Kipoyane Laiboni-Karatu


NA MWANDISHI WETU

WAREMBO sita wa Mkoa wa Arusha na mmoja kutoka Karatu, wamefanikiwa kufuzu katika mchujo wa kumsaka Kisura wa Tanzania 2010/11 uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii, ikiwa ni awamu ya pili ya mchakato huo ambao fainali zake zinatarajia kufanyika Machi mwakani.

Mwenyekiti na Mwazilishi wa Kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), waandaaji wa shindano hilo, Juliana Urio, aliwataja wasichana hao kutoka Arusha kuwa ni Dotinata Soro, Glory Ephrahim, Naomi Meckon, Neema Kirango, Neema Selle na Susan Manoko. Na kutoka Karatu ni Kipoyane Laiboni.

Alisema kwamba katika mchujo huo uliofanyika Via Via Club kwa siku moja,Jumanne, na baadaye kuelekea Karatu ambako mchakato huo ulikuwa ukifanyika mitaani (boma kwa boma), wasichana wengi walijitokeza kujaribu bahati yao, lakini ni hao tu waliokidhi vigezo vinavyotakiwa katika mashindano hayo.

“Tumefarijika mwitikio wa wasichana wa Arusha ulikuwa ni mzuri sana kwani tulipata wasichana zaidi ya 50 ambao wengi wao walikua katika ubora wa hali ya juu. Tunaamini mashindano ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake,” alisema Urio.Urio alivitaja vigezo vinavyotakiwa katika shindano hilo kuwa ni urefu wa sentimita 174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.

Alisema kuwa baada ya kufanya mchujo huo Arusha na Karatu, Jumanne na Jumatano, timu ya Kisura itaelekea mkoani Dodoma, kabla ya kuhamia Iringa, Mbeya na Ruvuma, Januari 3 hadi 7, ikiwa ni awamu ya tatu na ya mwisho.

Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa ni Family Health International (FHI), na wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni mzuri sana sikatai....ila je ataiweza ile miondoko ya PAKA na lugha jamani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...