Umetolewa mwito kwa wastaafu wa utumishi wa umma kwenye ngazi za uongozi, kuendelea kuutumikia umma katika ngazi ya ushauri, kufuatia uzoefu wao wa muda mrefu kwenye utumishi wa umma, hivyo kubakia na uwezo wa kuona zaidi kuliko watumishi wanao waachia uongozi.
Mwito huo, umetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Philemon Luhanjo, wakati wa hafla ya kumuaga Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bibi Thecla Shangali, pamoja na wastaafu wengine wa tume hiyo, iliyofanyia jana usiku kwenye ukumbi wa Paradise City Club, hapa jijini Dar es Salaam.
Bwana Luhanjo amesema, wastaafu wa utumishi wa umma ni hazina kubwa sana kwa taifa na ujuzi wao na uzoefu wao bado unahitajika sana katika ngazi ya ushauri, hivyo amewashauri viongozi wa utumishi wa umma walio madarakani, kuhakikisha wanaitumia hazina hii, kwa kuwatumia wastafu wao kwa huduma za ushauri, ‘consultancy’ kila watakapo ona hali inaruhusu.
Kwa upande wao, Katibu Mstaafu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bibi Thecla Shangali, akizungumza kwa niaba ya wastaafu wenzake, alisisitiza kuwa tayari wakati wowote, kuendelea kuipa Tume ya Utumishi, ushauri wake kila atakapohitajika.
Bibi Shangali, ambae ametumikia utumishi wa umma wa takriban miaka 40, ameasema utumishi wa umma, unakabiliwa na changamoto mbalimbali na kuelezea moja ya changamoto kubwa za watumishi wa umma, ni maslahi duni, ukilinganisha na sekta binafsi.
Amewasisitiza watumishi wa umma, kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi, ili kuleta tija zaidi katika maeneo yao, itakayoongeza mapato ya serikali na kuijengea serikali uwezo wa kuboresha zaidi maslahi yao.
Pamoja na changamoto hiza za maslahi duni serikalini, Bibi Shangali, ameisifu serikali kuwa ndiye mwajiri bora zaidi kwa ajira yenye uhakika (job security),na mwenye mazingira bora kabisa ya kufanyia kazi, (working envirionment), vitu vinavyosababisha watumishi wa umma kufanya kazi kwa moyo wa kujitolea (job satisfaction) na hivyo wengi hata walio kwenye sekta binasfi, kutamani kupata kazi serikalini.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Jovin Kitambi, alimpongeza Bibi Shangali kwa utumishi uliotukuka wakati Kaimu Katibu wa Tume hiyo, Bw. Donald Ndagula akiahidi kuyaenzi mazuri yote yaliyofanywa na Bi. Shangali, ambaye ndiye muasisi wa Tume hiyo iliyoundwa upya kwa sheria mpya ya Utumishi wa Umma, number 8 ya mwaka 2002.

Tanzania Tanzania nchi yangu nakupenda sana tena najivunia sana kuwa Mtanzania lkn kitu kimoja tu unachonichosha nchi yangu NCHI HII NI YA KUONGOZWA NA VIKONGWE TU. Haya mambo hadi lini???? je VIJANA hadi leo miaka 49 ni TAIFA LA KESHO??? Hiyo KESHO itafika lini??? wakikimbia hao vijana UNASIKITIKA. AMKA TANZANIA AMKA acha vijana nao washike hatamu kama siyo PATAMU wanapopaona hao wazee na nchi hawataki kuiachia. Sasa vijana wanasomeshwa au wanasoma ili IWEJE????
ReplyDeleteMimi sasa nina umri wa miaka 48 nimekuwa nikiwasikia baadhi ya viongozi tangu nipojiunga na elimu ya secondari (around 35 years ago).
ReplyDeleteHao hao ndio wakuwa wakuu wa kila idara, shirika, wizarani, vyuoni, ofisi za ubalozini n.k.
Mpaka sasa nakaribia kuachia ngazi wao bado wanaendelea hivi walianza kazi na umri gani na mpaka sasa wana umri gani?
Sishangai kuona mambo hayaendi kabisa...Africa watu mpaka wafie ofisi nyumbani hakukaliki....wanakwenda job mpaka wakati wa eid na Chrismas....na shughuli ni moja tu michogo.
Dunia imebadilika sana tunahitaji vichwa ambovyo haviogopi mabadiliko, havikasiriki kusahihishwa/kukosolewa na jamii.
HABARI NDIO HIYO KWA WALE WANAOFURAHIA BABA YAKE NANI KASTAAFU AU MAMA YAKE NANI . HAWASTAAFU NG'O . NCHI ITAJENGWA NA WAZEE . SISI VIJANA TUMEZOEA PESA ZA HARAKAHARAKA NA MAISHA YA JUU. PESA YA SERIKALI TUTAIWEZA TUSIJE TUKAFILISI NCHI BURE
ReplyDeleteYes, wastaafu wa utumishi wa umma continuously coaching and mentor the NEW Tanzanian leaders.
ReplyDeleteKwa kweli hii ni disapointment, serikali iache siasa za kusema eti kuwatumia wastaafu katika ushaurio. Ukisha staafu uwe umestaafu nchi ina watu zaidi ya milion 40, Bw. Luhanjo unatakiwa ujenge utumishi wa umma kwa kuwaandaa viongozi wa baadaye watakaochukua madaraka mara mtu akistaafu...succession plan ndiyo suluhisho la kuacha kuwakumbatia wastaafu. Ukistaafu hata akili yako inakuwa imechoka...
ReplyDeleteKama ukistaafu na hakuna anayeweza endelea na kazi zako basi ujue huyo mstaafu alikuwa na matatizo...
kwa ufupi ni lazima tuwe na utaratibu wa kuwa na kizazi endelevu katika kazi
Ukistaafu (retired public servants) akili is excited...inafurika na uzoefu wa kazi, service, implementation of succession plan na mengineyo. Aside of continuing COACHING and MENTORING the new Tanzanian leaders uko tayari na the next project. It all works out well like a well-oiled machine.
ReplyDeleteKAMA HAMUELEWI NI HIVI . MAKATIBU WAKKU WANAITWAGA PERMANENT SECRETARY ( WAKISTAAFU WANAPEWA VYEO VINGINE KAMA WENYEKITI WA WIZARA , UBALOZI , NA MKUBWA WA TUME FULANI HIVI , UNITED NATION INAWASUBIRIA NA MATAIFA MENGINE ) .
ReplyDeleteMNALO HILO WENGI WAO WANAKUWA MABALOZI OKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKKK
OBAMA ALIVYOINGIA MADARAKANI ALIWACHAGUA WOTE WA CLINTON WAZEE WENGINE . RAISI NI MWANASIASA VILEVILE SASA LAZIMA AWAEWEKE WATU ANAOWAFAHAMU NA MARA NYINGI SANA HATA MARAISI WA MAREKANI NA WOTE WANAWAWEKA WATU ALIOSOMA NAO AU MARAFIKI .
ReplyDeleteRAISI NI MWANASIASA MWANANGU
Nyie vijana mbona MNACHONGA sana......WAT IZ YUA PROBLEM?.......chapeni kazi bwana.....mambo yanaenda kwa kufuata kanuni na taratibu za kiutendaji.....mlikuwa mnatakaje kwani?
ReplyDeleteMimi nashauri tuwe makini na hawa watu tunaowaita washauri. Jamani nchi yetu tusijilinganishe na America ambapo wazee wa sasa walikuwa kwenye uongozi wakati nchi iko katika technological advancement.
ReplyDeleteNchi yetu kwa upande mwingine hawa wazee ndio walikuwa viongozi vijana miaka ile ya 47, nikisema hivyo hope mnaelewa nchi ilikuwa katika hali gani.
Sasa tunavyowatumia kwa ushauri? ni ushauri upi haswa. Sasa hivi tunatakiwa kusonga mbele na sio kurudi nyuma. Tunavyowatumia wazee hawa ambao hawajawa exposed katika ulimwengu wa maendeleo halisia yanayosukumwa na technology tunakosea. Mimi kwa mawazo yangu ni kama wanaturudisha nyuma. Labda tu ushauri wa kuishi bora na watu sio ushauri wa vipi tupange mipango ya maendeleo, mawazo watakayotupa ni ya miaka ile ya 47, na wengi tunajua Tanzania tulikuwa wapi.
Na mimi sidhani kama inafaa,mfano angalia viwanda vingapi viliyokuwa chini ya serikali vyote vimefilisika na vingi ni magofu, halafu mnawachukua waliokuwa viongozi ama waziri, au mkurugenzi eti kuwa mshauri..give me a break!!! Tanzania tusipoacha kuendekeza hizi tabia za kupeana sifa za uongo wakati ukweli unajulikana maendeleo yetu daima yatasuasua.
Sasa hivi ziwe zi zama za ukweli na uwazi kihalisia, kama waliboronga tuachane nao and we have to move forward...
WEWE HAPO 8;20 AM UNAONEKANA NGENI SANA WA MAMBO , HAWA WATU MAMBO YA TECHNOLOGIA YALIVYOOANZA WALIENDA MAREKANI COURSE KWA TAARIFA YAKO . MZAZI WANGU MIMI ANATYPE NA EXCEL ,ACCESS , POWER POINT AND ALL THAT MWENYEWE HAKUNA SECRETARY HAPO WIZARANI NA NI KATIBU MKUU POLE . NA SASA HIVI NAONGEA NA MZAZI WANGU KWA SKYPE AND ALL THAT NA WAFANYAKAZI WA NGAZI ZA JUU WANA BLACKBERRY KWA TAARIFA YAKO FUPI NA LAPTOP UNALO HILO . WIVU TU
ReplyDeleteAnon 08:20, Mchoree Mr. Yew hiyo scinerio ya miaka ile ya 47 uoneatakavyocheka sana ha ha ha na kunenepa kama tembo mkubwa. Huyu ndio naye alikua kijana miaka ile ile ya 47. Nchi hiyo ilikua katika hali gani? PAMOJA na new leadership ya vijana na 'not so vijana' katika nchi yake wanamtumia Mr. Yew kwa ushauri wake - wa aina yake - haswa haswa. Wanamuita MINISTER MENTOR Lee Kuan Yew. Kwaajili ya mchango wake mipango na maendeleo ya Singapore yanaendelea kukua na kusonga mbele zaidi. Na hayo mawazo anayotoa ni ya mtu kuanzia miaka ile ile yale yale ya 47 mpaka leo, albeit ataendelea kutoa ushauri mpaka siku ile atakayo pumua pumzi yake ya mwisho. Tusipoachana kuendekeza hizi tabia za baadhi ya watu wanao-practice the worst kind of intellectual thuggery maendeleo ya watu daima yatasuasua. Break or no break, eti former prime minister kuwa mshauri? haya waone wa-Singapore walivyo makini (overused word) na wanavyo-move forward…
ReplyDelete