Here below is a Home Office update and we hope you will participate in the survey intended to bring significant changes to the Home Office Visa regulations. Some of the changes include withdrawing the previledge of extending your visa while in the UK and closing completely the post-study permit route. Please note that your participation in this survey will in one way or another contribute to the efforts against these premature changes.

Director Of Communication
CCM Branch -Reading ,Berkshire .United Kingdom
Telephone No:+447876126862

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wewe kama mgeni hapo UK huna haki yoyote ya kumwambia serikali ya Uingereza afanye nini kuhusu maswala ya wageni nchini Uingereza.

    Kazi yako ni kufuata masharti na sheria za nchi za watu sio kupinga. Haki hio ni haki ya Raia wa Nchi sio Mgeni, kama nchi yoyote duniani.

    ReplyDelete
  2. Elimu ya UK imekwishapitiwa na wakati. Maprofesa wabaguzi, ukiwa mgeni unalipishwa kodi kubwa, hizo kazi za kubeba box kwenye theluji mishahara midogo na zinavunja uzazi. Sijui kitu gani kinachowafanya watu wanganganie kwenda!

    ReplyDelete
  3. Jamani jamani, Mimi si msomi nina ka-masters degree tu lakini, Elimu ya UK imepitwa na wakati...unaweza ukanihakikishia hilo? Mdau alichotaka ni "survey" sijui kuwa mdau anonym wa 03:01:00pm unaona shida gani watu wengine wanapong'ang'ania kwenda au kuishi UK. Kila mtu ana haki ya kuishi na kufanya anachotaka mradi tu asivunje sheria...Jamani jamani tuache chuki...tuzingatie mawazo ya kujengana kimaisha na siyo kubomoana tu kwa kila kitu... Heri ya X-mass na mwaka mpya wadau wote wa blog ya Michuzi.

    ReplyDelete
  4. Ndugu yangu inaonyesha unahamu kubwa ya kusoma UK. Sasa tafauti ya UK na Bongo ni lugha tu, maprofesa wa kibongo bora zaidi kuliko wa UK, utafahamu vizuri, hawakubagui, aliyesoma bongo anapata vitu vingi kuliko wa UK. Profesa wa UK anahikikisha unafaulu lakini huondoki na elimu. Nakila ukiwa Mwafrika ndio kabisa. Fieldwork huendi na kama ukienda basi kwenye makampuni huko hawakuonyeshi kitu. Kama unasoma kwa utafiti basi wale wasimamiaji wa eneo ulilochagua watakukwepa, utaishia wasimamiaji ambao wako kwenye utawala au wakuu wa idara, na ambao hawana ujuzi na eneo la utafiti wako. Lakini kama unataka uende UK kwa kupata hizo raha za ughaibuni na kutajirika basi jaza hiyo survey.

    ReplyDelete
  5. Michuzi, this consultation is for British people, not us.

    ReplyDelete
  6. we chizi ulietoa coment hapo juu eti elim ya uk imepitwa na wakati hauna akili timamu kama ya uk imepitwa na wakati basi ya bongo itakua mara mbili sababu mpaka leo tunafuata silabus kutoka uk udsm inasimamiwa na university of london mpaka leo hii ni hicho ndo chuo mnacho kiheshim bongo, na kwa mtoa taarifa na wewe ni desgrace kwa nini unataka watanzania wandelee kubaki huk bora wafute hio PSW yao co mijitu imamimasters bado utakuta imegangamaa huku inafanya mikazi ya kishenzi SECURITY, CLEANER, NI ni upuuzi mtupu uk wafute mrudi mfanye kazi za maana

    ReplyDelete
  7. mdau wa Wed Dec 22, 05:53:00 PM unayosema unaushahidi wowote? usjiekuwa unachanganya vyuo vya kweli kweli na vile vya kubabaisha wabongo wanavyokimbilia ili wapate wasaa wa kupiga boksi la uhakika!

    Mimi nimesoma uk, field nimefanya IBM portsmouth na baada ya kumaliza masomo yangu barclays bank na royal mail wote walinipa offer ya kazi. Si mimi tu kuna watanzania wawili na waafrika wengine wanne ambao wamemaliza masomo yao ya udaktari wa watoto, field zao zilikuwa Guys hospital amabayo ni moja ya hospitali kuu za watoto hapa uk. Na sasa wote wanafanya kazi katika hospitali mashuhuri hapa london.

    Katika intake yangu kulikuwa na vijana kama 25 wa kiafrika na wote tulienda field baada ya mwaka wa pili wa masomo, hakuna hata mmoja ambae aliporudi field alielalamika lolote, sote tulitembelewa na field tutors wetu kwa idadi sawa na wanafunzi wengine na wote tulianza final project zetu tukiwa field. Hii ni kudhihirisha kuwa kampuni tulizokwenda field zilikuwa zinatu-treat sawa.

    tatizo la watanzania wengi ni uvivu, wakitakiwa kujituma zaidi ni haraka sana wanatumia karata ya ubaguzi.

    kuna mtanzania tulikuwa nae university pamoja, yeye akisoma architecture, kila mtu anajua ugumu wa kozi hii na namna kila mwanafunzi wanavyojituma, muda mrefu wanatumia kwa assignments na tutorials kuliko lectures. Huyu ndugu yetu akawa anatumia muda mwingi wa tutorial na projects kwenda pubs na kuparty, matokeo yake akatakiwa kurejea mwaka, sote hatukushangaa isipokuwa yeye na kuanza kuleta kilio cha ubaguzi.

    ReplyDelete
  8. UK wanauhaba wa madaktari na Computing personnel. Unaweza kumaliza Bongo ukapata kazi kwenye maeneo hayo au ukamaliza UK ukapata kazi pia. Kama ni hodari wa fani uliyosomea basi chuo chochote kile duniani utasoma na bado utakuwa hodari. Kufanyakazi Barclays au hospitali mashuhuri duniani ambayo hatujui unachokifanya tutaingiwa na wasiwasi. Kazi kubwa utayofanya benki kama ni computing itakuwa ni IT support ambayo ni kiwango cha chini kabisa cha computing. M-UK sio mjinga akakupa kazi ya Surgeon wakati ndio kwanza umemaliza kusoma. Sana utakuwa juniour doctor. Baada ya miaka mitano waliofanya kazi bongo wana-experience kibao na wanakula vizuri kuliko wewe unayeng'ang'ania UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...