TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION OF BANGALORE
Uongozi wa waTanzania waishio Bangalore India chini ya Mwenyekiti Jumanne Rajabu Mtambalike (pichani) tunaungana na waTanzania wote walioko India na ulimwenguni kwa ujumla kusherekea sikukuu yetu ya uhuru.
Ndani ya miaka hii 49 ya uhuru na amani tunaipongeza serikali ya Jamhuri ya muungano waTanzania chini ya Muheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Pia tunakumbusha idara usika kwamba tovuti ya serikali kuu” http://www.Tanzania.go.tz“ inasumbua kupatikana kitaalamu ina DOS (Denial of service) na siku kama hizi ndio watu wanaitembelea sana hivyo wajitahidi kufanya iwezekanavyo iwe hewani haraka iwezekanavyo kwani tunakosa kuitangaza nchi yetu.
Tunakumbusha wanajumuiya wa TASABA sherehe ya miaka 49 ya uhuru Bangalore itakua ukumbi wa (WHITE TIGER –KAMANNALI JUMAMOSI HII) na JUMAPILI kutakua na bonanza la michezo ACHARYA COLLEGE kwa ajili ya uhuru karibuni wote.
Mwenyekiti TASABA
Jumanne R.Mtambalike.
+919901837490
mtambalike@yahoo.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...