuwajibika.They should be told IKULU's dressing code.TFF bado haijajiandaa kimichezo kabisa, wanaingiza pesa nyingi lakini ni madudu matupu wanayofanya.Basi hata wangewavisha Jezi za chini pamoja na viatu.Tatizo la WANUKA VIKWAPA kununua viatu vizuri na Suit nzuri ni hanasa lakini pombe ni ufahari.Hata kwenye minuso hapo bongo ni balaa tupu. Watu wanachanga pesa nyingi lakini wanavyovaa kunatia aibu sana.Sisi wabeba mabox tuliliona ilo na ndio maana tunavaa vizuri sana.

    ReplyDelete
  6. TFF lazima mlaumiwe kwa majeans kutinga IKULU. Nyie kama wasimamizi wa Soka lazima muwajibike katika kila kitu hasa Mavazi "Dress to impress". Watanzania tunasubiri maelezo na AIBU hii haitarudia Tena

    ReplyDelete
  7. alafu hizo skafu za nini na joto la dar lilivyo kali disemba hii jamani?

    ReplyDelete
  8. Wabongo bwana! eti kuvaa 'suti kama wenzetu'. ubunifu zero - hata wa kubuni vazi rasmi la taifa ambalo sio lazima iwe suti ya Marekani au Ulaya- mnabakia kulilia vya 'wenzenu' wasio wenzenu. Mimi naona viongozi wa TFF hapa wamepiga ka-hatua kidogo ka ubunifu - 'sio lazima kufanya kila kitu kama "wenzetu"'. kazi nzuri TFF. Tukitoka hapo tunakuja na ubunifu wa hali ya juu ambao nasi "wenzetu" wataanza kutuiga!!!

    ReplyDelete
  9. suti ya nini? vijana hizo jinzi zimewakaa na misuli yao ya mazoezi.

    ReplyDelete
  10. NI KWELI JAMANI. PICHA KIAKILI MNAONAJE KAMA WANGEPIGA NGUO ZIMEFANANA. INGEKUWA NZURI KULIKONI HIVO WALIVOVAA.. MDAU AMETOA WAZO ZURI.HAWAJAKAZTAZWA LAKINI PICHA YA PAMOJA HUPENDEZA PALE MAVAZI YANAPOENDANA.

    ReplyDelete
  11. kwa nini hilo kombe hinapelekwa ikulu kwani ndo office za TFF zilipo hamia ?

    mdau paris

    ReplyDelete
  12. jamani hata suti za kushonesha wanashindwa kuwapatia hao vijana ! wanabaki kujitandika ma scarf IKULU ! sema kweli awajapendeza !

    mdau paris

    ReplyDelete
  13. hongereni staz kwa kuifunga ivory coast B issa michuzi usiibanie coment yangu kuwa mzalendo huo ndio ukweli ukitaka usitake.

    ReplyDelete
  14. Nani amesema kuwa suti ndiyo vazi rasmi9 la ikulu? Viongozi wa dini wakienda ikulu wanatakiwa wavae mavazi yao yanayowatambulisha kwa kazi zao, na vivyo hivyo wachezaji wanapoenda ikulu wanatakiwa wajitambulishe kwa mavazi yao ya uwanjani. Wanafunzi pia wanapoitembelea ikulu wanapendeza wakiwa na sare zao za shule na si suti.

    ReplyDelete
  15. Watanzania wacheni kukariri mambo suti siyo issue kumbukeni hao ni wachezaji hata wakienda ikulu na pensi inaeleweka,Mbona Paulsen hajavaa suti na anatokea huko umnapotaka tuwaige...jamani watanzania acheni Umbeya,Tumeona Ivory Coast walipokuwa wakialikwa Ikulu walikuwa wkienda na Jezi na bukta,inamaana wakina Drougba hawana suti.....Kama mmekosa cha kuandika bora mkaushe..WATANZANIA mnataka nini Team imeshinda badala ya kutoa maoni kuusiana na kiwango chetu cha mpira kilivyokuwa mna anza ku-discuss mavazi(suti)..Mbona vijana wametoka poa tena wametoka ki-Ikulu ikulu/wamevaa bendera ya tanzania...au mlitaka wavae suti yenye bendera ya tanzania..Acheni Ushamba.

    ReplyDelete
  16. Naamini kila national team na kila klabu za walioendelea wana vazi la suti ya klabu na taifa pia, mtoa mada wa kwa na wote waliopendekeza suti si swala la mazaha ni kitu muhinmu na heshima pia, so TFF wanatakiwa kubuni vazi rasmi la matukio kama hilo la kwenda ikulu na hafla mbalimbali.

    Mdau uliyesema kwani wanacheza bure wewe ni ziro kabisa hizi suti ni vazi rasmi analotakiwa kupewa mchezaji wa taifa.

    Walioendelea huvaaa wanaposafiri na kwenye hafla mbalimbali suti yenye bendera ya taifa na nembo ya shirikisho la soka sio kwenda na matangazo ya Tusker ikulu

    ReplyDelete
  17. Kuna miwatu injidai inasiasa kali ati suti ya nini, mbona jk amevaa? na analibusu kombe ni utamaduni wetu? kiukweli walitakiwa wawe nadhifu kama wachezaji wa nje wakienda kwenye shughuli kubwa wanaulamba hadi unawasau, kama wameamua kuiga igeni kiukweli sio nusunusu, na skaf ni utamaduni wa wapi huo? au dar kuna winter siku hizi. mngevaa kama mrisho mpoto ndio watu wanavyotaka, hii si swaziland suti wangependeza sana, kunyakua kombe si mchezo lazima mtoke kikweli, nawakilisha

    ReplyDelete
  18. kwakweli kuvaa jeans ikulu si sawa, maana hata mgeni ukiitwa Ikulu msaidizi anakushauri nguo za kuvaa unaambiwa "ukivaa za ajabu ajabu ikiwemo jeans hautaruhusiwa kumuona huyo unayemuhitaji" inamaana kuna mavazi yanayokubalika mle ndani "dress code". TFF mkaze buti next time muwe makini katika mavazi.

    ReplyDelete
  19. Nakumbuka Kibonde aliserma siku ya kuapishwa kwa mawaziri mpiga picha wake alikwenda ikulu na jeans akarudishwa mlangoni

    ReplyDelete
  20. Uajabu wa vazi la jeans upo wapi? Vijana wametinga Ikulu wamevaa sare za fulana zao za ubingwa na hakuna aliyevaa bukta. Hapajaharibika neno hapo. Haya mambo ya kuigilizia tu 'wenzetu' ndio tunaendelea kuliwa.

    ReplyDelete
  21. “Mbona Paulsen hajavaa suti na anatokea huko umnapotaka tuwaige...jamani watanzania acheni Umbeya,Tumeona Ivory Coast walipokuwa wakialikwa Ikulu walikuwa wkienda na Jezi na bukta,inamaana wakina Drougba hawana suti.....Kama mmekosa cha kuandika bora mkaushe..”

    HAYA NI MAWAZO FINYU YASIYOJENGA. HUYU NI MIONGONI MWA WATU WANAOIGA BILA MANUFAA.
    MFANO: WAJAPANI WANAVAA SURUALI FUPI KWENYE MAJALUBA ILI KUONDOA USUMBUFU WA KUKUNJA KUNJA SURUALI WAKIWA NDANI YA MAJALUBA YA MPUNGA. WATU KAMA MTOA MADA HAPO WANAWAIGA NA KUONA KAMA FASHENI, BILA KUELEWA MAANA. NA HAWA NDIYO WANAKUWA MBELE MBELE KUBEZA USHAURI WENYE BUSARA.

    WATANZANIA SISI NI MABINGWA SANA WA KUBEZA PALE TUNAPOPEWA USHAURI. NA HII INATOKANA NA MARA NYINGI KUTOJUA MAANA YA KILE KINACHOZUNGUMZIWA, UMAARUFU WAKE, NK. NA HASA KUTOJUWA KABISA IKULU NI NINI NA PANA HADHI GANI.
    IKULU NI MAHALI NYETI, MUHIMU NA PA KUHESHIMIKA. HIVYO NI BUSARA SANA KWENDA KWA MTINDO WA HADHI YAKE.

    TFF, CHANGAMOTO HIZO ZICHUKUENI.

    NAMKUMBUKA SANA BABU YANGU, AMBAYE WALA HAKUSOMA HATA DARASA MOJA. LAKINI SIKU MOJA ALINIAMBIA KUWA, "MJUKUU WANGU, FAHAMU KUWA ULIMI HAUTOI NENO LISILO NA SABABU" MIMI NAZINGATIA SANA USEMI HUU. NI NANI ANABISHA KATIKA HILI?

    TFF, ACHENI KUSIKILIZA MANENO YA WATU WASIO NA UPEO, BUSARA NA MABINGWA SANA WA KUBEZA. NAWASIHI, POKEENI USHAURI HALAFU UFANYIENI KAZI. KUMBUKENI KUWA HAKUNA NENO LISILO NA SABABU.
    DUNIANI KOTE WANAFAHAMU KUWA IKULU NI MAHALI NYETI SANA. MBONA IKULU ZA MACHIFU ZINAHESHIMIKA NA KUNA NAMNA YAKE YA KUINGIA?
    LAKINI, KAMA MTU ALIWAJIBISHWA KWA SABABU YA MITAMBO KUTOFANYAKAZI NA KUSABABISHA NYIMBO ZA TAIFA KUTOSIKIKA KATIKA UWANJA WA TAIFA, HILI MNALIBEZA VIPI?

    WATU WENGINE BWANA BURE KABISA; ETI “mbona Ivory Coast waliingia ikulu na bukta na jezi” Kwanza tayari unasema waliingia na bukta na jezi, huu tayari ni utaratibu; walikuwa na uniform rasmi za mpira. Maana yake walikuwa na mavazi yaliyofanana. Haya sasa ona jamaa zetu hapa, mwingine jeans, mwingine suruali mtepeto, mambo mchanganyiko tu. HATA HIVYO, KWANI IVORY COAST WANAFANYA MAZURI TUUU? INA MAANA KAMA WATAKUNYA KIWANJANI UTAWAIGA KWA KUWA DROGBA ANACHEZA ULAYA!! JAMANI HEKIMA HAZIPATIKANI ULAYA TU. TUIGENI MAZURI BASI. HALAFU TUACHENI KUBEZA WATU PALE WANAPOTOA USHAURI.

    TFF, KAZI KWENU, NAWASIHI SANA YAPOKEENI YALE MAZURI.

    ReplyDelete
  22. MDAU ALIEPENDEKEZA SUIT LABDA ALIMAANISHA "TRACK SUIT" ILI WAWE UNIFORM.............SIONI KOSA KWA WAO KUVAA TSHIRT ZA KUFANANA MAANA WAMEVAA KIMICHEZO.

    ReplyDelete
  23. Wenye akili hawakuvaa skaf wabongo mnachekeshaga kweli, hilo joto na skaf mzungu kagoma kawaona mlivyo malimbukeniu, kifupi hawajapendeza ng'oooooo ni bora wangevaa fulanaz tujue moja, wengine suruali za jeans wengine kitambaa brown black, yani vululuvululu, hapo aliyependeza ni jk tuuuuuu!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...